Monday, June 24, 2013
MH. SUGU AMUOMBA RADHI WAZIRI MKUU
Mhe Sugu |
Waziri Mkuu, Mhe. Pinda |
BAADA
ya kauli yake iliyoibua mjadala mkubwa nchini dhidi ya Waziri Mkuu,
Mhe. Mizengo Pinda kufuatia majibu yake aliyoyatoa wiki iliyopita
Bungeni kwa kutaka Polisi kuendelea kuwapiga raia, Mbunge wa Mbeya
Mjini, Mhe Joseph Mbilinyi 'Sugu', aomba radhi.
Sugu
amemuomba radhi mhe Pinda na watanzania kwa ujumla kwa lugha aliyotumia
katika kuonyesha hisia zake juu ya kauli aliyoitoa mhe Pinda bungeni.
Kupitia
akaunti yake ya Facebook, Mbunge huyo machachari amenukuliwa akiwaomba
radhi Watanzania waliokerwa na kauli yake iliyodai kwamba Tanzania
haijawahi kuwapata Waziri Mkuu kama Mhe. Pinda kwa kusema;
"Ndugu
watanzania, naombeni radhi kwa tusi nililolitoa kwa mhe Pinda, kwani
nilikua nimeghafirika, halikuwa kusudio langu kumtukana mmoja wa
viongozi wa nchi."
ANGALIA PICHA ZA MAZISHI YA MAMA MZAZI WA BARNABA (BI MARIAMUARUBETH)
Mama Diamond |
Siku ya leo jumapili ndio ilikuwa siku husika kabisa katika kutoa heshima za mwisho kwa Bi Mariamu
Arubeth aliezaliwa 4/12/1967 na kufariki tarehe 22/6/2013.
Zifuatazo ni picha za Mazishi Ya Mama mzazi wa Barnaba kuanzia nyumbani hadi makaburini....
Sunday, June 23, 2013
The Finest : FA apata wakati mgumu kwa kulazimishwa na mashabiki kutaja jina la Lady Jay Dee.
by IRENE MWAMFUPE
Mwanamuziki
Hamis Mwinjuma, maarufu Mwana FA, amepata wakati mgumu kwa
kulazimishwa na mashabiki kutaja jina la Lady Jay Dee, baada ya
kuliruka jina hilo alipokuwa akiimba wimbo wa Mabinti ambao ndani yake
kuna jina la Jay Dee.
Mwana FA alisita kwa muda na baadaye aliamua kurudia wimbo huo na alipofika katika kipengele cha kumtaja Jide aliimba kwa kumtaja, hali iliyoufanya ukumbi huo ulipuke kwa shangwe na mashabiki kumtaka arudie tena na tena.
Kutokana na hilo FA aliamua kufunguka; “Tunaishi na watu hivyo lazima mtagongana, hata mapacha wanakosana na kusameheana, lakini wakati mwingine shida inawafanya mnapatana,” alisema Mwana FA.
Awali
shoo ilitangazwa kuwa ingekuwa ya watu 400 tu. Lakini mpaka inafika
saa nne kasoro usiku, muda uliotangazwa kuanzwa kwa shoo hiyo watu
waliokuwa wamefika walikuwa kama 250 tu.
Saa
nne kamili mwanamuziki Hamis Mwinjuma, Mwana FA alikanyaga ‘red
carpet’ akiwa na mbunifu wa mavazi Sheria Ngowi, na baada ya
kuchukuliwa picha kadhaa alianza kuelekea nje ya ukumbi sehemu
waliyosimama watu wakipata chakula na vinywaji, watu walizidi kufurika
lakini kila aliyeingia alikuwa alwatan kidogo.
Waliendelea kuwasili mastaa na shoo inaanza Mashabiki wanaanza kuingia ukumbini saa tano kamili baada ya kupata vyakula na vinywaji nje, huku muziki wa taratibu ukipigwa na bendi ya muziki wa dansi ya Njenje. Mashabiki wanaendelea kubadilishana mawazo mpaka inapotimu saa tano na robo usiku, ambapo Mwana FA anapanda jukwaani.
