Baadhi ya wajumbe
wa Bunge la Katiba waliopiga kura za hapana wamelazimika kuondoka Dodoma
na kurudi Zanzibar kwa madai ya vitisho walivyopata kutoka kwa wenzao.
Mmoja wa wajumbe hao, Salma Said alisema jana
jioni kuwa yeye na wajumbe wenzake wamekataa kuitikia wito wa Mwenyekiti
wa Bunge, Samuel Sitta kwenye Kamati ya Mashauriano ili kuhojiwa kuhusu
kura hiyo na kutokana na vitisho wanavyopata kutoka kwa wajumbe wenzao
wameamua kuondoka Dodoma.
Vitisho hivyo vimeripotiwa muda mfupi baada ya
Sitta kuunda Kamati ya Mashauriano ya watu tisa inayoongozwa na Makamu
Mwenyekiti, Samia Suluhu Hassan kushughulikia kura hizo zilizopigwa na
wajumbe saba zinazoweka njiapanda uwezekano wa kupatikana akidi ya
kupitisha Katiba inayopendekezwa.
Wajumbe waliopiga kura za wazi za hapana kwa ibara
zote ni Adil Mohamed Adil, Dk Alley Soud Nassor, Fatma Mohamed Hassan,
Jamila Ameir Saleh, Salma Hamoud Said, Mwanaidi Othman Twahir na Ali
Omary Juma. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz