Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila
Odinga ameeleza kuwa bila ya Pasipoti ya Tanzania aliyopewa kwa msaada
na Mwalimu Julius Nyerere asingeweza kwenda Ujerumani kusoma baada ya
Idara ya Uhamiaji ya Kenya kumnyima hati hiyo ya kusafiria.
Odinga ambaye hivi sasa ni kiongozi mkuu wa Muungano wa Cord ameeleza hayo katika kitabu chake kiitwacho The Flame of Freedom, ambamo ameelezea historia yake na familia yake katika mambo mbalimbali.
Idara ya Uhamiaji ya Kenya ilimnyima Odinga hati hiyo kutokana na Serikali ya kikoloni kuzuia hati ya baba yake, mzee Jaramogi Odinga kwa sababu alitembelea nchi za Urusi na China zilizokuwa maasimu wakubwa wa nchi za Magharibi.

Hata hivyo, Mzee Jaramongi aliamua kusafiria hati ya kimataifa alizopewa na Kwame Nkurumah wa Ghana, pamoja na Gamel Abdel Nasser wa Misri.
Odinga alihitaji hati hiyo kwa kuwa baba yake alitaka amalizie masomo yake nchini Ujerumani baada ya kukatishwa masomo akiwa kidato cha pili mwaka 1962 katika Shule ya Maranda.
Katika kitabu hicho, Odinga alisema hakushangaa kunyimwa hati hiyo.