Monday, September 28, 2015

MGOMBEA UBUNGE WA CHADEMA DODOMA MJINI APATA DHAMANA

Mgombea ubunge wa jimbo la Dodoma mjini kupitia
Mgombea ubunge wa jimbo la Dodoma mjini kupitia Chadema, Benson Kigaila  

Ulinzi mkali leo umewekwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Dodoma ili kuzuia wafuasi wa Chadema waliokwenda kusikiliza kesi inayomkabili mgombea ubunge wa jimbo la Dodoma mjini Benson Kigaila na kusababisha lango la kuingilia lifungwe.

Kigaila na wenzake 10 wanakabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo kumpiga na kumjeruhi polisi, kufanya maandamano bila ya kibali na pamoja na kutoa lugha za matusi katika kituo cha polisi makosa ambayo watuhumiwa hao waliyakana yote.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, James Karayemaha, Wakili wa Serikali Beatrice Nsana amesema kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa yote Septemba 25 mwaka huu majira ya jioni.
Nsana amesema kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba mahakama ipange tarehe ya kuanza kusikilizwa ambapo mahakama imekubali na kupanga Oktoba 12 mwaka huu huku dhamana ikiwa wazi.
Mara baada ya kutimizwa kwa masharti ya dhamana kwa washitakiwa wote, viongozi hao waliondoka chini ya ulinzi mkali wa polisi na kusindikizwa hadi katika ofisi za kanda za chama hicho ambako Kigaila alizungumza na waandishi wa habari. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...