Friday, April 12, 2013
JAY -Z KUNUNUA KISIWA KWA AJILI YA FAMILIA YAKE
Vyanzo vya habari vilivyopo karibu na nyota huyo vilieleza juzi kuwa ametenga pauni milioni mbili ili kununua eneo hilo lililopo kaskazini mwa wilaya ya Abaco kwa ajili ya familia yake.
Thursday, April 11, 2013
JOHARI AGOMA KUTINGISHA MAUNO YAKE MBELE YA RAY
MKONGWE
kwenye ‘Industry’ ya Filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ alitoa
kali ya aina yake baada ya kukataa kuzungusha nyonga mbele ya mwigizaji
mwenzake, Vincent Kigos ‘Ray’ anayedaiwa ni mpenzi wake
Tukio
hilo lililonaswa na mwandishi wetu juzikati, lilitokea katika Viwanja
vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar wakati wasanii hao walipojumuika
pamoja kwa ajili ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kitokee kifo cha
msanii mwenzao, Steven Kanumba.
Akiwa
viwanjani hapo, Johari aliitwa kupanda jukwaani na wasanii wenzake kwa
ajili ya kucheza sebene kidogo lakini yeye alikataa na mwandishi wetu
alimsikia akijitetea kuwa hawezi kukata nyonga mbele ya wasanii wenzake
hususan Ray ambaye ni bosi mwenzake kwenye kampuni yao ya RJ Company.
“Siwezi
kujidhalilisha mbele ya umati huo kwa kukata kiuno tena na bosi
mwenzangu yupo pale, labda ningekuwa nimelewa kiasi cha kutojitambua
hapo ningefanya madudu kama hayo,” alisema Johari.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, MULUGO ATANGAZA VITA NA WAZUSHI WAKE
NAIBU
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo amesema
atawafikisha mahakamani watu wanaodai kuwa ameghushi vyeti vya elimu ya
sekondari. Mulugo alisema amechoshwa na kashfa hizo zinazosambazwa na
baadhi ya watu atawafikisha mahakamani endapo wataendelea
kumdhalilisha.
Mulugo
alitoa kauli hiyo alipofungua mkutano wa mwaka wa Umoja wa Wamiliki wa
Shule za Sekondari na Vyuo Binafsi Tanzania (TAMONGSCO0) jijini Mbeya.
“Wanasema
eti nimeghushi vyeti, mara ooh sijui natumia jina la mtu. Nimechoshwa
na maneno haya… ni kweli nimerudia darasa kama walivyorudia watu
wengine, kwa nini iwe tatizo kwangu. Hata hapa tulipo wapo wengi tu
waliorudia darasa.
“Kama
kweli ningekuwa nimeghushi vyeti hivi leo ningekuwa naibu waziri wa
elimu? Sasa nimechoshwa, nitawachukulia hatua watu hawa, siwezi kusema
ni lini nitafanya hivyo ila nitakapoamua nitaanza,”alisema.
Kwa
miezi kadhaa sasa Mulugo amekuwa akidaiwa kughushi vyeti na kutumia
jina la mtu ili kufikia kiwango cha elimu alichonacho madai ambayo
alisema yanamchafulia jina katika jamii.
Kuhusu
suala la matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka jana, Mulugo alisema
matokeo hayo mabaya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na mmomonyoko wa
maadili miongoni mwa wanafunzi.
Naye
Ruth Mnkeni kutoka Dar es Salaam anaripoti kuwa Mlugo amezindua tovuti
ya elimu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ijulikanayo kama Shule
Direct.
Muluigo
alisema kuzinduliwa kwa tovuti hiyo kutawafanya wanafunzi kupata
maarifa mengi ya vitabu mbalimbali na kuinua kiwango cha elimu nchini
HALI TETE KWENYE SHIRIKA LA UTANGAZAJI TBC
Ndani ya Taasisi ya Utangazaji Tanzania(TBC) kwa sasa kuna mgogoro mkubwa sana unafukuta chini kwa chini ukihusisha pande mbili kuu, yaani Wafanyakazi wa kawaida na Uongozi wa juu wa shirika hilo, kuhusu madai yafuatao na huku wakitaka Mkurugenzi mkuu wa sasa wa TBC afukuzwe na bodi ya shirika hilo ivunjwe;source: JF
1/Ubaguzi katika kupewa vyeo, Posho na marupurupu(Suala la Itikadi, Ukanda na Udini linatajwa sana)
2/Kuruhusu wanasiasa(Viongozi wa serikali na makada wa CCM) kuingilia wanavyotaka kazi za kitaaluma katika utoaji wa habari hususani kuhariri(Kuchuja) habari.
3/Kutokulipwa malimbikizo ya madeni ya madai ya siku za nyuma.
4/Utendaji Duni na Mbovu wa Mkurugenzi mkuu Clement Mshana hadi kufikia kumpa jina la dhihaka la 'BOYA'
5/Vitisho vya kufukuzwa kazi kwa baadhi ya watumishi wanaohoji sana mwenendo mbovu wa shirika hilo kwa sasa.
6/Mvutano wa Chini kwa chini kati ya Wakurugenzi waliowekwa na Lowassa wakati akiwa waziri mkuu na wapya walioletwa na Pinda.
*Pia kuna issue ya mkataba tata(White Elephant) kati ya TBC na Startimes(Wachina!) ambao Terms, Conditions, Investment, Dividend na Shares havijawekwa wazi na sawasawa, japokuwa Mkurugenzi mkuu na Bodi yake ya sasa wanadai wameurithi tu lakini sio 'wapishi' kamili wa hicho kilichopikwa!!
KAULI YA ZITTO KUTOKA BUNGENI ASUBUHI HII
CAG
ameweka mezani taarifa yake asubuhi hii. Katika mkutano wa Kumi wa
Bunge, Serikali ilifanya mabadiliko ya Sheria ya Ukaguzi ya mwaka 2008
Kwa kubadilisha vifungu 38, 39 na 40 ambapo Serikali ingeleta majibu
yake sambamba na Taarifa ya CAG. Serikali haikuleta majibu hayo.
Wamevunja Sheria wakiisha nikiwa siku ya kwanza ya kuanza kutekelezwa
kwake. Spika alipowataka Serikali kutoa majibu, Mawaziri walibaki
kutazamana tu
HATARI : WALA MAHINDI HATARINI KUDUMAA AKILI
WATAALAMU
wa masuala ya afya na kilimo kutoka mataifa mbalimbali duniani,
wamebaini mahindi, karanga na mihogo yenye sumukuvu ni moja ya vitu
vinavyochangia saratani ya ini, udumavu wa mwili na akili kwa watoto.
Ingawa takwimu sahihi hazijapatikana kuonesha madhara ya kila
Kutokana
na ukubwa wa tatizo, wataalamu hao kutoka nchi 20, wanakutana jijini
Dar es Salaam kwa siku tatu, kuanzia jana, kutafuta njia madhubuti za
kukabiliana na sumukuvu. Tanzania inatajwa kuwa miongoni mwa nchi
zilizochukua hatua za awali dhidi ya tatizo hilo.
Akizungumza jana katika ufunguzi wa mkutano huo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi alisema,
“Lengo
la mkutano huu ni kuwapa fursa wataalamu kuja na mikakati
itakayoisaidia serikali na sekta binafsi kupambana na sumu ya aflatoxin
kwa kuwa hata hapa Tanzania ni tatizo kubwa.”
Dk
Mwinyi alifafanua kuwa, tatizo kubwa linaonekana kwenye mazao
yanayoathiriwa zaidi na sumukuvu ambayo ni mahindi, mihogo na karanga na
husababisha watumiaji kupata saratani ya ini na watoto hudumaa akili na
mwili.
Alisema
pamoja na serikali kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuwa na
sheria ya kudhibiti vyakula vinavyoingia nchini, lakini sheria pekee
haziwezi kumaliza tatizo hasa ikizingatiwa kuwa Watanzania wengi
wanatumia nafaka hizo wakati zikiendelea kukua shambani bila kuzipima
kiwango cha sumukuvu kinachotakiwa.
Sumukuvu
ni aina ya sumu inayosababishwa na kuvu katika mazao na ingawa
haiepukiki katika nafaka, kuna kiwango kinachopaswa kuwepo na
kinapozidi, huleta madhara hayo.
