Rais Jakaya Kikwete (katikati) akipita kwenye daraja la waenda kwa miguu
la Mabatini, Mwanza jana, baada ya kulizindua, daraja hilo limeghalimu
kiasi cha sh8bilioni litasaidia kuondoa tatizo la ajali zilizokuwa
zikitokea mara kwa mara eneo hilo. kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dk. John
Magufuli.
Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje jana
amebadilisha upepo kwenye mkutano wa Rais Jakaya Kikwete, kwa kueleza
kuwa miradi yote ya Serikali ni fedha za wananchi.
Wenje alisema hayo alipopewa nafasi ya kuzungumza
kwenye viwanja vya Mabatini mkoani hapa, akidai kuwa miradi yote
inayotekelezwa na Serikali ni kodi za wananchi wala siyo fedha za CCM.
Wenje alitoa kauli hiyo mbele ya Rais Kikwete
baada ya Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli kudai kuwa CCM ndiyo
inayotekeleza miradi yote ya maendeleo kupitia ilani yake ya uchaguzi ya
mwaka 2010.
Rais Kikwete alikuwa akizindua daraja ya Mabatini lililojengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh1 bilioni na Kampuni ya Adivance Life.
Kabla hajazungumza Wenje alipopanda jukwaani hapo,
mamia ya watu waliohudhuria uzinduzi wa daraja hilo walianza kupiga
kelele huku wakishangilia kwa kuonyesha ishara ya vidole viwili juu na
kuimba ‘Peoples Power’. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz