Friday, June 26, 2015

AL-SHABAAB YASHAMBULIA KITUO CHA AMISOM

Kituo cha kijeshi cha wanajeshi wa kimatifa wa kulinda amani nchini Somalia Amisom. 

Takriban watu 30 wamepoteza maisha yao baada ya shambulizi la kigaidi katika kituo cha kijeshi cha wanajeshi wa kimatifa wa kulinda amani nchini Somalia Amisom.

Walioshuhudia wanasema kuwa mlipuaji wa kujitolea mhanga aliendesha gari lake moja kwa moja hadi kwenye lango kuu la kituo hicho .

Kituo hicho kiko katika eneo la Leego, barabara kuu inayounganisha mji mku wa Mogadishu na Baidoa.

BURUNDI KUENDELEA NA RATIBA YA UCHAGUZI

Gervais Rufyikiri aliyekuwa makamu wa rais wa Burundi amekimbilia Ubelgiji. 

Serikali ya Burundi imesema haitashiriki katika mazungumzo yaliyodhaminiwa na Umoja wa Mataifa yakilenga kupunguza hali ya uhasama uliopo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wenye utata.

MKWASA AWAOMBA MASHABIKI WA SIMBA WASIMZOMEE

Kocha wa timu ya soka ya Taifa ya Taifa Stars, Charles Mkwasa.

KOCHA mpya wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amewataka mashabiki wa Simba kutomzomea pindi watakapomuona kwenye mazoezi au mechi, kwa vile atakuwa pale kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya wachezaji wake wa timu ya taifa. 

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Mkwasa alisema mashabiki wanatakiwa kufahamu kuwa yeye ni kocha wa taifa, hivyo atakuwa akitembelea katika mechi za timu mbalimbali kuangalia wachezaji na maendeleo ya wale wanaocheza timu ya taifa.

“Mashabiki wa Simba mnaponiona kwenye mechi zenu msinikimbize kwa mawe mkadhani kuwa nimekuja kwa ajili ya Yanga, nitakuwa na utaratibu wa kutembelea timu kuangalia wachezaji, mnajua kazi ya kocha wa taifa ndio hiyo,” alisema Mkwasa ambaye pia ni Kocha Msaidizi wa Yanga.

TAMBWE AIPANIA KAGAME

Amissi Tambwe

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe amesema anategemea kufanya vizuri zaidi katika michuano ijayo ya Kagame kuisaidia timu kuchukua taji katika michuano hiyo itakayofanyika nchini kuanzia mwezi ujao. 

Tambwe, ambaye aliwahi kufanya vizuri katika michuano hiyo iliyofanyika Sudan miaka miwili iliyopita kwa kuibuka mfungaji bora, aliliambia gazeti hili kuwa anajipanga kufanya vizuri zaidi.

Mchezaji huyo aliibuliwa na Simba katika michuano hiyo wakati akiichezea Vital’O ya Burundi iliyochukua ubingwa wakati huo, kutokana na kuisaidia timu yake kwa kiasi kikubwa na kufanya vizuri.

ENGLAND YATETEA WACHEZAJI CHIPUKIZI

Timu ya England U21 katika moja ya michezo yao ya michuano ya Ulaya

England imefanya uamuzi sahihi kuwaondoa katika michuano ya ubingwa wa Ulaya kwa wachezaji wa umri chini ya miaka 21, baadhi ya wachezaji wake ambao wanacheza ligi kuu ya nchi hiyo, amesema mkurugenzi wa chama cha soka wa maendeleo ya wachezaji Dan Ashworth.

Timu ya England chini ya kocha Gareth Southgate ilifuzu kucheza hatua ya makundi kwa kwenda Jamhuri ya Czech. "Tulifanya uamuzi na nautetea ," Ashworth amemwambia mwandishi mwandamizi wa BBC wa habari za mpira wa miguu Ian Dennis. 

"Timu za vijana zipo kusaidia kuwakuza wachezaji na kuwapa uzoefu kuingia katika timu ya wakubwa." Mchezaji wa ushambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling, kiungo wa Everton Ross Barkley, viungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain na Jack Wilshere na mlinzi wa Manchester United Phil Jones ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wakihitajika katika timu hiyo, lakini hawakuitwa.

England, ambayo ilikuwa na wachezaji wa ligi kuu, akiwemo mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, mlinzi wa Everton John Stones na mshambuliaji mpya wa Liverpool Danny Ings, ilipoteza kwa Ureno 1-0 , wakaifunga Sweden kwa idadi kama hiyo lakini ilipoteza 3-1 kwa Italia.

Wednesday, June 24, 2015

WAZIRI GHASIA, KAFULILA WATOFAUTIANA BUNGENI

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila 

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia jana walitofautiana bungeni kuhusu tuhuma za ubadhirifu wa fedha zinazomkabili Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Hadija Nyembo.

