Thursday, July 25, 2013
Wednesday, July 24, 2013
RAIS KIKWETE AWASILI BUKOBA, AKUTANA NA TAIFA STARS MWANZA, AWATAKIA USHINDI DHIDI YA UGANDA
Jakaya Mrisho Kikwete akifungua jengo la Kagera Coperative Union leo Julai 24, 2013
mjini Bukoba.
mjini Bukoba.
Picha ya Pamoja
MBONA MAJANGAAAAA: ALIKIBA NAE ATIWA MBARONI NJE YA NCHI... KISA ........!!!
Meneja wake Guru akiongea na mama yake Ally Kiba nyumbani kwao Kariakoo amesema bwana mdogo alikuwa uwanja wa ndege wa Amsterdam akisubiri ndege za American Airlines ili aelekee jijini Oklahoma City USA akiwa na mwanamama maarufu mwenye mvuto hapa bongo ndipo alipokamatwa.
Haijajulikana sababu za kukamatwa kwake na mpaka leo familia wapo kimya hawajafunguka na wanailinda habari isivuje japo baadhi ya wadau washazinasa. Haijajulikana sababu za kukamatwa ila mpaka kesho media zitatuambia sababu. Sina hakika kama kisa cha kukamatwa bwana Singleboy ni kitu cha Sembe au laaaaa!!! TUSUBIRI
HII NDIO PARTY TWO YA BIFU LA IRENE UWOYA NA LUCY KOMBA...!!!
NYOTA wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya ‘Mama Krrish’ ametoa kali ya mwaka baada ya kudai kwamba amemshika ugoni msanii mwenzake, Lucy Komba mara baada ya kuziona picha za msanii huyo akiwa na mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ wakiigiza filamu. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kutokea nchini Swaziland, Uwoya amepinga vikali utetezi unaosemwa kwamba Lucy na Kataut walikuwa wakishuti filamu na anaamini kuwa msanii huyo ameamua kumzunguka na kutaka kuibomoa ndoa yake. “Lazima kuna kitu kinaendelea kwani katika dunia hii sijawahi kuona filamu inayochezwa na watu wawili tu mwanzo mpaka mwisho, ninachotaka kusema ni kwamba Lucy ana mpango wa kuiharibu ndoa yangu,” alisema Uwoya kwa hasira.
Uwoya amehoji usiri wa filamu hiyo na kila alipokuwa akimpigia simu mumewe alikuwa akimjibu kwamba yuko Rwanda kumbe alikuwa Bongo akiigiza filamu na Lucy. “Kwanza Lucy ashukuru niko mbali, laiti ningekuwa karibu angenieleza vizuri kwa sababu hata yeye angeweza kunipigia simu na kunifahamisha ushiriki wa mume wangu kwenye filamu hiyo kwa kuwa namba zangu anazo, ilikuwaje hakufanya hivyo?” alihoji.
Kuonesha kwamba amechukizwa na kitendo hicho, Uwoya alisema kwamba akitua Bongo atamtafuta Lucy ili aweze kumshughulikia vizuri na ikiwezekana amuoneshe hiyo filamu waliyoigiza watu wawili tu. “Nitatua Bongo siku si nyingi na cha kwanza ni kumtafuta Lucy, anieleze vizuri kuhusu filamu hiyo waliyocheza na mume wangu,” alisema Uwoya. Filamu hiyo ambayo imekuwa maumivu makubwa kwa Uwoya, imechezwa na Lucy na Ndikumana tu mwanzo hadi mwisho na imepewa jina la Kwa Nini Nisikuoe
STARS YAMALIZA KAMBI YAKE JIJINI MWANZA KUONDOKA KESHO KUELEKEA UGANDA, KASEJA BADO CHAGUO BORA.
Kocha
mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen (kulia) akizungumza na wandishi wa
habari (hawako pichani) ikiwa ni siku moja kabla ya kuondoka jijini
Mwanza mara baada ya kumaliza kambi, kushoto ni Afisa habari wa TFF
Michael Wambura.
|
NA ALBERT G. SENGO: MWANZA
Ni
takribani majuma mawili sasa Taifa Stars imekuwa jijini Mwanza ikiweka
Kambi kuelekea kipute cha marudiano na 'The Cranes', katika mchezo
unaotarajiwa kuchezwa jumamosi hii ya tarehe 27 mwezi wa 7mwaka 2013
mjini Kampala.
