Sunday, October 13, 2013

IVORY COAST WAIFUMUA SENEGAL 3-1 NA KUBISHA HODI KOMBE LA DUNIA

WASHAMBULIAJI Didier Drogba, Salomon Kalou na Gervinho wote wamefunga jana Ivory Coast ikiifumua 3-1 Senegal na kuongeza matumaini ya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwakani.Drogba alifunga kwa penalti dakika ya tano, kabla ya winga wa zamani wa Arsenal, Gervinho kufunga la pili dakika tisa na baadaye kipindi cha pili Salomon Kalou akafunga la tatu mjini Abidjan.
article-2456451-18B3202400000578-136_634x423_49689.jpg
Tembo wauwaji: Wachezaji wa Ivory Coast wakishangilia ushindi wao leo
Sasa Ivory Coast watahitaji sare au kufungwa si zaidi ya wastani wa bao moja katika mchezo wa marudiano moja ili kujikatia tiketi ya Brazil mwakani. Seneal yenyewe itahitaji kushinda 2-0 tu nyumbani, ili kujihakikishia kurejea Fainali za Kombe la Dunia.
article-0-18B2FA6200000578-877_634x446_38bb0.jpg
Didier Drogba ameifungia Ivory Coast leo
article-2456451-18B3209700000578-178_634x453_e3f22.jpg
Salomon Kalou na Drogba walicheza pamoja Chelsea miaka kadhaa
article-2456451-18B3D49200000578-154_634x416_2ec82.jpg
Umefanya vizuri: Gervinho akizungumza na kocha Sabri Lamouchi baada ya mechi
Bao pekee la Senegal lilifungwa na Papiss Cisse dakika tano kabla ya filimbi ya mwisho.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...