Chama kikuu cha upinzani
kimemchagua leo (Jumamosi) mwanae muasisi wa chama hicho Felix
Tshisekedi kama mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Muungano
huo wa pinzani UDPS unasema Felix Tshisekedi, mwana wa waziri mkuu wa
zamani wa taifa hilo Etienne Tshisekedi, aliyefariki dunia mjini
Brussels mwezi wa February mwaka jana, ndiye atakayekuwa mgombea wake
katika uchaguzi wa mwezi Disemba.
Uchaguzi wake umefanyika baada ya mkutano wa wajumbe wa chama hicho uliofanyika usiku kucha katika mji mkuu Kinshasa.
Tshisekedi pia amechaguliwa kuongoza chama kwa idadi kubwa ya kura...akijizolea kura 790 kati ya 803 za wajumbe wa chama. "Nina imanikwamba UDPS itaingia madarakani mwaka huu kuweka mambo sawa nchini''
" alisema Tshisekedi
Uchaguzi
wa rais nchini DRC unatarajiwa kufanyika tarehe 23 Disemba baada ya
kuahirishwa mara mbili, jambo lililosababisha ghasia zilizohofiwa
kuliingiza taifa hilo vitani.
Rais Joseph Kabila amekuwa madarakani tangu mwaka 2001 na alitakiwa
kuondoka madarakani mwishoni mwa mwaka 2016 baada ya kumaliza mihula
yake miwili inayokubalika kikatiba.
Hofu juu ya hatma ya rais
Kabila mamlakani ilitawala miongoni mwa raia walioanzisha maandamano
yaliyokabiliwa na mashambulio ya vikosi vya serikali pamoja na kukamatwa
kwa waandamanaji.
Ghasia za maandamano ya upinzani zinakadiriwa kuwauwa makumi kadhaa ya watu.
Kulingana na matokeo ya kura ya maoni yaliyotangazwa Ijumaa, asilimia 69
ya raia hawana imani kwamba tume ya uchaguzi nchini humo inaweza
kuendesha uchaguzi wa haki na asilimia 80 wana maoni hasi juu ya kabila.
Asilimia 66 wangependelea kumchagua mgombea wa upinzani na kabila angepata asilimia sita tu iwapo angetaka kugombea tena urai. Muungano wa upinzani UDPS wulianzishwa mnamo mwaka 1982 wakati wa utawala wa dikteta Mobutu Sese seko.
Umekuwa katika upinzani tangu wakati huo na umekuwa ukitawaliwa na mgawanyiko miongoni mwa wanachama wake.
No comments:
Post a Comment