Sasa kambi
imefikia tamati, yamesalia masaa kadhaa ambapo kesho mchana majira ya
saa 7 na dakika 25, wawakilishi hao wa taifa la Tanzania, Taifa Stars
wataondoka kwa ndege ya Shirika la Precission Air kuelekea nchini Uganda
kuisaka tiketi ya CHAN.
Msikilize hapo chini
.
Msikilize hapo chini
.
KWA UFUPI:
Kocha mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen amezungumzia mapengo yaliyopo
kwenye kikosi chake kuanzia kutokuwepo kwa Kapombe kwenye idara ya
ulinzi na sasa Mwinyi Kazimoto katika idara ya kiungo, bila shaka kikosi
kitakuwa na utofauti ambao anaona ni sehemu ya marekebisho na
anamaboresho.
WASHINDI WA TIGO ‘MILIKI BIASHARA YAKO’ WAKABIDHIWA BAJAJI ZAO
Meneja
Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga (kulia) akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mshindi
wa pili wa promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’, Bw. Riziki
Lucas Kisemo (36) mfanyakazi wa viwandani, mkazi wa Makabe, Dar es Salaam. Tigo
tayari imelipia leseni ya barabani (Road license) na bima kwa ajili ya Bajaji
hizo. Anachotakiwa mteja sasa, ni kuanza biashara yake bila shida mara moja.
Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga
(kulia) akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mshindi wa kwanza wa promosheni ya
‘Miliki Biashara Yako’, Bw. Mohamed Ramadhani Mnjori (39) muuza nguo za
mitumba, mkazi wa Ilala – Dar es Salaam kwenye halfla ya makabidhiano
iliyofanyika eneo la Soko Kuu la Kariakoo, Dar es Salaam.
SHILOLE MATATANI WIZI SIMU ZA DIAMOND...!!!
Stori:Shakoor Jongo na Musa Mateja
STAA wa filamu na muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ..........
ameingia matatani akidaiwa kuingia mitini na simu tatu za mkononi alizoaminiwa nchini Afrika ya Kusini alikokwenda kufanya shoo.
Msanii huyo alikumbwa na kasheshe hilo Julai 19, 2013 nyumbani kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sinza Mori, Dar. Siku hiyo Diamond alikuwa akifuturisha na aliwaalika watu mbalimbali wakiwemo mastaa lakini nusura futuru iingie doa kufuatia zogo hilo.
Tuesday, July 23, 2013
MASELA WAUWANA KWA MARUNGU KISA DEMU WA KISUMKUMA...!!!
Mnamo tarehe 21/07/2012 majira ya saa 23:30hrs huko kijiji cha Nkwangu wilaya ya Chunya mkoa wa Mbeya, Seni s/o Sandu, miaka 20, Msukuma, mkulima na mkazi wa Nkwangu aliuawa kwa kupigwa fimbo kichwani na Tolo s/o Seko, miaka 20, Msukuma, mkulima na mkazi wa Nkwangu.
Chanzo ni ugomvi wa kumgombania msichana aitwaye Holo d/o Kulwa, miaka 16, Msukuma mkulima na mkazi wa Nkwangu.
Mtuhumiwa amekamatwa na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaandaliwa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi wa polisi diwani athumani anatoa wito kwa jamii kutojichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na kudhibiti hasira zao kwa kuyatatua matatizo ya kimapenzi kwa njia ya mazungumzo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.
Signed by, [Diwani Athumani – ACP] kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya.
Source: Watemi
KIKWETE AWATAKA UMOJA WA MATAIFA KURUHUSU SILAA KATIKA OPERATIONI ZAO
Rais
Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa marehemu askari waliouwawa huko
Darfur wakitekeleza majukumu ya umoja wa mataifa ya kulinda amani.
Dar es Salaam.
Rais
Jakaya Kikwete ameutaka Umoja wa Mataifa (UN), kuruhusu kutumika kwa
mtutu katika operesheni za kulinda amani zinazoendelea.