Anaanza kazi kwa shoo ya aina yake baada ya kuimba hip hop live akiwa na bendi ya muziki wa dansi, kwenye shoo hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
FA
alipanda jukwaani na wimbo wa Binamu akisindikizwa na wanamuziki
Mandojo na Domokaya waliovalia suruali nyeusi na mashati meupe huku
wakiwa wamevalia mikanda aina ya ‘suspender’, baadaye aliimba wimbo
Unanijua Unaniskia na Bado Niponipo Kwanza ambao uliwapendeza
mashabiki.
Alisimamisha shoo kwa muda na msanii Bernald Paul maarufu kama Benpol alipanda jukwaani na kuimba nyimbo zake tatu kwa kuziunganisha ukiwamo wa Maneno, Pete na Nikikupata na baadaye aliimba na Mwana FA wimbo wa Asubuhi aliomshirikisha Q Chief.
FA alipanda jukwaani na wanamuziki kadhaa katika vipindi tofauti akiwamo Linah Sanga ‘Linah’, Maua, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’.
Baadhi
ya nyimbo alizoimba ni pamoja na Kama Zamani, Alikufa kwa Ngoma,
Habari Ndio Hiyo, Leo, Mabinti, Unanitega, Yalaiti na nyingine nyingi.
HII NDIO HALI YA MSANII BARNABAS TANGU KUPOKEA TAARIFA ZA MSIBA WA MAMA YAKE
Kiukweli inasikitisha sana tangu asubuhi hajatia kitu chochote tumboni analia ananyamaza,akipewa chakula hakitaki.mungu mjalie ndugu yetu mpe nguvu aweze kumzika mama yake kwa aman na upendo.
R.i.P mamaa BARNABAS, Maziko ni leo saa 10 katika makaburi ya mburahati,kuanzia asubuhi saa 5 tutakuwa na misa maalum kwa ajili ya marehemu mama barnabas.
ASKOFU AITAKA SERIKALI KUWABANA WASIOTAKA NCHI ITAWALIKE.
RAIS
Jakaya Kiwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa
serikali na dini wakati alipohudhuria sherehe za miaka 25 ya Askofu wa
jimbo kuu la Morogoro Telesphol Mkude wa pili kulia kwa rais katika
viwanja vya shule ya ST Peter mkoani Morogoro jana.
SIKU
chache baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutaka Serikali iachwe ifanye
kazi yake katika kudhibiti vurugu zinazoibuka kila kukicha, Askofu wa
Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude naye
ameitaka Serikali kuwadhibiti wote wasiotaka nchi itawalike.Askofu huyo amesema kuonya pekee hakusaidii, bali inawajibu wa kuwachukulia hatua kali ili kukomesha vitendo vinavyotishia amani nchini.Askofu
Mkude aliyasema hayo jana wakati wa maadhimisho ya Jubilei ya miaka 25
ya uaskofu wake kwenye viwanja vya Seminari ya Mtakatifu Petro mjini
hapa ambapo Rais Jakaya Kikwete alikuwa miongoni mwa wageni mashuhuri
waliohudhuria.
RIHANNA AMPIGA SHABIKI WAKE NA KIPAZA SAUTA BAADA YA SHABAKI HUYO KUMKERA...!!!
MWIMBAJI nyota wa muziki wa R&B, Robyn Rihanna Fenty, anayefahamika zaidi kwa jina la Rihanna, amenaswa na kamera akimpiga shabiki ‘mic’ usoni alipokuwa akifanya shoo huko Birmingham, Uingereza Jumatatu iliyopita.
Rihanna alifanya tukio hilo la kushtua alipojichanganya kwenye umati wa mashabiki, huku akiimba kwenye shoo hiyo ambayo ni sehemu ya ziara yake ya dunia inayojulikana kama ‘Diamond World Tour’ akiitangaza albamu yake ya saba ya ‘Unapologetic’ iliyotoka mwaka jana.
Ilidaiwa kuwa Rihanna mwenye umri wa miaka 25 alishindwa kudhibiti hasira zake baada ya shabiki huyo asiyefahamika kumng’ang’ania mkono wake.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliandika kwenye ukurusa wake wa Twitter: "Rihanna amempiga mtu mmoja na mic yake katika ajali haha oops."
Na Rihanna alijibu akisema kuwa alikusudia kumpiga shabiki huyo kwa sababu alikuwa akimzuia.
