Friday, June 26, 2015

AL-SHABAAB YASHAMBULIA KITUO CHA AMISOM

Kituo cha kijeshi cha wanajeshi wa kimatifa wa kulinda amani nchini Somalia Amisom. 

Takriban watu 30 wamepoteza maisha yao baada ya shambulizi la kigaidi katika kituo cha kijeshi cha wanajeshi wa kimatifa wa kulinda amani nchini Somalia Amisom.

Walioshuhudia wanasema kuwa mlipuaji wa kujitolea mhanga aliendesha gari lake moja kwa moja hadi kwenye lango kuu la kituo hicho .

Kituo hicho kiko katika eneo la Leego, barabara kuu inayounganisha mji mku wa Mogadishu na Baidoa.


Wanamgambo hao wa Al shabaab wamesema wameteka kituo hicho, lakini wanajeshi wa muungano wa Afrika nchini humo , AMISON wamekanusha madai hayo

AMISOM inasema kuwa wanajeshi wake wanaendelea kukabiliana na wanamgambo hao wa kiislamu.

Kundi la al shabaab limeimarisha mashambulio ya kigaidi tangu kuanza kwa mwezi mtukufu wa mfungo wa ramadan.


Kituo hicho kinaendeshwa na wanajeshi kutoka Burundi chini ya mwavuli wa (Amisom). Jeshi hilo linazaidi ya askari 20,000 kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...