Wednesday, September 09, 2015

WANNE WAJITOSA KUWANIA UMUFTI WA TANZANIA


KAIMU Mufti wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata), Shekhe Abubakar Zuberi Ally ni miongoni wa mashehe wanne waliojitokeza kuwania kuchaguliwa kwenye nafasi ya Mufti kwenye uchaguzi utakaofanyika kesho jijini hapa. 

Akizungumza jana, Shehe wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajab aliwataja mashekhe wengine waliochukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi hiyo kuwa ni Ally Muhidin Mkoyogole, Khamis Abbas Mtupa na Hassan Ibrahim Kiburwa. 

Alisema maandalizi ya mkutano mkuu kwa ajili ya uchaguzi huo, yamekamilika na kwamba wajumbe zaidi ya 550 kutoka mikoa mbalimbali, wameanza kuingia. Katika mkutano huo wa uchaguzi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. 

Alisema wajumbe wa mkutano huo wa kumchagua Mufti wa kuiongoza Bakwata ni wengi, ambapo utawashirikisha mashekhe wote wa mkoa, wilaya, mwenyeviti na makatibu wa mkoa na wilaya na Baraza la Maulamaa, pia viongozi wa serikali wataalikwa.

Alisema Mufti atakayechaguliwa atakuwa wa awamu ya tatu, ambapo walitanguliwa na Mufti Hemed Bin Jumaa bin Hemed na Mufti Issa Bin Simba aliyefariki dunia Juni 22, mwaka huu katika Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...