Monday, April 02, 2018

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA 13 KWA NCHI ZINAZOVUTIA UWEKEZAJI


Shirika la Utafiti la Quantum Global limetoa ripoti ya nchi ambazo zinaongoza kwa kuvutia uwekezaji barani Afrika ambapo nchi ya Morocco imeshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Misri na Algeria.

Nafasi ya nne imeshikwa na Botswana, Ivory Coast nafasi ya tano, Afrika Kusini nafasi ya sita, Ethiopia nafasi ya saba, Zambia nafasi ya nane, Kenya nafasi ya tisa na Senegal ikishika nafasi ya 10.

Ripoti hiyo imeitaja Tanzania kuwa nchi ya 13 kwa kuwa na kuvutia uwekezaji. Nchi 10 ambazo zimetajwa kuwa hazivutii uwekezaji ni;
1. Afrika ya Kati
2. Liberia  
3. Somalia  
4. Eritrea
5. Equatorial Guinea
6. Gambia
7. Sierra Leone
8. Guinea  
9. São Tomé and Príncipe
10. Zimbabwe

WAZIRI MKUU AZINDUA MBIO ZA MWENGE MKOANI GEITA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwansha Mwenge wa Uhuru kuzindua mbio zake kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018 Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mwenge wa Uhuru kiongozi wa vijana sita watakaokimbiza Mwenge huo, Charles Kabeho wakati alipozindua mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018. Wapili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMATATU YA PASAKA APRIL 02, 2018 YA UDAKU, MICHEZO NA HARDNEWS




Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz

MPENZI WA CRISTIANO RONALDO APOST INSTAGRAM KWA KISWAHILI

Lugha ya Kiswahili inazidi kukuwa na kuwavutia watu wengi dunia, jana April 1, 2018 moja kati ya post za mitandao ya kijamii zilizochukua headlines ni post ya mwanamitindo Georgina Rodríguez ambaye ni mpenzi wa staa wa soka wa Real Madrid Cristiano Ronaldo.

Georgina Rodríguez ni mwanamitindo na ndio mpenzi wa sasa wa Ronaldo na wamefanikiwa kupata mtoto mmoja anayejulikana kwa jina la Alana Martina, hivyo katika insta story yake amepost picha yake na Ronaldo na kuandika ‘Hakuna Matata’

Msemo wa hakuna matata ni msemo wa Kiswahili ambao umeonekana kupendwa na umekuwa msemo maarufu sana kwa wageni wanaopenda kujua lugha ya Kiswahili, huo huwa ni msemo wao wa kwanza kujifunza lakini haijajulkana bado Georgina Rodríguez ameujulia wapi msemo huo.


Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz

AL SHABAAB WAVAMIA KAMBI YA AU NA KUDAI KUUA WANAJESHI 59

Wanamgambo wa kiislamu (Al-Shabaab) wamefanya shambulizi kwenye kambi ya wa jeshi la Muungano wa Afrika AU nchini Somalia.

Wanamgambo hao walilipua mabomu yaliyokuwa yametegwa ndani ya magari mawili nje ya kambi ya jeshi kwenye mji wa Bulamarer, kusini magharibi mwa Mogadishu.

Wenyeji wanasema kuwa walisikia makabiliano makubnwa ya risasi ambayo yalidumu kwa zaidi ya saa tatu.

Msemaji wa Al Shabaab alisema wapiganaji wake 14 waliuawa huku wanajeshi 59 wa AU wakiuawa. Bado madai hayo hayajathitishwa.

Miaka ya hivi karibuni, wanamgambo wa kislamu wamepoteza udhibiti wa miji ya Somalia lakini mara kwa mara hulipua mabomu na kuswashambulia walinda amani.

Sunday, April 01, 2018

MELI YA ABIRIA ILIYOZAMISHWA MWAKA 1942 YATOLEWA BAHARINI

SS Sagain kabla ya kushambuliwa.

Meli ya abiria ya Uingereza iliyozamishwa wakati ilishambuliwa kwa bomu na ndege za Japan wakati wa vita vya pili vya dunia, imeinuliwa kutoka baharini pwani mwa Sri Lanka baada ya miaka 75.

 SS Sagain, ambayo abiria wake wengi na mizigo iliokolewa mwaka 1942, imeinuliwa na kundi la wapiga mbizi kutoka kwa jeshi la wanaji wa Sri Lanka.

HII NDIO SABABU YA KKKT IRINGA KUSITISHA KUSOMA WARAKA WA PASAKA

Askofu wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Blaston Gavile akitoka ibadani baada ya kumalizika ibada ya kwanza leo usharika wa kanisa kuu.

Askofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT)  dayosisi ya Iringa Blaston Gavile leo amesitisha kusoma waraka wa maaskofu wa kanisa hilo kama ilivyopangwa kwa madai ya kuvuja kwa waraka huo.

Akitoa salamu za pasaka mara baada ya ibada ya kwanza katika usharika wa kanisa kuu leo, askofu Gavile alisema ilipangwa kusomwa waraka ila umesitishwa kusomwa baada ya kuvuja hivyo anayehitaji kusoma waraka huo wa kitume afike ofisini auchukue ila hautasomwa tena kanisani.

