Kamanda wa Polisi mkoa Arusha, Liberatus Sabas .
Kamanda wa Polisi mkoa Arusha, Liberatus Sabas amesema jeshi hilo limebaini vikundi vilivyojipanga kufanya vurugu na akavitaka kuacha kutekeleza mpango huo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda Sabas alisema wamebaini kuwa zaidi ya vijana 100 wamesambazwa mjini Arusha na Arumeru kwa ajili ya kufanya vurugu wakati wa uchaguzi.
Alisema polisi wamejipanga kukabiliana na uhalifu au vurugu zozote zitakazotokea katika kipindi cha uchaguzi kwa kuwa tayari wamepokea tetesi za kuwapo kwa makundi hayo.
“Natoa onyo kwa hayo makundi kuwa kama wanataka usalama waache mara moja kwa kuwa hawatakuwa salama,” alisema Liberatus.