Sunday, October 13, 2013

SINTOFAHAMU WAIZARA YA HABARI.....!!!


makala dca7a
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla, jana alitoa taarifa kwa umma akieleza bayana kwamba yeye ndiye aliyeliruhusu gazeti hili kuendelea kutolewa kwa njia ya mtandao (online) na Gazeti la Rai kutolewa kila siku.
Makalla alitoa ufafanuzi huo muda mfupi baada ya Idara ya Habari-Maelezo kutoa taarifa kwamba Serikali imesikitishwa na Gazeti la Mwananchi na gazeti dada la Rai, Mtanzania kukiuka masharti ya adhabu walizopewa.
Septemba 27, mwaka huu Serikali iliyafungia Mwananchi kwa siku 14 na Mtanzania siku 90.
Wakati likianza kutumikia adhabu yake, Mwananchi ambalo tayari limemaliza kuitumikia, liliendelea kutoa taarifa kwenye tovuti yake wakati Kampuni ya New Habari (2006) Ltd ambayo inamiliki Mtanzania ilianza kuchapisha kila siku gazeti la Rai ambalo awali lilikuwa likichapishwa kila wiki.
Katika ufafanuzi wake alioutoa
jana Makalla alisema: "Nimelazimika kueleza haya baada ya taarifa mpya ya Idara ya Habari-Maelezo iliyohoji uhalali wa gazeti la Mwananchi kuwa online (mtandaoni) na gazeti la Rai kutoka kila siku, badala ya mara moja kwa wiki (Alhamisi)."
Katika ufafanuzi wake Makalla alisema kuwa Oktoba 4 mwaka huu, alifanya mazungumzo na viongozi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) na New Habari Corporation (2006) Limited na Msajili wa Magazeti na kwamba katika kikao hicho yaliwasilishwa maombi matatu.
"Waziri aliombwa kupitia upya adhabu iliyotolewa kwa magazeti hayo. Katika hili majibu yangu niliwaambia kwamba mwenye mamlaka juu ya suala hilo ni waziri mwenye dhamana na masuala ya habari pekee," alisema.
Kuhusu gazeti la Mwananchi kuwekwa katika mtandao, Makalla alisema naibu msajili wa magazeti alisema kuwa hakuna sheria yoyote inayoweza kuzuia gazeti hilo kuwa mtandaoni, lakini aliwataka lisionekane gazeti zima kama lilivyo, pia wabadili nembo ya gazeti na kuweka ya MCL.
"Baada ya maelezo hayo niliridhia gazeti hilo liwe mtandaoni kwa kuzingatia angalizo lililotolewa na naibu msajili wa magazeti," alisema Makalla.
Kuhusu Rai kutoka kila siku, alisema kuwa awali Kampuni ya New Habari iliwahi kuomba kwa maandishi kwamba gazeti la Rai litoke kila siku ambapo naibu msajili wa magazeti licha ya kukiri kulikuwa na tatizo la kiufundi katika kurejea maombi hayo, alisisitiza kuwa hakuna kinachozuia gazeti hilo kutoka kila siku.
"Niliruhusu Mwananchi na Rai kuendelea na mambo yote niliyoyaeleza baada ya kuridhika kwamba hakukuwa na ukiukwaji wa sheria yoyote uliofanywa na waombaji," alisisitiza.Alisema ameamua kuweka sawa jambo hilo kutokana na taarifa ya Idara ya Habari Maelezo kutolewa bila kuwepo kwa mawasiliano kati yake na waziri, naibu waziri wa wizara hiyo pamoja na naibu msajili wa magazeti.
"Ndiyo maana kuanzia Oktoba 10 mwaka huu, gazeti la Rai lilianza kuchapwa kila siku na kusambazwa, gazeti la Mwananchi likaanza kuwa mtandaoni kwa kuzingatia maelekezo ya naibu msajili wa magazeti," alisema.
Ziafutazo ni taarifa mbili zinazokinzana za serikali;-
TAARIFA YA NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO, MH. AMOS MAKALLA KWA VYOMBO VYA HABARI
Napenda kuufahamisha umma kwamba mimi ndiye NILIYERUHUSU Gazeti la Mwananchi kuendelea na utoaji wa taarifa/habari kwenye tovuti yake, pia Gazeti la Rai kutoka kila siku.
Ninalazimika kutoa ufafanuzi kwa njia ya maandishi kutokana na kupigiwa simu nyingi na waandishi wa habari kuhusiana na tamko jipya la Mkurugenzi wa Habari – Maelezo, Ndg xxxxxxxxx kuhoji uhalali wa Gazeti la Mwananchi kuwa online na Gazeti la Rai kutoka kila siku, badala ya mara moja kwa wiki (Alhamisi).
Tarehe 4/10/2013 nilifanya mazungumzo na viongozi wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd (MCL) na New Habari Corporation (2006) Ltd kwa upande mmoja na msajili wa magazeti kwa upande mwingine.