Alitoa
kauli hiyo jana baada ya kutoa heshima zake kwa wapiganaji saba wa
Tanzania waliokuwa Darfur, Sudan katika operesheni ya kulinda amani ya
UN na Afrika (Unamid) ambao waliuawa na kundi linalodaiwa la wanamgambo
wa Janjaweed wanaoungwa mkono na Serikali ya Sudan inayoongozwa na Rais
Omar al-Bashir.
Wapiganaji waliouawa ni Oswald Chaula kutoka 42KJ
Chabruma, Songea, Peter Werema (44KJ Mbeya), Fortunatus Msofe (36KJ
Msangani, Pwani), Rodney Ndunguru (92KJ Ngerengere), Mohamed Juma (94KJ
Mwenge), Mohamed Chukilizo (41KJ Nachingwea) na Shaibu Othman (MMJ-
Upanga).
“Lazima nikiri kuwa taarifa hiyo ya vifo vya vijana wetu
ilinihuzunisha, kunisikitisha na kunikasirisha. Kwa nini watu wa Darfur
wawaue wanajeshi wetu ambao wamekwenda kule kuwasaidia wapate utulivu
ili kunusuru maisha yao, kuwaondolea wasiwasi na kuwawezesha wafanye
shughuli zenye tija kuendesha maisha yao?
“Moja kwa moja sikusita
kuamini kuwa waliofanya hivyo ni watu wahalifu. Tangu uhuru ni sera ya
nchi yetu kutetea wanyonge dhidi ya ukoloni, ubaguzi, uonevu, dhuluma na
watu wote walioko katika mazingira hatarishi Afrika na duniani. UN
ifanyie marekebisho sheria ili majeshi yanayolinda amani yawe na nguvu
za kujihami ili kuzuia maafa yanayoweza kujitokeza.”
GODBLESS LEMA AFYATUA KOMBORA LINGINE....!!!
CHAMA cha demokrasia na Maendeleo (Chadema),
kimetangaza kuanza kutoa mafunzo ya kujihami kwa vijana wao maarufu kama Red
brigedi kuanzia Agosti mosi, mwaka
huu.
Akitangaza tarehe hiyo jana wakati wa mkutano wa chama
hicho uliofanyika Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini, kiongozi wa ulinzi wa chama
hicho kanda ya Nyanda za juu kusini Lucas Mwampiki, alisema kuwa ameamua kuweka
wazi adhima hiyo ili serikali isiendelee kusumbuka kuwa inao uwezo wa
kuwazuia.
‘’Polisi msisumbuke
kutafuta kuwa tutaanza lini, ni hivi, tutaanza tarehe 1, mwezi wa nane mwaka
huu’’ alisema Mwampiki ambaye pia ni diwani wa kata ya Mwakibete
Jijini Mbeya.
TAIFA STARS KUIFUATA UGANDA 'THE CRANES' JUMATANO, KUKIPIGA JUMAMOSI
Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inaondoka Mwanza keshokutwa (Julai
24 mwaka huu) kwenda Kampala, Uganda kwa ajili ya mechi ya marudiano ya
Kombe la CHAN itakayochezwa Jumamosi (Julai 27 mwaka huu) Uwanja wa
Mandela kuanzia saa 10 kamili jioni.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini
Mwanza chini ya Kocha Kim Poulsen tangu Julai 14 mwaka huu kujiandaa kwa
mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo mbili itacheza Fainali
za CHAN zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Timu
hiyo itaondoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza saa 7.25 mchana kwa ndege ya
PrecisionAir, na inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Entebbe saa 10.15 jioni.
Wakati
huo huo, Kocha Kim Poulsen kesho (Julai 23 mwaka huu) atakuwa na
mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya kikosi chake.
Mkutano huo utafanyika saa 5 kamili asubuhi kwenye hoteli ya La Kairo
jijini Mwanza.
HAWA NDIO ASKARI WALIOKUFA DARFUR WAKILINDA AMANI - MUNGU ZILAZE ROHO ZAO PEMA PEPONI AMINA
MT 97024 PTE Fortunatus Wilbard Msofe- 36 KJ
Subscribe to:
Posts (Atom)