Friday, June 07, 2013
Thursday, June 06, 2013
AJALI MBAYA YATOKEA IFISI MBALIZI LEO MCHANA, YAJERUHI ZAIDI YA ABIRIA 15.
Daladala
ambayo ilikuwa inatoka Mbalizi kwenda Songwe yenye namba za usajili T
635 ALS ikiwa imeharibika vibaya Baada ya Ajali kutokea Eneo la Ifisi
Mbalizi Mbeya
Hapa
ndipo eneo ambalo Daladala iliingia wakati ilijaribu kulipita Gari
lengine akiwa mwendo kasi na kuukutana na Tela la Mafuta
Daladala upande wa nyuma
Lori aina ya Scania yenye namba ZA usajili T378 AGD likiwa limepaki Baada ya ajali hiyo kutokea
Mabaki ya daladala
ANGALIA PICHA ZA MAZISHI YA MSANII MAREHEMU ALBERT MANGWEA
Hapa ndipo Mwili wa Marehemu Albert Mangwea ulipopumzishwa leo Mkoani Morogoro
Baada
ya siku kadhaa zilizokuwa na kila aina ya harakati, ugumu na majonzi
makubwa, Albert Mangweha aka Ngwair hatimaye leo amezikwa kwenye
makaburi ya Kihonda mkoani Morogoro ambako ni nyumbani kwao.
Kabla
ya kuzikwa, wananchi wa Morogoro walipata fursa ya kuuaga mwili wake
kwenye uwanja wa Jamhuri. Umati mkubwa wa wananchi ulijitokeza kutoa
heshima zao za mwisho kwa mwili wa Ngwair aliyefariki nchini Afrika
Kusini, wiki iliyopita. Wasanii wengi kutoka Dar es Salaam nao
wamehudhuria mazishi hayo.
Hapa ndipo Mwili wa Marehemu Albert Mangwea ulipopumzishwa leo Mkoani Morogoro
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU MABADILIKO KWA BAADHI YA MAKAMANDA
(Msemaji wa jeshi la polisi nchini Advera Senso-SSP)
………………………………………………………………………………
Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734 Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556 S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja: DAR ES SALAAM.
Simu : (022) 2110734 Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556 S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja: DAR ES SALAAM.
06 JUNI, 2013
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Inspekta
Jenerali wa Polisi, IGP Said Mwema, amefanya mabadiliko ya makamanda na
wakuu wa upelelezi katika baadhi ya mikoa hapa nchini.
Katika
mabadiliko hayo aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Naibu
Kamishna wa Polisi (DCP) Michael Kamhanda amehamishiwa Makao Makuu ya
Polisi na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Ramadhani Mungi ambae alikuwa Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya
Jinai.
Aidha,
DCP Ally Mlege aliyekuwa Makao Makuu ya Polisi amehamishiwa Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam kwenda kuwa Mkuu wa utawala na raslimali watu.
Vilevile,
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela
amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi wa makosa ya jinai na nafasi yake
inachukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa
Arusha ACP Camilius Wambura. Aidha, ACP Duwan Nyanda aliyekuwa Makao
Makuu ya Upelelezi anaenda kuwa Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai
Mkoa wa Arusha.
Uhamisho huo ni wakawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi (T).
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi (T).
BABA YAKE DIAMOND YUPO HOI ANAUMWA...... DIAMOND HAJAWAHI KANYAGA KUMJULIA HALI...!!
Kwa mujibu wa chanzo makini, Baba Diamond anasumbuliwa na tatizo la miguu kuvimba hali ambayo imemfanya ashindwe kutembea lakini cha kushangaza mwanaye, Diamond hajaenda kumjulia hali.
“Baba Diamond ni mgonjwa kwa muda mrefu sana lakini Diamond hajawahi kuja kumuona hata siku moja,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, waandishi wetu walifunga safari mpaka nyumbani kwa mzee huyo, Magomeni-Kagera, jijini Dar ambapo alikiri kuugua kwa muda mrefu na kukosa msaada kutoka kwa Diamond.
“Nasumbuliwa na miguu kwa muda mrefu sana na ninatibiwa katika Hospitali ya Saint Monica, Manzese-Darajani. Diamond ana taarifa za kuumwa kwangu lakini hajawahi kuja kuniona.
“Namshukuru mwanangu Queen Doreen kwa kunijali kwa kila kitu,” alisema baba Diamond.
