Sunday, April 21, 2013

SHY- ROSE BHANJI APATA AIBU YA KARNE TOKA KWA ANNA KIBIRA

Aliyekuwa mjumbe baadae katibu mkuu wa CHANETA Anna Kibira amechaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa chama cha mpira wa pete chaneta Katika uchaguzi uliofanyika jioni ya leo hii Mkoani Dodoma , huku msimazi wa uchaguzi huo akiwa mkuu wa wilaya ya bahi na aliyekuwa Mtangazaji wa zamani wa itv Betty Mkwasa .
Anna Kibira amemshinda mpinzani wake Shy-Rose Bhanji kwa tofauti ya la kura arobaini katika nafasi ya uenyekiti Anna Kibira amepata kura 61 dhidi ya mpinzani wake Shy-Rose Bhanji ambaye amepata kura arobaini na moja .
Aidha kulikuwa na nafasi mbalimbali ambazo zilikuwa zikigombewa katika chama hicho cha mpira wa pete ambapo kulikuwa na wajumbe wa kamati ya utendaji ambao walikuwa wagombea tisa lakini wamepataikana wagombea sita tu.

Grace Khatib ambaye alikuwa hana mpinzani katika nafasi ya mweka hazina alipata kura za ndio 66 na kura za hapana 16 kati ya kura 82 zilizopigwa.
Katika nafasi ya makamu mwenyekiti kulikuwa na wagombea wawili Zainab Mbiro na Agnes Madasila katika nafasi hiyo Zainabu Mbiro alipata kura hamsini saba wakati mpinzani wake amepata kura 27
Kwa maana hii CHANETA imepata safu mpya kabisa ya uongozi baada ya ile ya mwanzo ile kuamua kuachia ngazi na wagombea wengine kuamua kutokugombea kabisa uongozi katika chama hicho cha mchezo wa pete kwani safu mpya inatakiwa kufanya kazi ya ziada kufikia malengo ya kuinua mchezo wa mpira wa pete kwani uongozi uliopita uliiwezesha CHANETA kuifikisha timu ya taifa ya mchezo huo katika mashindano ya dunia.
Chama kiliweza kuaandaa michuano ya mataifa ya afrika ni wazi kabisa wanachangamoto kubwa ya kufanya japokuwa mara baada ya ushindi kibira amesema kuwa anataka kuupeleka mchezo huo mikoani na kwenda kuuimarisha zaidi vijijini .

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...