Mwenyekiti wa chadema, mtaa wa Isamilo kaskazini B wilayani Nyamagana Philbert Bulinjiye amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kujipatia shs milioni 1,250,000 kwa njia ya udanganyifu.
Hukumu hiyo, imetolewa na hakimu Vaineth
Mahizi wa mahakama hiyo, kufuatia kesi ya jinai namba 196/2012, iliyofunguliwa
na Vedasto Mavubhi ambaye alimtuhumu mwenyekiti huyo kuchukua kwake
kiasi hicho cha fedha, kwa ajili ya kumuuzia kiwanja.
Hakimu
Mahizi katika hukumu yake, alidai ameridhika na ushahidi uliotolewa na
upnade wa mlalamikaji, mashahidi pamoja na wazee wa baraza hivyo
kumhukumu mwenyekiti kwenda jela.
Alisema
mwenyekiti huyo pamoja na Balozi Robert Byagaye wanastahili kutumikia
kifungo hicho cha mwaka mmoja jela kutokana na kutiwa hatiani.
"kitendo
kilichofanywa na viongozi hawa, kuwaibia raia wanaowaongoza kiutapeli
kwa kuwadanganya kuwauzia kiwanja na kisha kutafuta mtu bandia kwa madai
kuwa kiwanja hicho kiko katika mtaa wanaouongoza, ni udanganyifu" Alisema
hakimu na kuongeza kuwa Mwenyekiti huyo amehukumiwa kifungo hicho ili
iwe fundisho kwa viongozi wengine matapeli.
No comments:
Post a Comment