Jaja alishindwa kufunga dhidi ya Mtibwa na kwa bahati mbaya alikosa mkwaju wa penalti
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976
YANGA SC wakiwa na kumbukumbu
mbaya ya kufungwa 2-0 katika mechi ya ufunguzi wa ligi kuu soka Tanzania
bara, septemba 20 mwaka huu uwanja wa Jamhuri Morogoro dhidi ya Mtibwa
Sugar, leo jioni wanaikaribisha Tanzania Prisons katika mtanange wa
raundi ya pili uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Prisons wanaingia katika mechi
hiyo wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting
waliopata katika mechi ya ufunguzi iliyopigwa wikiendi ya septemba 20
mwaka huu uwanja wa Mabatini, Mlandizi, mkoani Pwani. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Kocha mkuu wa Yanga, Mbrazil,
Marcio Maximo bila shaka atatumia mbinu ya kushambulia zaidi kwa lengo
la kufunga mabao mengi, lakini akijaza viungo wengi kwa ajili ya
kujilinda.
Maximo hupendelea kuchezesha
viungo wengi na kumsimamisha mshambuliaji wa Kibrazil, Genilson Santos
Santana ‘Jaja’. Ni kocha ambaye huwa hahitaji mabao mengi, anapenda
kufunga goli moja au mawili, halafu anaimarisha ulinzi ili kuvuna pointi
tatu.
Habari njema kwa mashabiki wa
Yanga ni kwamba washambuliaji wawili, Mtanzania, Jerryson John Tegete na
Andrey Coutinho wamerejea baada ya kushindwa kucheza mechi iliyopita
kwasababu ya majeruhi.
Coutinho kipenzi cha mashabiki wa
Yanga ana asilimia ‘200’ za kuanza katika mechi ya leo kuliko Tegete na
maana yake atacheza nyuma ya Jaja.
Kutokana na aina ya uchezaji
wake, amekuwa mwiba kwa mabeki wa timu pinzani kwasababu ana vitu vingi.
Anaweza kupiga chenga, anamiliki mpira, anapiga pasi za mwisho, ana
mashuti ya mbali na kasi nzuri.
Coutinho (kulia) yako fiti kuivaa Prisons leo
Itakuwa mechi yake ya kwanza ya
ligi kuu, lakini alishaonesha uwezo mzuri kwenye mechi za kirafiki
wakati wa maandalizi ya kabla ya msimu.
Kama ataendelea kuwa katika ubora
wake, mabeki wa Prisons wanatakiwa kujipanga kuhakikisha hawampi nafasi
ya kucheza atakavyo. Wakimuachia, anaweza kuwafunga au kumtengenezea
nafasi Jaja.
Jaja alianza msimu kwa kufunga
mabao mawili kwenye mechi ya ngao ya jamii dhidi ya Azam fc Yanga
ikishinda 3-0 . Alitukuzwa na mashabiki wa Yanga na kugeuka kuwa habari
ya mjini. Lakini hakufanikiwa kufunga kwenye mechi ya ufunguzi dhidi ya
Mtibwa Sugar.
Kwa bahati mbaya zaidi alikosa
penalti katika mechi hiyo, hivyo leo anahitaji kufuta makosa hayo na
kurudisha imani kwa mashabiki wa Yanga.
Jaja ataingia uwanjani akiwa na
wazo moja tu la kutikisa nyavu. Uchezaji wake haukubaliki kwa mashabiki
wa Yanga, lakini mabao mawili aliyoifunga Azam yalimpa sifa kubwa,
hususani goli la pili ambalo alipiga mpira kiufundi mno.
Jaja anacheza ‘kivivu’, hana
uwezo wa kupiga rangi mpira,sio mkali wa kumiliki mpira, Jaja hana kasi
uwanjani, lakini ni mtu hatari sana anapofika golini kama atapigiwa pasi
za mwisho.
Katika mechi ya Mtibwa Sugar,
hukugusa sana mpira, lakini pasi nne alizopigiwa almanusura afunge
magoli. Tatu alipiga vichwa vya hatari, lakini kipa wa Mtibwa, Said
Mohammed aliendelea kuwa katika ubora wa kuokoa hatari hizo.
Moja alifunga goli, lakini
mwamuzi alikataa akidai nahodha wa Mtibwa, Shaaban Nditi alishika kwa
mkono mpira kabla na akatoa penalti ambayo Mbrazil huyo alikosa. Kwa
takwimu hizo, unaweza kuona jinsi gani Jaja anaona lango na anajua
kujipanga maeneo sahihi.
Tegete (kushoto) amerejea tayari kwa kuanza kazi
Kama Prisons wanahitaji kushinda leo au kutoa sare, wanahitaji kuzuia mipira ya Yanga kuanzia katikati.
