Monday, October 14, 2013

AU YATAKA ICC IAHIRISHE KESI YA KENYATTA


131013212235_kenyattareuters_043c3.jpg
Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika uliofanyika Ehiopia umetaka mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai (ICC) huko The Hague icheleweshe kesi ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, iliyopangwa kuanza kusikilizwa Novemba mwaka huu.
AU pia wamekubaliana azimio linaloeleza kuwa hakuna kiongozi mkuu wa taifa la Afrika aliyeko madarakani atakayefikishwa katika mahakama hiyo.
Wakati viongozi wa Kenya na Sudan wakikabiliwa na kesi huko ICC, viongozi wa nchi za Afrika wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu kuwa mahakama hiyo inafanya upendeleo na kuwaonea kwa makusudi.
AU ilijadili uwezekano wa nchi wanachama kujitoa, lakini wazo hilo halikuungwa mkono kiasi cha kutosha.
Wanasiasa na wanadiplomasia waandamizi akiwemo aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan wamekosoa mpango wa kujitoa kutoka ICC. Tembelea jambotz8.blogspot.com kila siku.
Kucheleweshwa
Viongozi hao wa AU, waliokutana Addis Ababa, walikubaliana kuwawekea kinga ya kutoshitakiwa kiongozi yoyote wa taifa la Afrika.
Pia wameitaka Kenya iandike barua kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataiga kuomba ucheleweshwaji wa kesi katika mahakama ya ICC dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya jinai.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...