Katika kikao hicho cha pamoja na viongozi wa Magazeti ya Mwananchi na Mtanzania maombi matatu yaliwasilishwa;
1. Ombi la kumuomba waziri apitie upya adhabu iliyotolewa kwa mageazeti hayo. Katika hili Majibu yangu niliwaambia kwamba mwenye mamlaka juu ya suala hilo ni waziri mwenye dhamana na masuala ya habari pekee.
2. Ombi la Gazeti la Mwananchi kuwa online na Gazeti la Rai kutoka kila siku badala ya kutoka siku ya Alhamis.
2.1 New Habari walieleza kuwa siku zilizopita waliwahi kuomba kwa maandishi (barua) kwamba gazeti la Rai litoke kila siku. Maelezo ya Naibu Msajili wa Magazeti katika kikao hicho yalikuwa kwamba, kulikuwa na tatizo la kiufundi katika kurejea maombi hayo na akakiri kuwa hakuna kinachozuia gazeti la Rai kutoka kila siku. Kutokana na maelezo hayo mimi niliridhia gazeti hilo sasa liruhusiwe kutoka kila siku.
2.2 Kuhusu gazeti la Mwananchi kuwa online, Naibu Msajili alisema hakuna sheria yeyote inayoweza kuzuia gazeti hilo kuwa onlineila aliwataka lisionekane gazeti zima kama lilivyo pia wabadili nembo (Master Head) kwamba waweke nembo ya MCL na siyo ya gazeti husika ambalo limefungiwa. Pia baada ya maelezo hayo niliridhia gazeti hilo liwe mtandaoni kwa kuzingatia angalizo lililotolewa na Naibu Msajili wa Magazeti.
3. Hoja ya tatu ilikuwa ni ile ya Serikali kupitia Idara ya Habari - Maelezo kuwa na uhusiano mzuri na vyombo vya habari, ili kuepuka misuguano isiyo ya lazima.
3.1 Pendekezo hili nililipokea na niliwasilisha kwa Mhe Waziri wa Habari kwa hatua zaidi, likiwamo suala la kupitia upya adhabu na ushauri wa kujenga uhisiano na vyombo vya habari.
3.2 Masuala ya Gazeti la Mwananchi kuwa online na Rai kutoka kila siku, NILILITOLEA UAMUZI siku hiyo hiyo, na uamuzi ni kwamba niliwaruhusu baada ya kuridhika kwamba hakukuwa na ukiukwaji wa sheria yoyote uliofanywa na waombaji.
Nimeamua kuweka sawa jambo hili kutokana na taarifa ya Mkurugenzi wa Maelezo ambayo ninaamini kwamba kutolewa na kusambazwa kwake ni kukosekana kwa mawasiliano kati yake kwa upande mmoja na Mhe. Waziri, Naibu waziri na Naibu Msajili wa Magazeti kwa upande mwingine.
Hivyo aliyeruhusu Gazeti la Mwananchi kuwa online na Rai ni mimi na ndiyo maana kuanzia tarehe 5/10/2013 Gazeti la Rai lilianza kuchapwa kila siku na kusambazwa, na Gazeti la Mwananchi likaanza kuwa mtandaoni kwa kuzingatia maelekezo ya Naibu Msajili wa Magazeti.
Imetolewa na:
Amos G. Makalla
Naibu Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MichezoIdara ya Habari – MAELEZO, inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kwamba Mheshimiwa xxxxxxxx Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo amepokea maombi kutoka kwa wamiliki wa Magazeti ya Mwananchi na Mtanzania wakiomba kupunguziwa adhabu au kusamehewa adhabu wanazozitumikia kuanzia 27 Septemba, 2013.
Wakati Mheshiwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo anatafakari maombi hayo, amesikitishwa kuona kwamba magazeti haya mawili yamekiuka masharti ya adhabu walizopewa.
Wamiliki wa Gazeti la Mtanzania baada ya kufungiwa wameamua kuligeuza gazeti la kila wiki la RAI kuwa la kila siku bila ya kibali cha Msajili wa Magazeti. Kwa mujibu wa ratiba ,gazeti la RAI linapaswa kutoka kila siku ya Alhamisi.
Wamiliki wa gazeti la Mwananchi nao wameendelea kuchapisha gazeti hilo katika mtandao kinyume na agizo la kufungiwa.
Serikali inawataka wamiliki wa vyombo habari nchini kuwa na utamaduni wa kutii sheria za vyombo vya habari zinazotumika wakati huu. Hivyo serikali kwa mara nyingine tena inawataka wamiliki wa Gazeti la MTANZANIA, kuzingatia ratiba yao ya kutoa gazeti lao kila siku ya ALHAMISI.
Aidha, serikali inawataka wamiliki wa Gazeti la Mwananchi kuacha mara moja kuchapisha gazeti lao katika mtandao kama amri ya kufungiwa ilivyoanisha.
Imetolewa na,
Idara ya Habari – MAELEZO
10 Oktoba, 2013
11 Oktoba 2013: CHANZO MWANANCHI.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...