Tukio hilo lilitokea baada ya swali la nyongeza la mbunge huyo, aliyetaka kujua msimamo wa serikali kuhusu Nyembo aliyedai kutoa kauli ya kutaka Wabembe waende kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) iliyosababaisha Wabembe kukamatwa na kupelekwa ubalozini, ambapo ubalozi wa DRC , uliwakataa na kusababisha wanyanyasike kwa karibu wiki mbili. 

Pia Mbunge huyo alidai Mkuu huyo wa Wilaya aliondolewa wilayani Chato akihusishwa na ufisadi wa mbolea yenye thamani ya Sh bilioni 1.5 na kwamba sasa ana kesi katika Mahakama ya Wilaya ya Chato, hivyo serikali haioni aibu kuwa na Mkuu wa Wilaya wa aina hiyo, ambaye anashitakiwa na serikali yenyewe.

IS YAPATA WAFUASI WAPYA WA KANDA YAO

Mpiganaji wa IS

Kundi la kigaidi la wanamgambo wa kiislam, maarufu kama Islamic State limekubali ombi na ahadi ya wanamgambo wa kutoka kusini mashariki mwa Asia na Ulaya kusini magharibi katika maeneo ya Chechnya and Dagestan.

Hii ni mara ya kwanza kwa kundi hilo la IS kukaribisha rasmi kundi la wanajihadi kutoka katika kanda yao kuingia katika shirika lake. 

Na hii inaelezwa kwamba imekuja baada ya Vyombo vya habari vinavyotangaza kwa lugha ya lugha ya Kirusi mwishoni mwa wiki iliyopita, kurushwa kwa kipande cha video kinachomuonesha kiongozi mkuu wa kijeshi kutoka Chechnya akiapa na kuahidi kujitoa sadaka na kuwa kuwa mtii kwa IS.

Taarifa za awali zinaeleza kwamba kundi kubwa la kigaidi lenye kujitoa muhanga la Chechnya lilikuwa likipinga harakati za Is.

MTUNZI WA FILAMU YA TITANIC AFARIKI DUNIA

James Horner, enzi za uhai wake.

James Horner mtunzi nguli wa eneo maarufu kwa watu maarufu la Hollywood ambaye aliandika na kushinda katika tuzo za Oscar juu ya filamu maarufu ulimwenguni ya Titanic, amefariki dunia mjini California kutokana na ajali ya ndege akiwa na umri wa miaka 61. 

James alipata mafunzo ya urushaji wa ndege, inaarifiwa alikuwa peke yake wakati alipopata ajali hiyo, na ndege binafsi ndogo ambayo alipata nayo ajali eneo la Kusini mwa Santa Barbara mwanzoni mwa wiki hii.

Mwandishi huyu na mtunzi wa tungo mbali mbali ametia mkono wake katika kazi tatu tofauti za filamu za msanii James Cameron, pamoja na filamu ya A Beautiful Mind, Braveheart, Troy na ile ya Apollo 13.

TAIFA STARS YAPATA KOCHA MZAWA....!!!


Kocha mpya wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa 

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania - TFF, Jamal Malinzi leo ameagana rasmi na aliyekua kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania mholanzi Mart Nooij na kumtangaza Charles Boniface Mkwasa kuwa kocha mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania akisaidiwa na Hemed Moroco.

Malinzi amesema kwamba, kocha mpya wa timu ya taifa, Charles Boniface Mkwasa atakuwa analipwa sawa na kocha Mholanzi, Mart Nooij aliyeondolewa.

Nooij aliyekuwa analipwa dola za Kimarekani 12,500 (zaidi ya Sh. Milioni 25) kwa mwezi, alifukuzwa mwishoni mwa wiki baada ya Taifa Stars kufungwa mabao 3-0 na Uganda Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Wednesday, June 17, 2015

PROF. LIPUMBA, DK. SLAA, ZITTO, KUVAANA KWENYE MDAHALO

Dk.Wilbroad Slaa akiwa na Profesa Ibrahim Lipumba 

Umoja wa watendaji wakuu wa kampuni wa CEO RoundTable (CEOrt) umeandaa mdahalo wa kuzungumzia mbio za urais utakaowahusisha viongozi wa vyama vya upinzani, Profesa Ibrahim Lipumba, Dk Willibrod Slaa, Zitto Kabwe na Emmanuel Makaidi, lakini Chadema imesema itakuwa tayari kwa midahalo baada ya mchakato wa ndani kukamilika.

Kauli hiyo ya Chadema inaweza kuwa kikwazo kingine kwa CEOrt kuendesha midahalo hiyo baada ya wa kwanza uliokuwa uhusishe makada 10 wa CCM wanaoomba ridhaa ya chama hicho kuwania urais, kushindwa kufanyika kutokana na viongozi wa sekretarieti kutoa kauli tofauti siku moja kabla.

Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNI 17, 2015 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.