Na Matukio Daima.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI YA PASAKA APRIL 01, 2018 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS

http://jambotz.co.tz/  Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz

FELIX TSHISEKEDI ACHAGULIWAKUWA MGOMBEA URAIS DRC

Chama kikuu cha upinzani kimemchagua leo (Jumamosi) mwanae muasisi wa chama hicho Felix Tshisekedi kama mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Muungano huo wa pinzani UDPS unasema Felix Tshisekedi, mwana wa waziri mkuu wa zamani wa taifa hilo Etienne Tshisekedi, aliyefariki dunia mjini Brussels mwezi wa February mwaka jana, ndiye atakayekuwa mgombea wake katika uchaguzi wa mwezi Disemba.

Uchaguzi wake umefanyika baada ya mkutano wa wajumbe wa chama hicho uliofanyika usiku kucha katika mji mkuu Kinshasa.

JAMBO TZ INAWATAKIA PASAKA NJEMA

 Jambo Tz Inawatakia Wakristo Wote Pasaka Njema 

Wednesday, March 28, 2018

TANESCO KUTUMIA MFUMO MPYA WA MALIPO YA SERIKALI KUUZA UMEME WA LUKU

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema wateja wake wote wanaotumia mita za malipo ya kabla yaani (LUKU) kuwa, kuanzia April 2, mwaka huu shirika hilo itahamia rasmi katika mfumo wa malipo wa Serikali ujulikanao Government e-Payment Gateway (GePG).

Mfumo utaanza kutumika kutokana na matakwa ya sheria kwa taasisi za Serikali. Taarifa ya Ofisi ya Uhusiano ya TANESCO makao makuu imeeleza kuwa shirika hilo ni miongoni mwa Taasisi za Serikali, hivyo itaanza kutumia mfumo huu kwa kufanya mauzo ya LUKU kupitia ofisi zake kampuni za simu pamoja na benki zote zinazofanya mauzo ya LUKU kupitia huduma za kibenki. 

"Serikali kwa kushirikiana na wataalamu wa TANESCO itahakikisha kuwa mfumo huu unafanya kazi bila kuathiri manunuzi ya LUKU. Ifahamike TANESCO ni miongoni mwa Taasisi za Serikali zitakazotumia mfumo huu mpya na hadi hivi sasa taasisi nyingine za Serikali zimeshaanza kutumia kwa mafanikio.

DIAMOND, MWAKYEMBE, SHONZA WAMALIZA BIFU LAO

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe jana Jumanne Machi 27, 2018 amekutana na mwanamuziki Nassibu Abdul 'Diamond Plutnumz' jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kaimu mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini, Lorietha Laulence imesema lengo la kukutana kwa wawili hao ni kulejesha maelewano kwenye tasnia ya muziki kufuatia hatua zinazochukuliwa na Wizara hiyo kufungia baadhi ya nyimbo zikiwemo mbili za mwanamuziki huyo.
Imeeleza kuwa katika kikao hicho kilichofanyika ofisi za Wizara hiyo na kuchukua zaidi ya saa tatu, kiliudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Juliana Shonza, katibu mtendaji wa Balaza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mwingereza.

VIWANJA VYA NDEGE 10 BORA HIVI HAPA

Tovuti ya utafiti wa anga ya Skytrax ya nchini Uingereza imetoa orodha ya viwanja vya ndege bora duniani ambapo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Singapore Changi umeshika nafasi ya kwanza.



Orodha ya viwanja 10 vinavyoongoza kwa ubora ni;
1. Singapore Changi Airport
2. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Incheon (Seoul, Korea Kusini)
3. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Tokyo Haneda)
4. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hong Kong
5. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamad (Doha, Qatar)
6. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Munich (Ujerumani)
7. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chubu Centrair Nagoya (Japan)
8. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa London Heathrow
9. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zurich (Switzerland)
10. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Frankfurt (Ujerumani)

JESUS AWAFUTA MACHOZI BRAZIL

Timu ya taifa ya Ujerumani walishindwa kwa mara ya kwanza katika mechi 23 baada ya mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus kuwafungia Brazil bao moja na kuwapa ushindi wa 1-0 jijini Berlin.

Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa mataifa hayo mawili kukutana uwanjani tangu Ujerumani walipowaaibisha Brazil 7-1 katika nusu fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2014 mjini Belo Horizonte.
Jesus aliwaweka Brazil mbele kwa mpira wa kichwa dakika za mwishi mwisho kipindi cha kwanza, dakika ya 37.

ARGENTINA WACHEZEA KICHAPO KITAKATIFU TOKA KWA UHISPANIA

Katika mchezo uliochezwa jana Mjini Madrid, Isco alifunga mabao matatu na kuwasaidia Uhispania kupata ushindi mnono wa 6-1 dhidi ya Argentina ambao walifika fainali Kombe la Dunia 2014.

Uhispania waliongoza 2-0 baada ya Diego Costa kumbwaga Sergio Romero kisha Isco akafunga bao lake la kwanza.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...