Tuesday, October 15, 2013

KLABU 7 ZATAWALA UBINGWA WA SOKA TANZANIA BARA

vodacom_premier_league_1497c.jpg
Na DANIEL MBEGA
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea kutimua vumbi katika harakati za kutafuta bingwa katika mwaka wake wa 49 tangu harakati za kutafuta klabu bingwa zilipoanza mwaka 1965.
Mikiki mikiki yote hii isingekuwepo leo kama lisingekuwa wazo la kocha

wa Taifa Stars wa wakati huo, Milan Celebic wa Yugoslavia, alilolitoa mwaka 1964 kama njia ya kusaidia kuchagua wachezaji wa timu ya taifa badala ya kutegemea michuano ya Sunlight Cup (sasa Taifa Cup).
Badala ya michuano ya Sunlight iliyohusisha klabu na timu za Majimbo, Celebic aliona kulikuwa na umuhimu wa kuwepo mashindano ya klabu pekee katika ngazi ya taifa na siyo yale ya mkoa, hasa wa Pwani (Dar es Salaam ya sasa), hivyo 'akaliuza' wazo lake kwa Chama cha Ligi ya Soka cha Dar es Salaam (DFLA) ambao walianzisha mashindano hayo mwaka 1965 yakijulikana kama Ligi ya Taifa.
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa TFA (TFF) uliofanyika kati ya Desemba 19-20, 1964 (Jumamosi na Jumapili) katika Ukumbi wa Arnautoglou mjini Dar es Salaam ndio uliojadili pamoja na mambo mengine, uanzishwaji wa Ligi ya Taifa. Tembelea jambotz8.blogspot.com na kenypino.blogspot.com kila siku.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...