Jeshi
la kulinda amani la Umoja wa Afrika nchini Somalia limesema askari wake
watatu na kandarasi raia wameuawa katika shambulio lililofanyika katika
makao yake makuu mjini Mogadishu.
Taarifa ya Umoja wa Afrika
imesema wapiganaji wa al-Shabab waliingia katika kambi wakivalia sare
kama askari wa jeshi la serikali ya Somalia.Taarifa hiyo imesema washambuliaji watano waliuawa na wengine kadha kukamatwa. Pamoja na kutoa eneo hilo kuwa makao makuu ya majeshi ya kulinda amani ya AU nchini Somalia, eneo hilo lililoimarishwa pia makao ya balozi za Uingereza na Italia. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Na BBC