Meneja
Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga (kulia) akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mshindi
wa pili wa promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’, Bw. Riziki
Lucas Kisemo (36) mfanyakazi wa viwandani, mkazi wa Makabe, Dar es Salaam. Tigo
tayari imelipia leseni ya barabani (Road license) na bima kwa ajili ya Bajaji
hizo. Anachotakiwa mteja sasa, ni kuanza biashara yake bila shida mara moja.
Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga
(kulia) akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mshindi wa kwanza wa promosheni ya
‘Miliki Biashara Yako’, Bw. Mohamed Ramadhani Mnjori (39) muuza nguo za
mitumba, mkazi wa Ilala – Dar es Salaam kwenye halfla ya makabidhiano
iliyofanyika eneo la Soko Kuu la Kariakoo, Dar es Salaam.
Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga
(kushoto) akimpa mkono wa pongezi mshindi wa kwanza wa promosheni ya ‘Miliki
Biashara Yako’ ibuka na Bajaji Bw. Mohamed Ramadhani Mnjori (39) alipopanda
kukagua Bajaji yake. Bajaji hiyo ina thamani ya Tsh 6,700,000.
Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga
akimtambulisha mshindi wa tatu wa promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’ Bw. Adam Saidi
Kalulu (36) mkulima, mkazi wa Kiluvya kabla ya kumkambidhi Bajaji yake mpya
mbele ya wanahabari na wananchi waliojitokeza eneo la Soko Kuu la Kariakoo
kushudia makabidhiano hayo.
Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga
(mwenye kofia ya Tigo) katika picha ya pamoja na washindi watatu wa kwanza ya
promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’ ibuka na Bajaji wakati wa sherehe ya
makabidhiano iliyofanyika leo eneo la Soko Kuu, Kariakoo. Mteja wa Tigo anao uwezo wa kujishindia Bajaji moja kila
siku kwa muda wa siku 60 kwa kuongeza vocha ya Tsh 1,000 tu kwa siku.
Mshindi wa pili wa promosheni ya ‘Miliki
Biashara Yako’, Bw. Riziki
Lucas Kisemo (36) mfanyakazi wa viwandani, mkazi wa Makabe, Dar es Salaam
akitoa ushuhuda mbele ya vyombo vya habari jinsi hapo zamani alipokuwa
akihangaika na kazi ‘ngumu ngumu’ ambazo zilikuwa hazimpi kipato cha kutosha cha
kuendeshea maisha yake. Mshindi huyo ametoa shukurani nyingi sana kwa Tigo na
ametoa rai kwa watanzania wengine waweze kushiriki. “Hakika Tigo imebadilisha
maisha yangu,” Riziki alisema. Pembeni yake ni Meneja
Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga,
Bajaji 3 kati ya Bajaji 60 zilizoshindwa
na washindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’ zikipaki
eneo la Soko Kuu, Kariakoo kabla ya kukabidhiwa kwa washindi mapema leo.
Zimebakia Bajaji 57 zakushindaniwa, droo inayofuata itachezwa siku ya Jumatatu
29 Julai, 2013 kwa ajili ya kuwapata washindi 7 wa wiki hii. Wateja wanaweza kuendelea kushiriki kwa kuongeza salio mara
nyingi wawezavyo ili kujiongezea nafasi zaidi ya kujishindia Bajaji na kumiliki
biashara zao wenyewe.
No comments:
Post a Comment