Friday, June 26, 2015

TAMBWE AIPANIA KAGAME

Amissi Tambwe

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe amesema anategemea kufanya vizuri zaidi katika michuano ijayo ya Kagame kuisaidia timu kuchukua taji katika michuano hiyo itakayofanyika nchini kuanzia mwezi ujao. 

Tambwe, ambaye aliwahi kufanya vizuri katika michuano hiyo iliyofanyika Sudan miaka miwili iliyopita kwa kuibuka mfungaji bora, aliliambia gazeti hili kuwa anajipanga kufanya vizuri zaidi.

Mchezaji huyo aliibuliwa na Simba katika michuano hiyo wakati akiichezea Vital’O ya Burundi iliyochukua ubingwa wakati huo, kutokana na kuisaidia timu yake kwa kiasi kikubwa na kufanya vizuri.

“Ni kazi yangu kuhakikisha nafanya vizuri katika timu, ndio maana kila siku najituma kuwezesha timu yangu kushinda, na kwa sasa najipanga kwa ajili ya Kagame nikitegemea kufanya makubwa zaidi,” alisema.

Alisema kwa mbinu ambazo aliwahi kuzionesha Sudan akiwa na timu yake ya zamani atazitumia kuipa ushindi Yanga.

Mchezaji huyo aliyejiunga na Yanga msimu uliopita, ni miongoni mwa wachezaji waliokisaidia kikosi hicho cha Jangwani kuchukua taji la ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita.

Aliahidi kufanya vizuri zaidi ikiwezekana kujitahidi kufungwa na kuwa mfungaji bora katika michuano yote ijayo.

Mrundi huyo ni kati ya wachezaji tegemeo wa kikosi cha Yanga wanaotarajiwa kushuka dimbani kesho katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Sports Villa ya Uganda, mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...