Sunday, April 21, 2013

MUME WA MTU ATIWA MBARONI KWA KOSA LA KUFANYA MAPENZI NA MBUZI MWENYE MIMBA NA KUHARIBU MIMBA YA MBUZI HUYO

Marcel ambaye ni mume wa mtu, alifunguliwa kesi namba 29/2013 katika Mahakama ya Mwanzo ya Bashneti mkoani Babati kwa kosa la kuiingilia kimwili mifugo, kinyume na kifungu cha 325 kanuni ya adhabu, sura ya 16 na kesi hiyo ilisomwa hivi karibuni.
Mshitakiwa aliwekewa dhamana lakini siku chache baadaye kesi ilipotakiwa kuendelea, hakuonekana na imebainika mahakamani hapo kuwa ametoroka.

Kesi hiyo ipo mbele ya Hakimu Julius Dagharo wa mahakama hiyo na aliyethibitisha mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa ametoroka ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Bashneti, Omari Mwanditi.
Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita, mmiliki wa mbuzi anayedaiwa kuingiliwa,  Clementina Masay alidai kuwa mtuhumiwa huyo amemsababishia hasara kwani mbuzi wake alikuwa na mimba lakini baada ya kitendo hicho, imeharibika.
Jamii ya wafugaji wa Kiiraq wa eneo hilo wamesikitishwa na kitendo cha mtuhumiwa kudaiwa kuiingilia mifugo yao kimwili mara kwa mara na wameahidi kumsaka hadi wamkamate.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Babati, ACP Akili Mpwapwa amekiri kutokea kwa tukio hilo na ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa wakimuona mtuhumiwa huyo ili afikishwe mahakamani.

AMA kweli dunia imekwisha kwani mtu mmoja, Daniel Marcel (27), mkazi wa Kijiji cha Madunga, wilayani Babati, Manyara, amekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa madai ya kufanya mapenzi.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...