'Hekalu' linalomilikiwa na Mchungaji Getrude Lwakatare. |
Wabunge
wamemtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira Terezya
Huvisa kuzivunja nyumba mbili zilizopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam
zilizojengwa katika fukwe ya bahari ya Hindi ikiwemo ya mbunge licha ya
kwamba kuna zuio la mahakama.
Bila kutaja majina ya wamiliki hao, wabunge hao walitaka hatua hizo zichukuliwe kwa haraka kwa nyumba hizo zilizojengwa kwenye fukwe kinyume cha sheria zivunjwe kwa maelezo kuwa hazina ofa wala hati.
Sambamba
na hilo wametaka watendaji wa serikali waliohusika kutoa vibali
kuruhusu ujenzi huo kwa maelezo kuwa walichukua rushwa wachukuliwe
hatua.
Mbunge
wa kwanza kuanza kuzungumzia hilo ni wa viti maalum, Esther Bulaya
(CCM) aliyetaja viwanja viwili vyenye namba 2019 na 2020 kikiwemo cha
mbunge ambaye ni kiongozi wa kiimani waliojenga nyumba zivunjwe licha
ya kuwepo zuio la mahakama.
“Mwaka
jana waziri wa Ardhi, Profesa Anna Tibaijuka alivunja nyumba za kawaida
licha ya zuio la mahakama, lakini nyumba zilizo kwenye viwanja namba
2019 na 2020 hazikuvunjwa kwa sababu ya zuio la mahakama hii ni double
standard hatuwezi kuvumilia.
“Wengine
wenye nyumba ni viongozi tupo nao humu tena wa kiimani, lakini kwa nini
viongozi tunafaya hivi wakati tunatakiwa tuwe wa mfano na tunawafanya
viongozi wenzetu washindwe kufanya kazi zao?…hakuna haja ya kuogopa
waziri Huvisa (Mazingira) vunja nyumba, haiwezekani kuwa na nguvu ya
fedha.
“Wabunge
wenzangu tuazimie Manispaa ya Kinondoni na NEMC (Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira), wakavunje nyumba hizo ndani ya wiki
moja , naomba kutoa hoja,” alisema.
Hata hivyo, Spika Anne Makinda alimweleza; “Haiwezekani kutoa hoja kwa kuingilia vyombo vingine”.
Mbunge
ambaye ni kiongozi wa kiimani mwenye nyumba katika eneo hilo la Mbezi
Beach aliyejenga katika fukwe ya bahari kwa kuondoa mikoko na kuweka
kifusi na kujenga nyumba ni Mbunge wa Viti Maalumu, Mchungaji Dk.
Getrude Lwakatare (CCM).
Naye
Mbunge wa viti maalumu, Grace Kiwelu (Chadema) akichangia bajeti ya
Ofisi ya Makamu wa Rais, alisema kamati yake ya Ardhi na Mazingira
ilitembelea eneo hilo la Mbezi Beach na kukuta aliyejenga katika kiwanja
2019 hakuwa na ofa wala hati.
“Ametumia
pesa kuwarubuni watendaji akaondoa mikoko, akaweka kifusi na akajenga
nyumba naomba wizara ya Ardhi na ya mazingira wawachukulie hatua
watendaiji hao,” alisema.
Akijibu
hoja ya Bulaya, kuwa kwanini nyumba ya Mchungaji Lwakatare haikuvunjwa
wakati nyingine zilivunjwa, mwanasheria mkuu wa Serikali, Frederick
Werema alisema:
“Sisi
ni wajibu wetu twende mahakamani kusema watu hao wamevunja sheria
kujenga hapo. Wao wanaruhusiwa na Katiba na mahakama itafuata sheria.
“Nashauri Bulaya usitoe shilingi kuzuia Bajeti ya Waziri, uje tuone huyo kigogo itakuwaje.”
Hata hivyo, Huvisa alisema: “Nyumba tulizovunja hazikuwa na kesi na hii tuliyoiacha ilikuwa na kesi.”
Jumba
la kifahari linalodaiwa kuwa la Mchungaji Lwakatare ambalo
lilizinduliwa mwaka jana, limekuwa klikitajwa kuwa lina thamani ya
takribani sh bilioni 1.5.
No comments:
Post a Comment