Saturday, October 11, 2014

WENJE ABADILI UPEPO MKUTANO WA RAIS KIKWETE

 

Rais Jakaya Kikwete (katikati) akipita kwenye daraja la waenda kwa miguu la Mabatini, Mwanza jana, baada ya kulizindua, daraja hilo limeghalimu kiasi cha sh8bilioni litasaidia kuondoa tatizo la ajali zilizokuwa zikitokea mara kwa mara eneo hilo. kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli.


Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje jana amebadilisha upepo kwenye mkutano wa Rais Jakaya Kikwete, kwa kueleza kuwa miradi yote ya Serikali ni fedha za wananchi.

Wenje alisema hayo alipopewa nafasi ya kuzungumza kwenye viwanja vya Mabatini mkoani hapa, akidai kuwa miradi yote inayotekelezwa na Serikali ni kodi za wananchi wala siyo fedha za CCM.

Wenje alitoa kauli hiyo mbele ya Rais Kikwete baada ya Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli kudai kuwa CCM ndiyo inayotekeleza miradi yote ya maendeleo kupitia ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2010.

Rais Kikwete alikuwa akizindua daraja ya Mabatini lililojengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh1 bilioni na Kampuni ya Adivance Life.

Kabla hajazungumza Wenje alipopanda jukwaani hapo, mamia ya watu waliohudhuria uzinduzi wa daraja hilo walianza kupiga kelele huku wakishangilia kwa kuonyesha ishara ya vidole viwili juu na kuimba ‘Peoples Power’. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Baada ya mbunge huyo kuanza kuhutubia alisema: “Naomba nimjibu Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli kwamba miradi hii siyo ya CCM, bali ni kodi za Watanzania wakiwamo, wakulima, polisi, wafanyabiashara, hivyo asitambe hapa kuwa hii ni nguvu ya CCM siyo kweli hata kidogo.”

Wenje akihutubia kwa jazba alisema kuwa yeye siyo mtu wa kawaida na hana chembe ya CCM wala wasitegemee kuwa yeye ni muumini wa chama hicho.

Alitoa mfano kuwa yeye siyo kama tikiti maji kwamba nje lina rangi ya kijani, lakini ndani lina rangi nyekundu, na kwamba ataendelea kupiga kelele ili CCM waendelee kufanya mambo ya maendeleo, kwani bila hivyo hawawezi kufanya lolote.

Kabla Wenje hajamaliza kuhutubia mkutano huo aliwataka wananchi hao kukunja ngumi ili waagane kwa salamu yao.

“Mheshimiwa Rais hapa Mwanza tuna salamu zetu naomba niage kwa salamu hiyo, haya ndugu zangu naomba tukunje ngumi, koroga koroga, peoples,” alitamka na mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wakaitikia ‘Power’ huku wakinyoosha vidole viwili juu.

Hali hiyo ilisababisha wafuasi wa CCM kuibuka na kuanza kusema CCM oyee, jambo lililosababisha wafuasi hao kuanza kutupiana maneno na kupiga kelele na kusababisha watu kutosikilizana.

Hatua hiyo ilisababisha askari polisi waliokuwa wamevalia sare kuongezwa kwenye uzinduzi huo ili kuimarisha ulinzi.
Awali akihutubia kwenye viwanja vya Kisesa Dk Magufuli alisema kuwa anampongeza Mbunge wa Nyamagana Wenje kwa kuwa na moyo mzuri, huku akisema kuwa wote ndani ya chama chake wangekuwa kama yeye mambo yangekuwa safi.
Dk Magufuli alisema, “Naomba nimpongeze Wenje kwa kuwa na moyo mzuri, kwani ameweza kushiriki na sisi, viongozi wa chama chake wangekuwa kama yeye mambo yangekuwa safi, lakini haya yote ya maendeleo yanafanywa na CCM.”
Akiwa kwenye viwanja vya polisi Mabatini, Dk Magufuli alijibu kauli ya Wenje baada ya kutoa mfano wa tikiti maji kuwa nje lina rangi ya kijani, lakini ndani lina rangi nyekundu.
Dk Magufuli alisema, “Ndugu zangu naomba niwaambie kuwa hata kama ukubali usikubali maendeleo haya ikiwamo ujenzi wa daraja hili ni nguvu za CCM na Wenje anakubaliana na hilo na mmesikia wenyewe kuwa yeye siyo kama tikiti maji, lakini ndiyo hivyo kwani nje rangi yake kijani na ndani nyekundu ndiyo Wenje huyo.”
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga akihutubia baada ya uzinduzi huo alisema kwenye msafara wa kenge na mamba wapo, hivyo hatashangaa kuona wapinzani wanahudhuria sherehe za miradi hiyo kwani wanatambua kazi inayofanywa na CCM. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
JK ahutubia
Akizungumzia na wakazi wa Mabatini na Kisesa, Rais Kikwete alisema kuwa kazi ya kuandika Katiba imemalizika hivyo kazi iliyopo ni wananchi kumalizia kazi yao.
Alisema kwenye Katiba iliyopendekezwa hakuna jambo lililoachwa na kwamba upande wa wanawake asilimia 50 kwa 50 imewekwa na kwamba watalitazama kwa kina kama ikiwezekana uchaguzi ujao suala hilo litumike.
“Ndugu zangu naomba niwaambie kuwa kazi ya Katiba imemalizika, hivyo kilichobaki ni kazi yenu kumalizia. Suala la 50 kwa 50 limewekwa na kwamba tutalitazama kwa kina ili uchaguzi ujao liwepo suala hilo,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
“Lakini haya yote majibu yatatoka baadaye baada ya kulitazama jambo hilo kwanza, lakini kama Katiba haitapita, iliyopo itaendelea kutumika, hivyo msiwe na hofu.”
Azishukia Halmashauri za Jiji la Mwanza
Rais Jakaya Kikwete aliagiza kuwa fedha za mfuko wa barabara ambazo zimekuwa zikitolewa zinapaswa kutumika vyema, ili kukamilisha kazi zilizopangwa.

“Nafahamu kuwa kuna mchwa ambao wanakula fedha za maendeleo, Mwanza kuna kama bilioni saba zimetolewa kwenye mfuko huo, hivyo naagiza zitumike kwenye kazi zilizokusudiwa na zisiishie kulipana posho kwenye vikao vya mabaraza ya madiwani.”
Awali akitoa taarifa ya miradi hiyo, Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroad), Crispianus Ako alisema Barabara ya Usagara Kisesa yenye urefu wa kilometa 16 imejengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh17 bilioni na Kampuni ya Nyanza Road na kwamba imekamilika kwa asilimia 45.
Alisema Daraja la Mabatini limejengwa kwa zaidi ya Sh1 bilioni na kwamba limeakamilika na kuanza kutoa huduma. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
 Na Mwananchi

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...