HII NDIO HALI YA KHADIJA KOPA MARA BAADA YA KUPOKEA TAARIFA ZA MSIBA WA MUMEWE KIPENZI HII LEO...!!
Mkuu wa mkoa Rukwa Eng. Stalla Manyanya akimfariji msanii na taarab na malkia wa mipasho Tanzania,Khadija omar Kopa alipokua kwenye chumba maalum cha kupumzikia wageni kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia leoa alfajiri kutokana na ugonjwa, Bi Khadija Kopa alikua akitokea kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani kitaifa yaliyoaadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana.
Baadhi
ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa na Mpanda wakimsindikiza
kuapanda ndege msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania Khadija
Omar kopa kwenye uwanja wa ndege wa mpanda baada ya kupewa taarifa ya
kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia leo alfajiri
kutokana na ugonjwa, Bi Khadija Kopa alikua akitokea kwenye Maadhimnisho
ya siku ya Mazingira Duniani kitaifa yaliyoadhimishwa Namanyere Mkoani
Rukwa jana.
Mkuu
wa mkoa Rukwa Eng. Stalla Manyanya kushoto akimfariji msanii na taarab
na malkia wa mipasho Tanzania Khadija omar Kopa alipokua kwenye chumba
maalum cha kupumzikia wageni kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya
kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia
leoa alfajiri kutokana na ugonjwa, Bi Khadija Kopa alikua akitokea
kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani kitaifa
yaliyoaadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana. (Picha na ofisi ya Makamu
wa Rais)
UMATI WA WAKAZI WA MOROGORO WALIOJITOKEZA KUUAGA MWILI WA NGWEA.... UWANJA WA JAMHURI WAFURIKA..!!
Wananchi waliojitoka uwanjani
Huyu nimmoja kati ya walipoteza fahamu uwanjani
zoezi la uuagaji wa mwili ukiendelea
Rafiki
wa wa karibu wa marehemu Albert Mangwea aliyekuwa amelazwa nchini
Afrika Kusini amerejea Tanzania na yuko njiani akielekea mkoani Morogoro
kwaajili ya kushiriki mazishi ya swahiba wake Mangwea jioni ya leo
PICHA MBALIMBALI KWENYE SEND OFF YA FROLA MVUNGI ILIYOFANYIKA JANA
Msanii H.Baba akiwa na bestman wake wakiwa kwenye sendoff ya mke wake mtarajiwa
ANGALIA PICHA ZA M2 THE P AKIMUAGA RAFIKI YAKE ALBERT MANGWEA MJINI MOROGORO
M2 THE P
amefanikiwa kutoa salamu zake za mwisho kwa rafiki yake kipenzi
ambaye alikuwa naye huko Afrika kusini tena walikuwa ndani ya
chumba kimoja kabla ya mauti kumkuta Ngwea..Mwanzoni, M 2 THE P
alikuwa amefichwa na kudanganywa kuwa Ngwea alikuwa ametangulia
Tanzania. Baadaye Maggie alilazimika kumweleza ukweli
AFISA WA BANDARI ANASWA AKIOMBA RUSHWA YA NGONO KWA MWANAFUNZI ILI AMPE AJIRA BANDARINI
Mtuhumiwa akihojiwa na polisi
MWANAMUME
aitwaye Andrew Kabula (34), mkazi wa Kimara Mwisho jijini, hivi
karibuni alinaswa gesti akiwa na mwanafunzi ‘denti’ aliyetaka kufanya
naye ngono ili ampatie kazi bandarini..
Kabula
a.k.a Afisa Feki alijitapa kwa denti huyo kwamba ni Afisa wa Mamlaka ya
Bandari jijini Dar na ana uwezo wa kumpatia kazi kama atampa rushwa ya
ngono.
Kwa
kutambua kwamba kitendo hicho ni kosa kisheria, denti huyo (jina lake
kapuni) aliwasiliana na Oparesheni Fichua Maovu ili kumnasa afisa huyo
feki.
Waandishi
wetu waliwasiliana na polisi wa Kituo cha Mbezi Luis jijini Dar na
kumwekea mtego jamaa huyo katika gesti aliyoichagua, iliyopo maeneo ya
Kimara jijini Dar.
Afisa huyo kila mara alikuwa akiwasiliana na denti huku akimsisitiza kutoondoka hapo kama kweli alitaka ajira.
Waandishi, askari na denti walitangulia katika gesti hiyo na afisa akataarifiwa na denti kwamba ameshafika eneo la tukio.
