Kocha
mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen (kulia) akizungumza na wandishi wa
habari (hawako pichani) ikiwa ni siku moja kabla ya kuondoka jijini
Mwanza mara baada ya kumaliza kambi, kushoto ni Afisa habari wa TFF
Michael Wambura.
|
NA ALBERT G. SENGO: MWANZA
Ni
takribani majuma mawili sasa Taifa Stars imekuwa jijini Mwanza ikiweka
Kambi kuelekea kipute cha marudiano na 'The Cranes', katika mchezo
unaotarajiwa kuchezwa jumamosi hii ya tarehe 27 mwezi wa 7mwaka 2013
mjini Kampala.
Sasa kambi
imefikia tamati, yamesalia masaa kadhaa ambapo kesho mchana majira ya
saa 7 na dakika 25, wawakilishi hao wa taifa la Tanzania, Taifa Stars
wataondoka kwa ndege ya Shirika la Precission Air kuelekea nchini Uganda
kuisaka tiketi ya CHAN.
Msikilize hapo chini
.
Msikilize hapo chini
.
KWA UFUPI:
Kocha mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen amezungumzia mapengo yaliyopo
kwenye kikosi chake kuanzia kutokuwepo kwa Kapombe kwenye idara ya
ulinzi na sasa Mwinyi Kazimoto katika idara ya kiungo, bila shaka kikosi
kitakuwa na utofauti ambao anaona ni sehemu ya marekebisho na
anamaboresho.
Lakini
pia hakufurahishwa na namna alivyoondoka Mwinyi Kazimoto akitegemea
Shirikisho la Soka nchini TFF litatumia busara zake kumwajibisha
mchezaji huyo kukosa uzalendo.
Amezungumzia
pia baadhi ya maoni ya wadau wa soka mfano suala la Juma Kaseja kutajwa
na baadhi yao kuwa amezeeka, kiwango kimeshuka hivyo hastahili kuchezea
Taifa stars. Amehoji-Hivi factor ya msingi unayotizama kwa mchezaji ni umri wake au kiwango chake uwanjani? Kwa idara ya goalkeeping kwa uri wa Kaseja miaka 29 ni umri mzuri sana kwa golikipa, lakini pamoja na hayo yote ana kiwango kikubwa mno.
Amejaribu pia kuizungumzia idara ya difensi' kwa tathimini ya baadhi ya mechi kubwa ambazo timu ya taifa imecheza siku zilizopita akisema kuwa kwa wale wanaofikiri kuna mapungufu makubwa kwenye safu ya ulinzi, mechi ngumu dhidi ya Zambia, dhidi ya Cameroon, akiuliza magoli mangapi yalifungwa goli la Stars kwenye mechi hizo?... jibu ni goli moja huku Stars ikiibuka na ushindi.
Hivyo haoni kama kuna tatizo kubwa kama linavyozungumzwa bali kilichokosekana kwa wachezaji wake hususani kwa mechi dhidi ya Uganda ni kukosa umakini.
Afisa habari wa TFF Michael Wambura na Kim Poulsen wakiwa mbele ya wandishi wa habari katika ukumbi wa Nyerere hotel Lakairo jijini Mwanza Tanzania |
No comments:
Post a Comment