Uamuzi wa kesi inayomkabili rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak
kuhusu mashtaka ya ufisadi na mauaji ya waandamanaji wakati wa mapinduzi
ya mwaka 2011 umeahirishwa.
Jaji alisema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na sahabu ya kuwepo kwa ushahidi ambao bado mahakama haijausikiliza.
Wakati wa kesi ya leo kanda moja ya video ilionyesha mrundiko wa stakabadhi za ushahidi.
Bwana
Mubarak alipatikana na hatia mnamo mwaka 2012 na kuhukumiwa kifungo cha
maisha gerezani lakini baadaye hukumu hiyo ikabatilishwa.
Mahakama hiyo imesema kuwa itatoa hukumu yake mwezi Novemba. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment