Sunday, September 28, 2014

SALVA KIIR ATAKA KUSITISHWA KWA VITA

Rais Salva Kiir na Riek Machar wakibadilishana makubaliano ya kusitisha vita
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amesema kuwa serikali yake imejitolea kumaliza vita nchini nchini humo.
Akiongea kwenye mkutano mkuu wa baraza la umoja wa mataifa mjini New York Kiir ameitaka jamii ya kimataifa kuwashinikiza waasi kuheshimu makubaliano ya kusitisha vita.
Vita vya kisiasa nchini Sudan Kusini kati ya rais Kiir na makamu wake wa zamani Riek Machar vimesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwalazimu mamalioni ya wengine kuhama makwao.
Mzozo ulianza mwezi Disemba mwaka uliopita na makubaliano ya kumaliza vita yameshindwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...