Thursday, June 06, 2013

AFISA WA BANDARI ANASWA AKIOMBA RUSHWA YA NGONO KWA MWANAFUNZI ILI AMPE AJIRA BANDARINI

Mtuhumiwa  akihojiwa na polisi

MWANAMUME aitwaye Andrew Kabula (34), mkazi wa Kimara Mwisho jijini, hivi karibuni alinaswa gesti akiwa na mwanafunzi ‘denti’ aliyetaka kufanya naye ngono ili ampatie kazi bandarini..
Kabula a.k.a Afisa Feki alijitapa kwa denti huyo kwamba ni Afisa wa Mamlaka ya Bandari jijini Dar na ana uwezo wa kumpatia kazi kama atampa rushwa ya ngono.

Kwa kutambua kwamba kitendo hicho ni kosa kisheria, denti huyo (jina lake kapuni) aliwasiliana na Oparesheni Fichua Maovu  ili kumnasa afisa huyo feki.
Waandishi wetu waliwasiliana na polisi wa Kituo cha Mbezi Luis jijini Dar na kumwekea mtego jamaa huyo katika gesti aliyoichagua, iliyopo maeneo ya Kimara jijini Dar.
Afisa huyo kila mara alikuwa akiwasiliana na denti huku akimsisitiza kutoondoka hapo kama kweli alitaka ajira.


Waandishi, askari na denti walitangulia katika gesti hiyo na afisa akataarifiwa na denti kwamba ameshafika eneo la tukio. 

Yakafuata maelekezo ya kuchukua chumba kutoka kwa afisa huyo aliyedai kwamba yupo mbali kidogo.
Saa moja usiku, afisa feki alifika katika eneo la tukio na kuingia chumbani katika gesti hiyo (jina tunalo), huku askari na waandishi  wakifuatilia nyendo zake.

Bila ya kushtuka kama amewekewa mtego, moja kwa moja afisa aliingia chumbani na kumkuta denti huyo ambaye alizidi kumsisitizia lengo lake.

Baada ya kuhakikishiwa kile anachokitaka na denti huyo, afisa alisaula viwalo vyake vyote na kuwa tayari kwa tendo.

Denti aliendelea kujibaraguza na kutuma taarifa kwa askari na waandishi  wetu kwamba jamaa alikuwa tayari kwa tendo ndipo timu nzima ikavamia chumbani.

Mara baada ya askari kumkamata na kumuweka chini ya ulinzi, afisa huyo alipekuliwa katika simu yake ya kiganjani na kukutwa na meseji kadhaa zikionesha kwamba alikuwa akifanya mawasiliano na wasichana wengi kwa ajili ya kuwapa kazi bandarini.

Katika kudhihirisha kuwa ni tapeli mzoefu, siku hiyohiyo  afisa huyo alikuwa na ahadi na msichana mwingine ambaye katika simu jina lake ‘liliseviwa’ kwa jina la Mariam ili apewe rushwa ya ngono.
Inadaiwa kwamba, tapeli huyo amekuwa akiwadhalilisha wasichana wengi kwa staili yake hiyo ya kuwadanganya kuwapatia kazi na kisha kuwaacha bila ya ajira. 


Baada kutiwa nguvuni na kupelekwa Kituo cha Polisi, ilibainika kwamba jamaa si mfanyakazi wa Mamlaka ya Bandari bali ni deiwaka wa udereva wa daladala zinazofanya safari zake kati ya Ubungo na Msata mkoani Pwani.

Katika kuonesha jamaa ni mtata, alipofikishwa kituoni na baada ya kuandikisha maelezo alisema kwamba alikuwa akihitaji selo ya peke yake kwani hataki kuchanganyika na watu.

Credit: GPL

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...