Mbunge wa Arumeru Mashariki(Chadema) Joshua Nassari akiwa amelazwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi), jana, baada ya kuhamishwa kutoka Arusha kwa ajili ya kupata matibabu zaidi baada ya kuumizwa kwenye vurugu za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Makuyuni mkoani Arusha.Picha na Silvan Kiwale.
DAR ES SALAAM.
MBUNGE wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amemtuhumu Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kwamba anahusika na kipigo alichokipata kutokana na chuki aliyonayo kwake.
MBUNGE wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amemtuhumu Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kwamba anahusika na kipigo alichokipata kutokana na chuki aliyonayo kwake.
Aidha
amemtuhumu Spika wa Bunge, Anne Makinda kwamba naye ni miongoni mwa
watu wanaomchukia pamoja na viongozi wengine wa Bunge, kwa kuwa hakuna
kati yao aliyempigia simu au kumtumia ujumbe wa kumjulia hali kutokana
na kipigo alichopata ambacho kimemsababishia maumivu makali.
Akizungumza jana akiwa kwenye chumba alicholazwa katika Taasisi ya Tiba ya Magonjwa ya Mifupa
na Ufahamu Muhimbili (Moi), Nassari alidai Lowassa ambaye amewahi kuwa
waziri mkuu kabla ya kujiuzulu, amemchukia tangu alipomshinda mkwewe
Sioi Sumari, kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika Aprili mwaka
jana.
Nassari
aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Selian ya jijini Arusha kabla
ya kuhamishiwa MOI, alidai kupigwa na kuchaniwa nguo na Green Guard
wakati alipokuwa katika jitihada zake za kuhesabu kura kwenye uchaguzi
wa udiwani wa Kata ya Makuyuni-Monduli.