Mtindo wa maisha, ulaji na msongo wa mawazo, vimewasababishia Watanzani wengi maradhi lukuki hata vifo.Hata hivyo, wataalamu wa afya kutoka Afrika Kusini wamekuja na dawa maalumu, zilizo na uwezo wa kurudisha kumbukumbu, kuongeza upeo darasani, kuondoa sumu mwilini na kumfanya mzee kuonekana kijana.
Dawa
hizo zinazotumia vitamini zilizomo kwenye vyakula vya kila siku, zina
uwezo wa kuongeza kiwango cha uelewa kwa mwanafunzi au mfanyakazi.
Kiwango hicho cha uelewa kitaalamu unatambulika kama ‘IQ’.
Mratibu wa dawa hizo hapa nchini, John Haule anasema kuwa dawa hizo zina uwezo wa kufanya kazi kwa haraka.
“Virutubisho hivi ni vizuri kwa wale wanaokwenda katika
mitihani au wanataka kufanya kazi inayohitaji umakini wa hali ya juu,” anasema Haule na kuongeza: “Zimetengenezwa kwa vyakula tunavyotumia na siyo kemikali.”
mitihani au wanataka kufanya kazi inayohitaji umakini wa hali ya juu,” anasema Haule na kuongeza: “Zimetengenezwa kwa vyakula tunavyotumia na siyo kemikali.”
Haule
ambaye ni mtaalamu wa tiba asili na mimea anasema kwamba mtindo wa
maisha na vyakula vinavyoliwa na watu mara kwa mara kwa sasa huufanya
mwili kuhifadhi sumu nyingi mwilini.
Anasema
kuwa dawa hizo pia zina uwezo kuondoa sumu mwilini na kuufanya mwili wa
binadamu kurejesha rangi yake halisi na kumeng’enya vizuri chakula
anachokula.
Haule
anayefanya kazi pamoja na Shirika la Nativa linalotengeneza dawa hizo
la nchini Afrika Kusini, anaeleza kuwa tangu kuingiza dawa hizo nchini
watu wengi wamejitokeza kuzihitaji.
Ofisa
Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza
anasema kuwa mamlaka hiyo inazitambua dawa hizo kama virutubisho vya
chakula, zimesajiliwa na ni salama kwa binadamu.
“Tuna taarifa kuwa bidhaa za ‘Go Woman’ na ‘Go Man’ zimesajiliwa na ni salama,” anasema.
Dawa
nyingine zinazotengenezwa na kampuni hiyo zimetajwa kuwa na uwezo wa
kuunda mifupa kwa watu wazima na majeraha ya wagonjwa wa kisukari.
SOURCE::MWANANCHI::
“Ni
vigumu kwa watu wazima wenye miaka 50 na kuendelea kupona haraka
wanapopata ajali, lakini hizi dawa zinaponya majeraha na kuunga haraka
mfupa,” anasema Haule.
Anasema
kuwa kadri umri wa binadamu unavyoongezeka mwili wake unashindwa
kuzalisha baadhi ya virutubisho vinavyoupa mwili uimara.
Dawa hizo zina mchanganyiko wa madini, vitamin, viondoa sumu pamoja na dawa za mitishamba.
Virutubisho vya chakula kwa kawaida hupungua ubora wake kwa sababu ya udongo, mionzi au kuweka vyakula hivyo katika majokofu.
Mambo mengine yanayofanya virutubisho vya chakula visifanye kazi yake sawasawa ni msongo wa mawazo na uchafu wa mazingira.
Ugonjwa wa kukosa raha na kusononeka kila wakati au sonona, pia unaweza kutibiwa kwa dawa hizo.
“Sonona
inaua. Hata wataalamu wa afya wa nchi za Ulaya wamethibitisha, lakini
dawa hii ina madini ya amino acidi ambayo hupatikana baada ya mtu
kucheka,” anasema.
Anabainisha kwamba dawa hizo zina vitamin maalumu zinazoweza kuongeza kinga ya mwili na kuondoa sumu mwilini.
“Zina vitamin a, c na e, madini ya zinki na selenium na zina uwezo wa kuongeza nguvu ya mwili,” anasema.
Anadokeza kuwa kati ya dawa hizo, zipo pia dawa kwa ajili ya wanawake na wanaume pekee, zilizo na kazi maalumu.
Kwa
mfano dawa ya wanawake ina uwezo wa kumsaidia mwanamke apate raha ya
tendo la ndoa, inarutubisha nywele zake na kuzifanya zikue kwa haraka.
Vilevile, dawa hiyo inasaidia kuimarisha ngozi ya mwili kwa kuondoa sumu mwilini.
“Hii dawa kwa ajili ya wanawake ina Vitamini maalumu za kukuza nywele kama ‘Omega3 na Omega 6,’” anasema Haule.
Kwa upande wa wanaume, dawa hiyo itawasaidia kuongeza uwezo wa tendo la ndoa, kuimarisha mifupa pamoja na viungo.
Dawa zote mbili, yaani ile ya wanawake na ya wanaume zina uwezo wa kuimarisha ubongo na kumbukumbu.
Haule
anaongeza kuwa ipo dawa kwa ajili ya wanawake wenye tatizo la kutokwa
damu kwa wingi kunakosababishwa na hedhi au maradhi mengine.
Hata
hivyo, Dk John Semkuya kutoka Hospitali ya Mwananyamala anasema kuwa ni
vigumu mtu kupata tiba ya akili akiwa tayari ni mtu mzima, kwani uwezo
wa kiakili unajengwa kuanzia utotoni.
“Lakini suala hili linahitaji utafiti zaidi kwa sababu kama hujafanya tafiti, huna haki ya kuzungumza,” anasema Dk Semkuya.
Anasema ikiwa virutubisho hivyo vya chakula vitatumiwa tangu utotoni basi vinakuwa na manufaa zaidi kuliko kutumiwa ukubwani.
Wagonjwa wa Ukimwi
Miongoni mwa dawa hizo ipo dawa ya ‘Life Gain’ mahususi kwa kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi.
Haule
anasema kuwa kwa virutubisho vilivyo katika dawa hizo vina uwezo wa
kupandisha kinga ya mwili kwa haraka, bila kumwathiri mgonjwa.
Mwananchi
ilifanya mazungumzo na mwanamume mmoja mkazi wa Tandika (jina
linahifadhiwa) anayeishi na VVU ambaye alitumia dawa ya Lifegain.
Mtu
huyo alisema alikuwa hoi kwa maradhi, lakini baada ya kutumia dawa hiyo
kwa muda wa wiki mbili, alinyanyuka na sasa anaendelea na shughuli zake
za kawaida.
SOURCE::MWANANCHI::
No comments:
Post a Comment