WANAFUNZI
wa shule ya sekondari ya Mizengo Pinda kata ya Kibaoni Wilayani Mlele
mkoani Katavi, wamemshambulia kwa mawe na matofali mkuu wa shule hiyo
na mwalimu wa taaluma na kuharibu jengo la utawala na nyumba za walimu
hao baada ya kuwatuhumu walimu hao kuwa ni washirikina.
Kaimu
kamanda wa polisi wa mkoa wa katavi, Joseph Myovela, alisema tukio hilo
limetokea juzi saa 2:30 usiku shuleni hapo baada ya kuzuka kwa tafrani
iliyodumu kwa zaidi ya saa 1:30.
Habari
kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa chanzo cha tukio hilo kilitokana na
mwanafunzi mmoja aitwaye Jofley Pinda kushikwa na ugonjwa wa mapepo
uliomfanya aanguke chini ambapo tukio hilo lilitokea mchana wa saa saba.
Myovela
alisema ilipotimia muda huo wa saa mbili wanafunzi hao walijikusanya
na kuandamana hadi kwenye jengo la utawala na kuanza kulishambulia kwa
mawe na matofali na kuvunja mlango na dirisha la jengo hilo.
Alieleza
baada ya kufanya uharibifu kwenye jengo la utawala walielekea kwenye
ofisi ya mwalimu wa taaluma ambapo waliharibu mtandao wa mawasiliano
kwenye Computer.
Wanafunzi
hao ambao muda wote walikuwa na hasira walielekea nyumbani kwa mkuu wa
shule, huku wakiwa na matofali na mawe walipofika na kumkosa mkuu
washule aliyekuwa amekwenda kwenye matembezi ya jioni walianza
kushambulia nyumba yake kwa mawe na tofali na kuharibu mlango na
madirisha.
Kaimu
kamanda Myovela alisema kundi hilo lilielekea nyumbani kwa mwalimu wao
wa taaluma Bonifasi Nsalamba ambapo walimkuta akiwa anajiandaa kuingia
ndani ya nyumba yake akitokea matembezini.
Ndipo walipoanza kumshambulia kwa mawe katika sehemu mbalimbali za mwili wake huku wakimzomea kuwa mchawi huyo mshirikina ..
Alisema
katika shambulio hilo wanafunzi walimjeruhi mwalimu Bonifasi na
kumsababishia majeraha katika mwili wake na aliweza kutibiwa katika
zahanati ya kibaoni na kuruhusiwa na hali yake inaendelea vizuri.
Jeshi
la polisi mkoa wa katavi limetoa wito kwa wanafunzi wa shule hiyo na
shule nyingine za mkoa huo waachane na kuamini imani za ushirikina na
polisi inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kuwabaini waliohusika
na
waweze kuchukuliwa hatua.
No comments:
Post a Comment