. .
 Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

SERIKALI YA MUUNGANO WA PALESTINA KUVUNJIKA


Rais Mahmoud Abbas wa Palestina
Rais wa Palestina amesema kuwa serikali ya muungano kati yake na wanamgambo wa Hamas itavunjika.
Bwana Mahmud Abbas ameliambia vuguvugu lake la Fatah, kuwa lazima uhusiano huo uvunjike kwa kuwa Hamas haitairuhusu serikali yake kuendesha shughuli katika eneo la Gaza, ambako wameshikilia wao.
Kiongozi wa Hamas kushoto Khaled Meshaal na rais wa Palestina Mahmoud Abbas
Serikali hiyo iliundwa mwaka uliopita na ilitarajiwa kumaliza uhasama kati ya makundi hayo mawili lakini malengo yake yamekumbwa na matatizo mengi.
Hamas wanaongoza Gaza ilhali kundi la bwana Abbas la Fatah limeshikilia maeneo ya wa Palestina ya West Bank.

 Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

OPERATION ZA UN ZIFANYIWE MABADILIKO

Baraza la usalama la umoja wa mataifa
Ripoti iliyoandaliwa kwa hisani ya umoja wa mataifa imeelezea kuwa oparesheni za kulinda usalama za shirika hilo zinahitaji kufanyiwa mabadiliko makubwa.
Ripoti hiyo imekusanywa baada ya madai kutolewa hivi karibuni dhidi ya vikosi vya umoja huo vya kulinda amani kwamba baadhi wamekuwa wakiwanyanyasa kingono watoto wadogo.
Miongoni mwa mapendekezo ya ripoti hiyo ni kuwa nchi ambako maafisa husika wanatoka, zisikubaliwe kuchangia tena wanajeshi katika vikosi vya umoja wa mataifa.
Pia ripoti hiyo inasema kuwa wanajeshi waliotajwa kuhusika na uovu huo wanastahili wakabiliwe na sheria, na nchi zao pia zinafaa kushurutishwa kueleza wazi ni hatua zipi za adhabu zilizochukuliwa dhidi yao.
Pendekezo jingine lililotolewa katika ripoti hiyo ni kuwa madai yote ya unyanyasaji wa ngono yanastahili kufanyiwa uchunguzi wa kina kwa chini ya miezi sita.
 Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

RATIBA YA MECHI ZA EPL YATOLEWA


Meneja wa Chelsea Jose Mourinho
Chelsea itaanza utetezi wa taji la ligi ya Uingereza wakati itakapoikaribisha nyumbani Swansea katika wikiendi ya tarehe 8-9 mwezi Agosti.
Manchester City iliomaliza pointi nane nyuma ya Chelsea itaelekea West Bromwich huku Manchester United ikikabiliana na Tottenham katika uwanja wa Old Trafford.
Arsenal
Arsenal itaialika West Ham ,Liverpool ikienda Stoke,Newcastle itakabiliana na Southampton huku Leicester ikiialika Sunderland nyumbani.
Bournemouth iliopandishwa daraja,Watford na Norwich zitakabiliana na Aston Villa,Everton na Crystal Palace mtawalia.
Manuel Pellegrini
Msimu huu utanza wiki moja mapema ikilinganishwa na msimu uliopita.  Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

MAN CITY YATOA MILIONI 35 KUMNUNUA STERLING

Man City yatoa pauni milioni 35m kumnunua Raheem Sterling

Klabu ya Manchester City imeimarisha ombi la kumsajili mashambulizi machachari wa Liverpool Raheem Sterling.
Mabingwa hao wa mwaka wa 2014 wametoa pauni milioni 35 sawa na dola milioni 55 kusajili huduma za mshambulizi huyo.
The Reds walikataa ombi la kwanza la kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 wakisema thamani yake ni pauni milioni 50.
Kuwepo kwa mchezaji huyo raia wa Uingereza katika soko kumetokana na nia yake ya kuondoka Liverpool .
Sterling alijiunga na Liverpool mwaka wa 2010 akitokea QPR kwa mkataba utakaomalizika mwaka wa 2017.
Brendan Rodgers anamtarajia Sterling kusalia Anfield hadi kandarasi yake itakapokatika 2017.
Hata hivyo alizua mjadala baada ya kuzima pendekezo la nyongeza ya mshahara wake hadi pauni laki moja kwa wiki.
Manchester City inaaminika kuwa iko tayari kutoa marupurupu mengine yatakayofikisha gharama yake hadi pauni milioni 40 japo wanalalamika kuwa Liverpool imeongeza maradufu thamani yake ikifahamika kuwa wenyewe hawakuwa hata wakimlipa pauni laki moja kwa juma.
Kwa upande wake kocha Brendan Rodgers anashikilia kukutu kuwa anamtarajia Sterling kusalia Anfield hadi kandarasi yake itakapokatika.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...