Na Maelezo Zanzibar
Makamo
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Dkt Ali Muhammed Shein
amesema kuwa ataendelea kukiimarisha na kukienzi Chama Cha Mapinduzi
pamoja na kuulinda Muungano wa Serikali mbili uliopo.
Kauli hiyo ameitoa leo huko katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani wakati akizindua ziara yake ya Mikoa mitano ya Zanzibar.
Dkt
Shein ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amesema
kuwa kuna kila sababu ya kukiimarisha chama hicho kutokana na umuhimu
wake na kwamba Muungano uliopo wa Serikali mbili ndio njia bora ya
kuendeleza mashirikiano ya kidugu yaliyodumu kwa muda mrefu.
Amesema
kuwa lengo kuu la ziara hiyo ni kupata taarifa za matukio mbali mbali
pamoja na changamoto zilizopo katika mikoa hiyo zinazohusu CCM.
Aidha
amewataka viongozi wa CCM kuwa na mashirikano mazuri katika
kukiimarisha Chama na kuhakikisha kwamba kinapata ushindi katika kila
uchaguzi unaokuja.
Dkt.
shein amesema kuwa ana imani na Chama chake kuibuka mshindi katika
chaguzi kutokana Chama hicho kuchagua uongozi makini ambao utahimili
vishindo vya uchaguzi ujao.
Katika
hatua nyingine Dkt Shein aliwataka Wananchi kuendelea kujishughulisha
na harakati zao za kujiletea maendeleo na kuepuka kuvunja sheria za
nchi.
“Serikali
inataka amani na utulivu kwa Wananchi wake sambamba na kuimarisha
maendeleo kama Malengo ya Mapinduzi yalivyoelekeza na kwa njia hiyo
hatuna budi kuyaenzi Mapinduzi” alieleza Makamo Mwenyekiti wa CCM.
Katika
ziara hiyo Makamo Mwenyekiti amezindua Tawi jipya la CCM la Vikokotoni,
Kikwajuni SACCOS BANK pamoja na kutoa kadi 270 kwa wanachama wapya wa
Chama cha Mapinduzi.
No comments:
Post a Comment