Yakafuata maelekezo ya kuchukua chumba kutoka kwa afisa huyo aliyedai kwamba yupo mbali kidogo.
Saa
moja usiku, afisa feki alifika katika eneo la tukio na kuingia chumbani
katika gesti hiyo (jina tunalo), huku askari na waandishi wakifuatilia
nyendo zake.
Bila
ya kushtuka kama amewekewa mtego, moja kwa moja afisa aliingia chumbani
na kumkuta denti huyo ambaye alizidi kumsisitizia lengo lake.
Baada ya kuhakikishiwa kile anachokitaka na denti huyo, afisa alisaula viwalo vyake vyote na kuwa tayari kwa tendo.
MUME WA KHADIJA KOPA AFARIKI DUNIA
Khadija Omar Kopa akiwa na mumewe Jaffari Ally enzi za uhai wake.
Mume wa Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki, Khadija Omar Kopa, aitwaye Jaffari Ally amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Marehemu
alikuwa anasumbuliwa na matatizo katika mfumo wa upumuaji na mpaka
mauti yanamfika alikuwa amelazwa katika hospitali ya wilaya Bagamoyo.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN.
MTANZANIA KUONGOZA JESHI LA KULINDA AMANI DARFUR.
Kwa mara nyingine Bendera ya Tanzania imeendelea kupepea katika Tasnia ya Ulinzi wa Amani ya Kimataifa.
Mapema
wiki hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon na Mwenyekiti
wa Umoja wa Afrika Bi. Nkosizana Dlamin Zuma wametangaza uteuzi wa
Luteni General Paul Ignace Mella Kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (
JWTZ) kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa
huko Darfur ( UNAMID)
Taarifa
iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon,
na nakala yake kutumwa katika Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, imeeleza kwamba, Lt. Gen.
Mella anachukua nafasi iliyoachwa na Mkuu wa zamani wa Jeshi hilo
(UNAMID), Lt. Gen Patrick Nyamvumba kutoka Rwanda ambaye amemaliza muda
wake wa utumishi March 31,2013.
Wasifu
wa Luteni General Paul Ignace Mella unaelezwa kuwa ni Mwanajeshi wa
muda mrefu na mwenye uzoefu na utumishi uliotukuka katika JWTZ akiwa
amewahi kushika nyadhifa mbali mbali muhimu za uongozi.
Baadhi
ya nyadhifa hizo ni pamoja na Naibu Kamanda Kikosi cha Tanzania chini
ya Umoja wa Mataifa huko Liberia ( 1993-95), Kamanda wa Kikosi
cha JWTZ, Afisa Mnadhimu-Makao Makuu ya Jeshi, Mwambata Jeshi-Ubalozi
wa Tanzania Uganda na hadi sasa alikuwa ni Mkuu wa Usalama na Utambuzi-
JWTZ.
Uteuzi
wa Lt. Generali Mella unafuatia mchakato mrefu ulioshindanisha
wateuliwa kutoka nchi mbalimbali duniani, na hatimaye yeyé akaibuka
mshindi.
OFISI YA UBALOZI WA TZ UN
Wednesday, June 05, 2013
MPYA KUHUSU BINTI WA KITANZANIA ALIYEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA NA KUHUKUMIWA KUNYONGWA IJUMAA HII
Hii
ndio picha ambayo imesambaa kwenye mitandao mingi ya msichana
anesemekana ni Fatma aka Brown Berry wa Ilala Dar es Salaam ambae
amehukumiwa kunyongwa huko egypt baada ya kukamatwa na unga.
MR NICE APIGWA CHINI NA LABEL ALIYOKUA AKIFANYA NAYO KAZI KENYA, KISA NI MVIVU.
GrandPa
Records Ya Kenya Imevunja Mkataba Wake Wa kazi na Msanii Mr Nice kutoka
Tanzania Baada ya miezi michache ya kufanya nae kazi. Fahamu Mr Nice
alipewa mkataba na GrandPa Records huku akijua kuwa ana mkataba mwingine
Tanzania na Producer Lamar. GrandPa Wamesema Mr Nice Ni Msanii Mvivu na
Asiye toa ushirikiano kwenye kazi kabisa ndio maana wameamua Kuvunja
mkataba wake. Hii Ni Post ya FaceBook Ya GrandPa Records. Bado Taarifa
Zina Kuja Kaa Na Mimi Utaiskia Interview Yao Hapa Soon
Subscribe to:
Posts (Atom)