JK Atia Saini Kitabu cha Maombolezo ya Bi. Margaret Thatcher
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
Jana, Jumatano, Aprili 10, 2013 ametia saini Kitabu cha Maombolezo cha
aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Bi. Margaret Thatcher ambaye
alifariki dunia Jumatatu wiki hii kwa ugonjwa wa kiharusi akiwa na umri
wa miaka 87.
Rais Kikwete ametia saini Kitabu hicho kwenye Ubalozi wa Uingereza katika Tanzania ulioko Jengo la Umoja mjini Dar es Salaam.
Rais
alikaribishwa kwenye Ubalozi huo na Balozi wa Uingereza katika
Tanzania, Mheshimiwa Bi. Dianna Melrose na wafanyakazi wengine wa
ubalozi huo na amekwenda moja kwa moja kutia saini kitabu hicho mara
baada ya kuwasili kwenye Ubalozi huo.
Wednesday, April 10, 2013
Irene Uwoya afunguka kuhusu skendo yake na Diamond.......!!!
Baada ya majaribio mengi ya kupiga simu yake ambayo ilikuwa haipatikani muda wote wa mchana baadaye kwenye mida ya saa kumi na mbili hivi jioni tuliweza kumpata hewani na Jibu lake lilikuwa moja tuu kuwa “achana nazo” na sisi tukaona kweli tuachane nazo ila tukufukishie wewe msomaji wetu mpendwa “response” hiyo ili mwenyewe uamue na kutafakari. Hilo ndo jibu alilotupa mwanadada mrembo wa bongo movies Irene Uwoya kuhusu tuhuma za yeye kutoka kimapenzi na msanii Diamond.
Source:Bongo Movies
SHILOLE ANASA KWENYE PENZI LA MZUNGU...!!
Kwa mujibu wa shushushu wetu, tukio hilo lilijiri hivi karibuni katika hoteli moja maarufu jijini hapa ambapo Shilole alikuwa kwenye ziara ya shoo yake.
Ilidaiwa kuwa mara tu baada ya kumaliza ziara ya shoo, Shilole hakuondoka jijini hapa na badala yake alionekana sehemu tofauti akijivinjari na jamaa huyo ambaye uchunguzi wetu ulibaini kuwa ni bosi wa klabu moja maarufu ya usiku Kanda ya Ziwa.
Kabla ya kuondoka katika jiji hili la sangara na sato, Alhamisi iliyopita na ndege ya jioni, Shilole alinaswa kimalavidavi na Mtasha huyo Jumatano katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere wa Gold Crest kulipokuwa na maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Syria.
Shilole alishuhudiwa akifanyiwa ‘shopping’ ya kufuru na bwana huyo ambapo gazeti hili lilinasa mpango mzima ambapo lilipotaka kujua kama ni wapenzi, Mtasha huyo alijibu kwa kifupi sana: “No comment” (sina la kusema).
Kwa upande wake Shilole alipobanwa mbavu alifunguka: “Nisingependa kuongelea jambo hilo kwani sasa najipanga kimuziki zaidi, shopping ni mambo ya kawaida sana kwa hiyo ni vyema tukaongelea muziki wangu kwani shoo yangu ya Pasaka ilijaa mashabiki wa kufa mtu so nakubalika sana Mwanza na siku moja nitaweka makazi hapa.”
SHAA AAHIDI KUVUA NGUO ZOTE HADHARANI ENDAPO VIDEO YAKE ITAFIKISHA VIEWS 100,000
Kwa
waliokuwa na hamu ya kumuona huyu naye akiwa nusu uchi na
kivazi cha kuogelea tuu, huu sasa ni wakati wao.....
Coca
Cola pop Star maarufu kwa jina la Shaa amedai kuwa yupo
tayari kuvua nguo zake hadharani na kuyaanika maungo yake nyeti
na kubakiza kichupi cha kuogelea tu endapo video yake mpya
ya Lava Lava itafikisha views 100,000 katika mtandao wa youtube
Popout
“Lava
Lava Video imefikisha views 44,000+ leo.Endapo itafikisha 100,000
basi ntavua nguo zote na kuogelea coco beach mchana kweupe lets do,”Alitweet Shaa katika mtandao wa kijamii wa Twitta na kuongeza
“Niliitupia kiutani tu nikidhani in one day kupata views elfu50 ni ngumu…sasa naona watu wameniamkia! Kwa spidi hii…mmmh…noma,”
Subscribe to:
Posts (Atom)