Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
NAHODHA wa Polisi Morogoro
Nicholas Kabipe amefichua siri ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya Simba
katika mchezo wa raundi ya pili ya ligi kuu soka Tanzania bara iliopigwa
jana uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Simba walikuwa kwa kwanza
kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 32 kipindi cha kwanza kupitia
kwa Emmanuel Okwi, lakini Danny David Mrwanda aliisawazishia Polisi
katika dakika ya 50 kipindi cha pili.
Kabla ya mechi ya jana, Polisi
walifungwa 3-1 na Azam fc katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa wikiendi
ya septamba 20 mwaka huu uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Baada ya mechi ya jana dhidi ya
Simba, Kabipe alisema: “Kwa matokeo haya sisi tumefurahi kwasababu
tulipoteza mchezo wa kwanza. Kuna makosa yalikuwa yanatugharimu na Azam
wakatufunga magoli matatu.
“Tumerekebisha hayo makosa na
tumeweza kupata sare. Wakati wa mapumziko tukiwa nyuma kwa goli moja kwa
bila, mwalimu alituelekeza kuwa Simba wana kasi sana sehemu ya kiungo”.
“Kwahiyo akasema tunatakiwa tuwe
wengi katikati ili tusiwape nafasi ya kucheza, tuwe tunaenda kukaba watu
watatu na tulifanya hivyo, ikawezekana na tukaweza kupata sare hiyo”. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment