Monday, October 05, 2015

DEREVA BODABODA AUAWA NA KUNYOFOLEWA KICHWA NA SEHEMU ZA SIRI



 Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wakiwa katika kijiwe chao. PICHA NA MAKTABA

Watu wasiofahamika wamemuua kwa kumchinja mwendesha pikipiki maarufu kama bodaboda, Hosam Abdallahaman (18) na kutoweka na kichwa chake, sehemu zake za siri na pikipiki.   

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo juzi usiku katika Kijiji cha Silimka, Kata ya Itilo wilayani hapa.



Kamanda Issa alisema kabla ya mauaji hayo, saa moja usiku, Hosam alikodiwa na abiria ampeleke eneo la Silimka na hakurudi kwenye kituo chake cha kazi hadi alipokutwa akiwa ameuawa majira ya saa 4 asubuhi siku iliyofuata. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
Alisema hadi sasa kichwa na sehemu za siri za kijana huyo na pikipiki havijapatikana.
Alisema polisi wanaendelea kuwasaka watuhumiwa hao wa mauaji ili wakamatwe na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji na uporaji wa pikipiki.

Baba mzazi wa Hosamu, Abdullahaman Sudeni maarufu kwa jina la Babu Trans, alisema mauaji hayo yamemshtusha na kwamba, kinachomsikitisha ni kukosa fursa ya kuuona mwili wa kijana wake huyo kutokana na kuharibika vibaya.

“Mwanagu alikuwa mtulivu nasikitika, Mungu amrehemu, kwani atafika peponi namshukuru Mungu tu japo sijapata hata fursa ya kuuona mwili wake, nilikatazwa na majirani zangu, amezikwa bila kichwa, bila sehemu za siri naomba jeshi la polisi lifanye kazi yake,” alisema huku akibubujikwa na machozi.

Baadhiya wakazi wilayani hapa, wamelaani vikali mauaji hayo huku wakiwaomba polisi kuhakikisha wauaji hao wanakamatwa na sheria kuchukua mkondo wake.

Mwenyekiti wa Bodaboda wa Wilaya ya Nzega, Burabuza aliyefahamika kwa jina moja la Joseph, amelaani mauaji hayo na kuahidi kutoa ushirikiano kwa polisi ili kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa na kufikishwa mahakamani. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...