Lissu, ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni, aliyasema jijini Dar es Salaam jana wakati akihojiwa na kituo cha televisheni cha ITV.
Alisema fujo hazitaisha kama watu hawatafuata kanuni na Spika kusimamia na kuzingatia mamlaka yake bila ya upendeleo wowote.
“Tatizo
kubwa Spika anafanya kazi bila kufuata kanuni za Bunge. Kuna mambo
mengine anayatolea maamuzi bila kufuata kanuni za Bunge. Mfano suala
letu la adhabu tuliyopewa wabunge watano wa Chadema ya kutohudhuria
vikao vitano. Hakuna katika kanuni za Bunge.
Spika
alipaswa kupeleka majina yetu katika Kamati ya Maadili ili ichunguze na
kupendekeza adhabu kisha ipeleke taarifa bungeni na Bunge ndilo litoe
adhabu," alisema.