Muungano wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Zimbabwe al maarufu Zinasu,
umesema kwamba unawasilisha kesi mahakamani hii leo kutafuta ufafanuzi
zaidi wa namna mkewe rais Grace Mugabe alivyopata shahada ya udaktari wa
falsafa.
Mwanafunzi mmoja mwanaharakati amesema kuwa ni muhimu kwa taifa hilo kuhifadhi hadhi yake ya elimu.Baadhi ya watu wamehoji kasi aliyosomea shahada hiyo huku wengine wakidai ni njama za kumuandaa kwa urithi wa kiti cha rais baada ya rais Mugabe.
Gazeti moja linalomilikiwa na serikali , the Herald limechapisha kuwa Bi Grace Mugabe alipata shahada hiyo kwa utafiti wake juu ya mabadiliko ya mfumo wa kijamii na miundo ya familia. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC
No comments:
Post a Comment