Uhai wa Jaja unatokana na viungo
wa kati na pembeni. Kama Mrisho Ngassa ataanza winga ya kushoto na
Saimon Msuva winga ya kulia, halafu kiungo mchezeshaji akaanza Haruna
Niyonzima na kiungo mshambuliaji (namba 10 ) akaanza Coutinho na bahati
mbaya wakawa katika kiwango chao, nina uhakika Jaja atafunga.
Bila shaka Mbuyu Twite atacheza
nafasi ya kiungo wa ulinzi, yaani mbele kidogo ya Yondani na Cannavaro.
Nyota huyu amekuwa akifanya vizuri eneo hili na mipira mirefu
inayorusha, inawasaidia sana Yanga kutengeneza hatari kwa wapinzani.
Yanga wamekuwa bora zaidi
katikati japokuwa staili ya uchezaji wa Niyonzima imebaki kuwa ile ile.
Anapenda kugeuka na kupiga pasi za nyuma , anapenda kupiga chenga na
wakati fulani hupunguza kasi ya kupanga mashambuliaji.
Niyonzima ndivyo alivyo,
kumbadilisha sio rahisi, lakini ni mtu anayeweza kupiga pasi nzuri na
zikafika maeneo sahihi. Kama hatachungwa leo, anaweza kutengeneza hatari
kubwa kwani anaweza kuwapa mipira mizuri akina Ngassa, Msuva, na
Coutinho ambao watampa pasi za mwisho au krosi nzuri mshambuliaji wa
kati, Jaja au kufunga wenyewe.
Mrisho Ngassa (kulia) ni mtu hatari sana na anapaswa kuchungwa na Prisons
Prisons wanatakiwa kuja na mpango
mkakati wa kuzuia mipira yote ya katikati. Staili ninayoona inaweza
kuwasaidia ni kutowafanya Yanga wawe huru kucheza mpira wao.
Wanatakiwa kukaba mtu kwa mtu na kurudi wengi nyuma kama timu. Haitawafaa kupaki basi, lakini timu inatakiwa kukaba kwa pamoja.
Wakipoteza mpira wanatakiwa
kurudi wote nyuma ili kuweka ngome imara ya ulinzi. Kama wataamua kupaki
basi moja kwa moja itakuwa hatari zaidi kwao kwasababu watawaruhusu
Yanga kukaa zaidi katika eneo lao. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Ikitokea hivyo, watashambuliwa sana na wanaweza kujikuta wanapoteza umakini na hatimaye kufungwa magoli mengi.
Prisons wana marali kubwa baada ya kushinda 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting
Mfumo wa kujilinda na kushambulia
kwa kushitukiza unaweza kuwasaidia zaidi Prisons. Lakini kama wataingia
na mfumo wa kucheza mpira wa wazi (open football), naamini itakuwa
ngumu kwao kutokana na mazingira halisi ya Yanga.
Nina uhakika Yanga watapiga mpira
mwingi na wana hasira za kuanza vibaya, watashambulia sana, lakini hiyo
itakuwa faida kwa Prisons kama watatumia mashambulizi ya kushitukiza.
Kama watapiga mipira mirefu
inaweza kuwasaidia kwasababu Yanga wana tatizo la kujisahau. Kama wana
mpira basi wanauchezea sana, lakini wakipokonywa na kukimbizwa kwa
mipira mirefu, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Yondani wanajikuta katika
wakati mgumu. (kumbuka mechi na Mtibwa).
Inawezekana Maximo amerekebisha
tatizo hilo, lakini mpira wa miguu ni mchezo wa makosa, wanaweza kufanya
makosa tena. Hivyo Prisons wajiandae.
Mpira umebadilika, timu yoyote inaweza kupata matokeo nyumbani na ugenini.
Prisons walishinda ugenini dhidi
ya timu ngumu ya Ruvu Shooting. Hii imewaongezea morali kubwa . Wanaweza
kushindana na kupata matokeo mazuri.
Polisi Morogoro walicheza vizuri
mno jana. Waliinyanyasa Simba hususani kipindi cha pili na kuambulia
sare ya 1-1. Wengi waliwachukulia poa, lakini wakaonesha kuwa wanaweza
kufanya lolote.
Hata Prisons ambao ni wakongwe na ligi kuu wanaweza kuwazuia Yanga leo, lakini itawabidi wafanye kazi ya ziada.
Hata historia inawahukumu wanapocheza na Yanga uwanja wa Taifa. Mechi mbili za mwisho walifungwa 3-1 na 5-0.
Licha ya kufungwa, hawakucheza
kabisa mpira. Lakini sahizi wamejijenga upya chini ya kocha David
Mwamwaja. Wana morali kubwa, wana wachezaji mchanganyiko, nadhani
wanaweza kutoa changamoto.
Yanga wanaweza kuifunga Prisons, lakini ikitokea sare au kufungwa wasishangae. Ni matokeo yanayoweza kutokea kabisa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment