MBUNGE wa Nkasi,Ally Kessy (CCM) ametoa mpya bungeni baada ya kuuliza
swali la kuitaka serikali ihalalishe kilimo cha bangi ili kujipatia
fedha za kigeni.
Akiuliza swali la nyongeza jana, Kessy
alisema kwa kuwa zao la tumbaku limekuwa likipigwa marufuku dunia
nzima, lakini limendelea kulimwa na kuchangia pato la mataifa
mbalimbali ikiwemo Tanzania, kwanini serikali isihalalishe kilimo cha
bangi kama ilivyo kwa tumbaku ili kuchangia pato la taifa?
Swali hilo liliibua vicheko kwa wabunge
wote, akiwemo Spika na Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula, Adam Malima.
Hata hivyo, Waziri Malima akijibu swali hilo alisema kuwa
pingamizi dhidi ya zao la tumbaku duniani limepungua na zao hilo sasa
ni moja ya mazao makubwa ya biashara.
Kuhusu bangi kuhalalishwa kuwa zao la biashara, Waziri
Malima alisema kuwa katika nchi zingine imeruhusiwa kuwa moja ya zao la
biashara na linachangia pato la taifa.
“Hapa nchini bado
bangi haijaruhusiwa kuwa zao la biashara, lakini kama utafiti
utafanyika na kubaini kama linaweza kupata soko la kuingizia pato
taifa, tutaliangalia hilo,” alisema.
No comments:
Post a Comment