TAMASHA LA KILI MUSIC AWARDS NDANI YA UWANJA WA JAMHURI DODOMA.....OMMY DIMPOZ APIGWA CHUPA NA MASHABIKI JUKWAANI..!!
Ommy
dimpoz arushiwa chupa na mawe jukwaaani dodoma na kushindwa kufanya
show ya kilimanjaro muzik award dodoma. Wadau wa dom wasema kamwe msanii
yoyote atakaye mdisi msanii wa dodoma awatamkubari kufanya show dom na
watamshusha jukwaani kama walivyo fanya leo
Msanii
wa Muziki wa Kizazi Kipya,Linex akiwasalimia mashabiki na wapenzi wa
Muziki waliofurika kwa wingi ndani ya Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma
leo,ambapo usiku huu kulikuwa na bonge moja la Show ya Kilimanjaro
Tanzania Music Tour 2013.
Msanii Ben Pol akighani moja ya nyimbo zake.
POLISI 7 WAFUNGWA JELA MIAKA 5 KWA KOSA LA MAUAJI HUKO KIGOMA
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora imewahukumu kifungo cha miaka mitano jela askari saba wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma ambao walikuwa wakishtakiwa kwa mauaji.
Akitoa
hukumu yake katika kikao cha Mahakama Kuu kilichokuwa kikifanyika
mkoani Kigoma Jaji wa mahakama hiyo, Sam Mpaya Rumanyika alisema kuwa
baada ya kupitia ushahidi mbalimbali Mahakama hiyo imewatia hatiani
askari hao kwa kosa la kuua bila kukusudia.
Katika
kesi hiyo namba 35 ya mwaka 2012 washitakiwa hao walifikishwa
mahakamani hapo na kusomewa shitaka la kumuua Festo Stephano, mkulima wa
kijiji cha Rungwe Mpya Wilaya ya Kasulu mkoani hapa katika tukio
lililotokea Agosti 6, mwaka 2011.
Askari
hao waliohukumiwa ni pamoja na Baraka Hongdi, Koplo Mawazo, Koplo
Swahib, D/C Charles, D/C Shamsi, D/C Jerry na D/C Amrani ambao kwa
pamoja walikana shitaka lao katika kesi hiyo namba 35 ya mwaka 2012.
Akitoa
utetezi kabla ya hukumu hiyo wakili wa washitakiwa, Method Kabuguzi
aliiomba Mahakama kuwafutia shitaka washitakiwa hao na kuwaachia huru
kwani wote bado vijana na wameoa hivi karibuni.
Sambamba
na hilo Kabuguzi alisema kuwa askari hao walikumbwa na mkasa huo wakati
wakitekeleza jukumu lao la ulinzi wa taifa ambapo walimkamata mtuhumiwa
wa kutumia silaha na ndipo kifo kikatokea wakati wakitekeleza majukumu
yao.
Source: http://www.wavuti.com
AMANDA APIMA NGOMA, PRESHA YAPANDA YASHUKA
Stori:Gladness Mallya
MSANII
wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ hivi karibuni alijikuta
akipandwa na kushukwa na presha mara baada ya kwenda hospitali kupimwa
Ugonjwa wa Ukimwi.Kikizungumza na Exclusive chanzo makini ambacho
kilishuhudia tukio zima katika Hospitali ya Dokta Mvungi, Kinondoni,
jijini Dar kilisema baada ya Amanda kupewa majibu ya vipimo na daktari,
alianza kuhaha huku na kule kama mtu aliyechanganyikiwa, kisha presha
ikampanda baadaye ikashuka.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Amanda na kumuuliza juu ya tukio hilo ambapo bila hiyana alitiririka:
“Ile
ilikuwa ni mara ya tatu kupima ngoma yaani wakati nikisubiri majibu,
presha ilipanda ghafla mpaka daktari akawa na wakati mgumu wa kunipa
majibu.
“Nilienda
kuchukua majibu na sikutaka kuyaangalia, nilimpelekea daktari ambaye
aliniambia niko safi yaani sikuamini nilitoka nikiwa naongea peke yangu,
nilikuwa sijiamini si unajua tena ujana ni maji ya moto sasa presha ,”
alisema Amanda.
