Thursday, June 06, 2013

ANGALIA PICHA ZA MAZISHI YA MSANII MAREHEMU ALBERT MANGWEA

bb21b674cea911e2918122000a9f4d8a_7

Hapa ndipo Mwili wa Marehemu Albert Mangwea ulipopumzishwa leo Mkoani Morogoro
Baada ya siku kadhaa zilizokuwa na kila aina ya harakati, ugumu na majonzi makubwa, Albert Mangweha aka Ngwair hatimaye leo amezikwa kwenye makaburi ya Kihonda mkoani Morogoro ambako ni nyumbani kwao.
Kabla ya kuzikwa, wananchi wa Morogoro walipata fursa ya kuuaga mwili wake kwenye uwanja wa Jamhuri. Umati mkubwa wa wananchi ulijitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Ngwair aliyefariki nchini Afrika Kusini, wiki iliyopita. Wasanii wengi kutoka Dar es Salaam nao wamehudhuria mazishi hayo.

16f11344cea711e2813a22000a1f8f34_7


75e8603ecea511e29ecd22000aaa08de_7

4406673ccea511e2850422000a1f9a85_7
“Marehemu Albert Mangweha azikwa kishujaa sana ni umati usioelezeka mungu akulaze mahali pema peponi,” ameandika Izzo B kwenye Instagram.
Naye Lady Jaydee kupitia Twitter ameandika: Mpaka hapa tulipomsindikiza panatosha. Mungu amrehemu, kazi tumeimaliza. Life goes on.”
e1147594cea211e2a86422000a1f9839_7
ee9d94facea411e2a9ea22000ae81462_7
f18745b2cea411e2aa3022000a9e2931_7
Picha kutoka kwenye akaunti za Instagram za Millard Ayo, Mboni Masimba na Mwasiti. (140)

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...