Wednesday, October 01, 2014

DRC: WAPIGANAJI WA ZAMANI WAFA NJAA

Wapiganaji hao wa zamani wamekuwa wakila chakula kutoka kwa mashamba ya wakulima
Shirika moja la kimataifa la kutetea haki za binadamu linasema kuwa zaidi ya watu mia moja wamefariki kutokana na njaa pamoja na maradhi katika kambi moja ya kijeshi katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Shirika hilo Human Rights Watch, limesema kuwa watu hao ambao walikuwa wapiganaji wa zamani na wake zao pamoja na watoto walihamishwa katika kambi nyingine iliyotengwa Kaskazini mwa DRC.
Ilikuwa baada ya wao kujisalimisha kutoka kwa kundi la wapiganaji Mashariki ya nchi.
Walipokea chakula kidogo na huduma ya afya baadhi wakiponea kifo kwa kuiba chakula kutoka kwa mashamba ya wakulima.
Serikali ya DRC inasema kuwa inachunguza ripoti hiyo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...