Saturday, June 22, 2013
HATIMAE NDUGU YETU MPENDWA CHARLES HILILA AZIKWA LEO KIJIJINI KWAO
NYUMBA YA MILELE ALIMOLALA MWANDISHI WA HABARI KITUO CHA MATANGAZO CHA CHANELL TEN
Habari Na Steven KanyephMwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa chaneli ten Charles hilila umezikwa leo katika makaburi ya nyumbani kwao katika kijiji cha Dumida kata ya Tinde mkoani Shinyanga nakuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji akiwemo mkuu wa mkoa wa shinyanga na viongozi wengine wa kiserikali , vyama vya siasa pamoja na viongozi wa kidini.
Mazishi hayo yametanguliwa na ibada ya misa takatifu iliofanyika katika kanisa la mama mwenye huruma Ngokolo mjini Shinyangsa na baade kufuatiwa na ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwao na kuongozwa na padre Emmanueli Makolo akisaidiana na padri Josephati Mahalu kabla ya maziko.
katika mahubiri padre Mahalu amewaasa wanajamii kudumisha upendo na kuwakumbusha kuwa kifo kipo mahali popote hivyo wanajamii wanapaswa kumrudia Mungu na kutenda matendo mazuri yenye kuleta amani na yanayompendeza Mungu.
Hali kadhalika mkuu wa mkoa wa Shinyanga Alli Nassoro Lufunga ametoa salamu za rambirambi kutoka katika serikali ya mkoa na kuwaomba wanahabari kudumisha upendo zaidi hasa katika umojawao kwani utawasaidia kufanya kazi kwa weledi na kuleta tija zaidi kwa wanajamii.
Marehemu Charles hilila amefariki juni 19 katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa TB ya mifupa uliokuwa unamsumbua .
Aidha marehemu ameacha mjane na watoto watatu ,
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema mbinguni amina
*********************************************************************************
MEYA AZIMIA BAADA YA KUPIGWA NA POLISI
Meya wa Mji Mkuu wa Kampala nchini Uganda akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kukamatwa kwa tuhumza za kusababisha vurugu.
Kampala, Uganda. Watu wawili wameuawa kwa risasi nchini Uganda juzi, wakiwa katika mkusanyiko kwenye eneo la soko la Kisekka.
Meya wa mji mkuu wa Uganda, Kampala, Erias Lukwago, pia alizirai baada ya kupigwa na polisi hao waliofyatua risasi za mipira kuutawanya umati wa wafuasi wake.
Akiwa kitandani, Meya huyo amesema baada ya kupata kipigo hicho alipoteza fahamu na kukimbizwa hospitalini.
“Bomu ambalo lilinifanya nipoteze fahamu lilirushwa katika gari langu na kuingia ndani,” amesema.
Meya huyo ni mpinzani wa rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni, alieleza kwamba maofisa wa polisi walimpiga kifuani na kuzirarua nguo zake wakimtuhumu kwa kuchochea ghasia.
NKAMIA AZUA VURUGU TENA BUNGENI SAFARI HII ATAKA KUMPIGA MBUNGE MWENZAKE...!!!
Tukio hilo
lilitokea mwanzoni mwa wiki ambapo imeelezwa kuwa Nkamia mbali na kutaka
kumpiga mbunge huyo, pia alimtolea matusi mazito ya nguoni (gazeti hili
haliwezi kuandika).
Kwa mara ya
kwanza mbunge huyo aliingia katika kashfa baada ya kutoa kauli bungeni
kuwa hazungumzi na mbwa, bali anazungumza na mwenye mbwa kabla ya
kuingia katika mzozo na wahariri na baraza la habari aliposema kuwa
Jukwaa la Wahariri na Baraza la Habari ni NGOs za kutafuta fedha.
Uchunguzi wa
Mwananchi ambao umethibitishwa na Nkamia mwenyewe umebaini kuwa chanzo
cha tukio hilo ni kutokana na kuzomewa kwa Nkamia katika kampeni za
uchaguzi mdogo Kata ya Dalai Wilaya ya Chemba.
Kwa mujibu wa
wabunge mashuhuda ambao waliliona tukio hilo, ilielezwa kuwa Nkamia,
ambaye pia ni mwandishi wa habari, alianza kumshushia matusi Moza wakiwa
ndani ya Bunge hadi walipotoka nje alimfuata na kutaka kumpiga.
Subscribe to:
Posts (Atom)