Monday, February 11, 2013

Papa Benedict kujiuzulu

Huko Ujerumani, msemaji wa serikali amesema kuwa anaheshimu kazi kubwa iliyofanywa na Papa huyu aliyezaliwa katika Jimbo la Bavaria la nchini humo.
Papa Benedict
Baba Mtakatifu ameelezea kwamba matatizo ya kiafya yamemfanya kutangaza kujiuzulu
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron, amemsifu Papa kwa jitihada zake za kuimarisha mahusiano baina ya Vatican na Uingereza.

Askofu mkuu wa Canterbury amesema amazipokea taarifa za kujiuzulu kwa Papa kwa huzuni mkubwa ingawa anaelewa undani wa hatua yake.
Kiongozi wa Ujeremani, Bi. Angela Merkel amesifu mchango wa Papa wa kupendekeza mjadala baina ya makanisa, waislamu na wayahudi.

Alikumbusha hotuba ya Papa alipozuru bunge la Ujerumani mnamo mwaka 2011.
Uwamuzi na hatua ya Papa Benedict XVI wa kujiuzulu mwishoni mwa mwezi huu baada ya takriban miaka minane akiongoza Kanisa Katoliki kwa hoja kuwa umri wake wa miaka 85 ni mkubwa kiasi kwamba hawezi kuendelea kuhudumu zaidi ya umri huo.

Makao makuu ya Kanisa Katoliki huko Vatican yanasema yanatarajia Papa mpya atachaguliwa kabla ya mwisho wa mwezi wa tatu, na sherehe za Pasaka.

Tabia ya kujiuzulu kwa Papa si ngeni, ingawa ni tukio jipya katika karne za hivi karibuni.
Mwandishi wa BBC mjini Roma Alan Johnston anasema habari hizi zimetokea kama radi, na kwamba hakukua natetesi yoyote juu ya uwezekano kama huu.

Msemaji wa Vatikani Father Federico Lombardi, amesema kuwa hata wasaidizi wa Papa wa karibu mno hawakuwa na fununu juu ya tukio hili.

Kakake Papa huyu mzaliwa wa Ujerumani alipewa ushauri na Daktari wake asifanye ziara nyingine yoyote ya Marekani na kwamba kwa miezi kadhaa Mtakatifu Papa amekuwa akitafakari kujiuzulu.
Akizungumza kutoka nyumbani kwake huko Regensburg, Ujerumani, Georg Ratzinger amesema kuwa Kaka yake alikuwa ameanza kupata shida ya kutembea na kwamba kujiuzulu kwake ni hatua ya kimaumbile.
Wakati wa kutawazwa kama Papa, Kadinali Joseph Ratzinger alikuwa mmojawapo wa mapapa wapya kuchaliwa akiwa mwenye umri mkubwa wa miaka 78.

Alitangazwa Papa mnamo mwezi Aprili 2005 kufuatia kifo cha marehemu John Paul wa pili.
Uongozi wake ulitokea wakati wa wimbi kali la ubakaji kulikumba kanisa katoliki katika kipindi cha miongo mingi, ubakaji uliofanywa na watawa dhidi ya watoto wavulana.

Katika taarifa yake, Mtakatifu Papa amesema: "baada ya kujichunguza binafsi na nafsi yangu mbele ya Mola wangu, nimefikia uwamuzi kua uwezo wangu na afya, ukiambatana na umri mkubwa, ni mambo yatakayokwaza jitihada zangu za kuendelea kuliongoza Kanisa Katoliki.

Kuna kipengele katika sheria ya Kanisa kinachosema kuwa kujiuzulu kwa Papa kunakubalika iwapo kitendo hicho kimefanywa kwa hiari na kwa utaratibu unaostahiki

Sokoni kwetu hapaaaa!!!

   
Hili ni soko la lililopo eneo la Ilomba jijini Mbeya, na izo ndizo ofisi za soko hilo ambapo camera yetu ilikuta mbwa zikiwa nje ya ofisi hiyo na haijulikani zipo hapo kwa lengo gani. ( Picha na Keny Pino)

Ubunifu

Maisha ni magumu kweli hadi tunalazimika kuwa wabunifu, huyu ni mbunifu wa hereni, katumia makopo ya maji

Picha na Keny Pino

Profesa Jay awavulia Kofia wakali wa MIC walipozichana kwa ufasaha nyimbo zake

Mshiriki wa kinyang’anyiro hicho, Bahati Charles Kuyela, kutoka Kigamboni akionesha ‘maukali’ yake.
Profesa Jay (kulia) na Nick Mbishi wakifurahia baada ya kunogeshwa na wakali hao.
…Wakali hao wakionesha jinsi ya kuchana mistari jukwaani baada ya washiriki hao kumaliza mpambano.
DJ Juice akipangilia ‘beat’ katika kipute hicho.
Majaji wa kipute hicho kutoka kushoto ni Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’, John Dilinga ‘DJ JD’ na Ally Mohammed ‘Baucha’ wakifuatilia kwa makini mpambano huo.
Kundi la TOT Taarab likifanya mambo baada ya kinyang’anyiro hicho.
Malkia wa mipasho, Khadija Kopa (kulia) akiserebuka na mashabiki wake ukumbini hapo.
WASHIRIKI wa kinyang’anyiro cha kumsaka ‘The Mic King’ kinachotimua vumbi kila Jumapili ndani ya Ukumbi wa Dar Live ambacho mshindi anatarajiwa kujinyakulia gari jipya la kisasa, jana usiku walimtoa jasho mkali wa rap hapa nchini, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ kwa kuchana mistari ya nyimbo zake kiufasaha.
(PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY/GPL)

WASANII WENGI WA KIBONGO WANATEGEMEA UCHAWI"...T.I.D



Mnyama TID amefunguka kuizungumzia ‘indirectly’ scandal inayomzunguka hitmaker wa Kesho, Diamond ya kupata mafanikio kwa kutumimia waganga wa kienyeji.



Kupitia Twitter Top in Dar ambaye jina lake halisi ni Khalid Mohamed alitweet kwa utani akisema, “ I really want to meet a witch doctor who can make me win big brother money ntatoa percentage we go thru a contract,Yupo?!

Tuliamua kumuuliza kama anamaanisha alichokiandika ambapo alijibu, “ am kidin mate I just heard some of them were making foolish artist look big ndo maana I make fool out it.”

Akijibu swali kama anaamini katika uchawi ama kama unaweza kumsaidia msanii asiye na kipaji afanikiwe, TID alisema, “I don’t mean nobody all I know is all this mathaf**z they don’t have talent all they have is witchcravity, huh.

AIRTEL YATOA SARE NA VIATU VYA SHULE KWA WANAFUNZI WOTE WA SHULE YA KIROMO


 Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Tanzania Dangio Kaniki akimvalisha sare za shule na viatu mwananfunzi wa shule ya msingi Kiromo zilizotolewa na Kampuni ya simu ya Airtel mwishoni mwa wiki hii.Airtel metoa msaada wa sare za shule zikiwemo Kaptura 600 , skirt 600 , mashati 1193 na viatu 728 vyote vyenye dhamani ya shilingi milioni 50 kwa shule ya msingi Kiromo.
Meneja wa uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kushoto) akimkabidhi sare za shule Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kiromo Nasib Pangahela  mwishoni mwa wiki hii, akishuhudiwa na meneja wa huduma kwa jamii (katikati) bi Hawa Bayumi.
Meneja wa uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kushoto) akimkabidhi  mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Kiromo sare za shule zilizotolewa na Kampuni ya simu ya Airtel mwishoni mwa wiki hii, akishuhudia makabidhiano hayo (wa pili kushoto) meneja wa huduma kwa jamii bi Hawa Bayumi akifuatiwa na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kiromo Nasib Pangahela,  Airtel metoa msaada wa sare za shule zikiwemo Kaptura 600 , skirt 600 , mashati 1193 na viatu 728 vyote vyenye dhamani ya shilingi milioni 50 kwa shule ya msingi Kiromo.
 Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Tanzania Dangio Kaniki  (Kulia) akimpongeza Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Kiromo (kulia) baada ya makabidhiano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki hii wakishuhudiwa na meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel Hawa Bayumi (wa pili kulia) akifuatiwa na mmoja wa wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo bi Zuwena Salumu, Airtel metoa msaada wa sare za shule zikiwemo Kaptura 600 , skirt 600 , mashati 1193 na viatu 728 vyote vyenye dhamani ya shilingi milioni 50 kwa shule ya msingi Kiromo.
 
Airtel Tanzania yatembelea shule ya Kiromo mwishoni mwa wiki hii na kukabidhi sare za shule pamoja na viatu vyenye dhamani ya shilling milioni 50. Katika msaada huo Airtel imetoa sare za shule zikiwemo Kaptura 600 , skirt 600 , mashati 1193 na viatu 728, hafla ya makabidhiano ilifanyika katika shule hiyo iliyopo Kiromo -Bagamoyo.
***  ***
 Alhamisi 10 February 2013,  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa gharama nafuu zaidi Tanzania, leo imegawa sare za shule pamoja viatu katika shule ya msingi Kiromo iliyopo Bagamoyo ikiwa ni sehumu ya shughuli zao za kusaidia jamii.

Shule ya kiromo ni moja kati ya shule zilizofaidika na mpango wa shule yetu na kuingia kwenye ukarabati wa majengo na madarasa na kubadili mazingira ya shule na kutoa vifaa vya kufundishia pamoja na computer. sasa Airtel imetoa Sare na viatu vya shule kwa wanafunzi wote shuleni hapo.

Katika kauli iliyotoleawa na kampuni ya Airtel Tanzania kupitia Meneja shughuli za kijamii bi. Hawa Bayumi alisema” Airtel imedhamiria kuendelea kuisadia shule mbalimbali kwa kutoa vifaa mbalimbali ikiwepo vya kufundishia ili kuhakikisha elimu bora inatolewa kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla. Na leo tunaendelea kuboresha shule yetu ya Kiromo kwa kutoa msaada wa uniform na viatu kwa wanafunzi.

M msaada wa sare zashule tunazoto ni pamoja na Kaptura 600 , skirt 600 , mashati 1193 na viatu 728 vyenye dhamani ya shilingi milioni 50 kwa shule ya msingi Kiromo.

Airtel Tunayo malengo ya dhati kabisa katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu hapa nchini na kuhakikisha kiwango cha ufaulu kinaongezeka na upatikanaji wa vitabu kwa wanafunzi wa shule za sekondari. 

Leo tunathibitisha dhamira yetu ya kusaidia mashule kwa kutoa sare za shule na viatu Kiromo shule ya msingi”, alisema Bayumi Airtel itaendelea kusaidia mashule kwa kutoa vitabu na vifaa mbali mbali vya kufundishia ikiwa ni sehemu ya shughuli zetu za kusaidia jamii, nia yetu ni kuwafikia shule nyingi zaidi katika mikoa yote ya Tanzania aliongeza.

Kampuni ya simu ya Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia sekta ya elimu hapa nchini. Tangu tulipoanza mradi wa “ shule yetu” mpango wa  kusaidia vitabu na vifaa vya shule , shule mbalimbali nchini zimeshafaidika na mradi huu mpaka sasa.

Kutoweka kwa mashahidi wa mashitaka kesi inayowakabili vigogo wa CHADEMA Singida kwasababisha kesi kuahirishwa


Mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya kumtolea lugha ya matusi mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mwita Waitara Mwakibe akitoka nje ya mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida baada ya kesi yao kuahirishwa leo, Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 11 mwaka huu,baada ya mashahidi wa upande wa mashitaka kuingia mitini.
Wakili wa washitakiwa vigogo wa CHADEMA Onesmo Kyauke (katikati) akiwaeleza jambo wateja wake muda mfupi baada kesi ya wateja wake kuahirishwa hadi Machi 11 mwaka huu.Vigogo hao wanaoshitakiwa kwa kumtolea lugha ya matusi mbunge wa jimbo la Iramba magharibi, Mwigullu Lameck Nchemba.  Dk.Kitila Mkumbo (kushoto) na afisa sera na utafiti, Mwita Waitara Mwakibe (kulia).(Picha na Nathaniel Limu).

Mashahidi watano wa upande wa mashitaka yanayowakabili vigogo wawili wa CHADEMA taifa, wameingia mitini na kusababisha kesi kuahirishwa kusikilizwa hadi Machi 11 mwaka huu.
Mashahidi hao walikuwa watoe ushahidi dhidi ya washitakiwa Afisa Sera na Utafiti wa CHEDEMA Makao Makuu Mwita Waitara Mwikwabe (37) na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam na Mshauri wa CHADEMA Dk.Kitila Mkumbo.
Vigogo hao wanatuhumiwa kutoa lugha ya matusi kwa mbunge wa jimbo la Iramba magharibi Mwigullu Lameck Nchemba.
Mwendesha mashitaka mwanasheria wa serikali Mary Mudulugu amedai mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida Rusth Massam, kuwa askari polisi ambaye ni mpelelezi wa kesi hiyo yupo Dar-es-salaam kitendo kilichopelekea mawasiliano baina yao,yakatike.
Amesema kutokana na mpelelezi huyo kuwa jijini Dar-es-salaam, mawasiliano na mashahidi hao watano ambao ni wa mwisho katika kesi hiyo,yamekuwa magumu na yamesababisha washindwe kufika mahakamani.
Kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo,wakili wa washitakiwa Onesmo Kyauke, aliiomba mahakama hiyo kutaja tarehe ya mwisho kwa upande wa mashitaka kuleta mashahidi wao na endapo watashindwa kuwaleta, mahakama ifunge ushahidi kwa upande wa mashitaka.

Chris Brown anusurika kifo baada ya kupata ajali ya gari akiwakimbia Paparazzi

Muimbaji machachari wa Marekani Chris Brown amenusurika baada ya kugonga gari yake katika ukuta akidai alikuwa akifuatwa na mapaparazzi .
Polisi mjini Beverly Hills wamesema mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 23 ambaye katika ajali hiyo hakujeruhiwa, alishindwa kulimudu gari lake aina ya Porsche Turbo Nyeusi  alipokuwa ajaribu kuwatoroka.
Taarifa zinasema Brown alikuwa akiendesha gari hilo mwenyewe na aligonga ukuta.
Ajali hiyo imetokea siku moja kabla ya kutolewa kwa tuzo za Grammy huko LA’s Staples Center ambapo alikuwa mmoja wa wagombea.
Mapema wiki iliyopita rekodi za kimahakama zilidai kuwa  mwezi uliopita Chris Brown alimtishia kumpiga risasi muimbaji Frank Ocean  wakati wa mapambano ya kugombea sehemu ya kuegesha gari.

Taswira za maandamano ya Chadema jana




 Picha Juu Mamia ya wakazi wa Dar es salaam walijitokeza kuunga mkono maandamano yaliyoandaliwa na chadema kupinga Uonevu wanaofanyiwa wabunge wa Upinzani Bungeni.
 Viongozi wa chadema wakiwa katika mshikamano mkubwa, wakiandamana kupinga vitendo vya uonevu vinavyofanywa na Spika na Naibu wake dhidi ya wabunge wa Upinzani.
 Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa akiwa jukwaani katika mkutano wa kulaani vitendo vya uonevu kwa wapinzani. Mkutano uliofanyika katika kiwanja cha mwembeyanga Temeke leo.
 Mbunge wa singida Magharibi-Chadema na Mnadhimu mkuu wa kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu akiongea kwenye mkutano uliofanyika Viwanja vya Mwembeyanga
 Mbunge wa Jimbo la Ubungo-Chadema,John Mnyika akiongea katika mkutano.
 Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema,Godbless Lema naye akimwaga cheche jukwaani.
 Mbunge wa iringa Mjini-Chadema, Pter Msigwa akiunguruma
 
 Mbunge wa Kawe-Chadema,Halima  Mdee amesema tukianza 2014 itakula kwetu, tuanze sasa.
 Katibu mkuu wa AFP amesema chama chao kinaunga mkono chama makini kama Chadema
 Viongozi wa Chadema wakiwa Meza kuu kutoka kushoto katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa, Mwenyekiti Mh Freeman Mbowe na naibu katibu mkuu Mh Zitto Kabwe.Picha Zote na CHADEMA

VODACOM WAENDELEA NA PROMOSHENI YA KUBORESHA MTANDAO WAO

1 
dc8de
Mtoa huduma wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Najma Rashid akiwahudumia wateja eneo la Buguruni Sokoni jijini Dar es Salaam jana wakati Vodacom Tanzania walipokuwa wakifanya promosheni ya kuwajuza wananchi pamoja na wateja wake kuwa imeboresha mtandao kwa ajili ya kuwafikia wananchi mahali popote Tanzania.

Mh.Lowassa ahudhuria mazishi ya mama yake Dr Kimei

msiba1 a23b2
Mawaziri wakuu wastaafu Mh Edward Lowassa na Mh Fredrick Sumaye wakijumuka na viongozi wengine katika msiba wa mama yake mkurugenzi mtendaji mkuu wa CRDB, Dr Kimei mwishoni mwa wiki huko Komakundi Marangu Mkoani Kilimanjaro.
msiba2 b42ff
Mh Lowassa akitia saini kitabu cha maomolezi ya kifo cha bibi Eliangichopasia, ambaye ni mama yake mkurugenzi mtendaji wa CRDB Dr Kimei.bibi huyo alifariki wakiwa na umri wa miaka 97.

msiba3 7034b
Mh Lowassa akiwapa pole Dr Kimei(katikati) na dada yake
msiba 
6634d

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka Kuzindua Kampeni ya Okoa Mtoto wa Kike Tanzania Machi 3 -2013

WAZIRI  wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa kampeni ya Okoa Mtoto wa Kike Tanzania itakayofanyika baadaye mwezi ujao wilayani Tarime, Mara. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Nyumbani Kwanza Media Group inayoratibu kampeni hiyo, Mossy Magere.Na Mpigapicha Wetu
---- 
SERIKALI imeshauriwa kuangalia upya adhabu zinazotolewa kwa watu wanaofanya vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake na watoto nchini.

Ushauri huo umetokana na kuendelea kushamiri kwa vitendo vya unyanyasaji huku vyombo na mamlaka husika vikishindwa kutoa adhabu kali kwa lengo la kukomesha.

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, aliyasema hayo mjini hapa jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa Kampeni ya Okoa Mtoto wa Kike Tanzania.

Kwa kuanzia kampeni hiyo itazinduliwa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, na baadaye kusambaa kwenye maeneo mbalimbali nchini hasa yaliyoshamiri kwa vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake na watoto.

Gaudentia, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, alisema licha ya kuwepo kwa sheria lakini bado vitendo vya unyanyasaji vimezidi kushika kasi, jambo linaloashiria kuwa adhabu zinazotolewa bado ni ndogo.

“Unyanyasaji umekuwa kwa kiwango kikubwa mno na umekuwa ukirudisha nyuma maendeleo ya wanawake nchini. Sheria zipo na watu wanapewa adhabu, lakini tunadhani kuna kila sababu ya kuangaliwa upya ili kukomesha kabisa vitendo hivi,” alisema Gaudentia. Alisema zaidi ya moja ya tatu ya wanawake nchini wameshakabiliana na ukatili wa kijinsia na kwamba, mgawanyo wa unyanyasaji ni mkubwa zaidi kwa wanawake hasa waliotalikiwa na wajane. 

“Hili ni tatizo kubwa kwani, utafiti unaonyesha asilimia 23 ya wasichana wenye umri kati ya 15 hadi 19 tayari wamejifungua, hivyo kushindwa kuendelea na masomo kwa ajili ya kuajiandaa na maisha yao ya baadaye,” alisema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Nyumbani Kwanza Media Group (NMG), Mossy Magere, alisema kampeni hiyo itazinduliwa rasmi Machi 3, mwaka huu.

Alisema wameamua kushirikiana na Gaudentia kutokana na kuwa mstari wa mbele kutetea haki za wanawake na kwamba, tatizo hilo la unyanyasaji limekuwa kubwa mkoani Mara.

Mossy alisema kampeni hiyo itakuwa endelevu na kwamba, itakwenda sambamba na uanzishwaji wa klabu za kupinga unyanyasaji katika shule mbalimbali kwa lengo kuleta usawa.

“Unyanyasaji wa kijinsia unaumiza wanawake na watoto wengi nchini, ni lazima jamii ikubali kubadilika ili kila mtu awe na furaja katika maisha badala ya wengine kufikia hatua ya kujuta kuzaliwa,” alisema Mossy.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete Afungua Semina Maalum Kwa Ajili ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mjini Dodoma


 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula (kushoto) na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana wakiingia katika ukumbi wa mikutano wa White House uliopo katika makao makuu ya CCM mjini Dodoma leo.Rais Kikwete amefungua na kuongoza semina kwaajili ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa ambayo pamoja na mambo mengine itachagua wajumbe wa Kamati kuu.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akielekeza jambo wakati wa ufunguzi wa Semina maalum kwa ajili ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa iliyofanyika mjini Dodoma katika ukumbi wa White House makao makuu leo.Kushoto anayesikiliza kwa makini ni Makamu  Mwenyekiti Mstaafu wa CCM bara Pius Msekwa.Wengine katika picha ni Rais Wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein(Wapili kushoto),Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana(wanne kushoto), na kulia ni Makamu Mwenyekiti CCm Bara Ndugu Philip Mangula.
Baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya CCM taifa wakihudhuria semina maalum iliyofunguliwa na kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa White House,Makao makuu ya CCM mjini Dodoma.Picha na Freddy Maro-IKULU

Waziri Mkuu ashiriki mjadala kuhusu juhudi za Serikali ya Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa Malaria uliofanyika Afrika Kusini


Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa anahojiwa na Mtangazaji wa habari za michezo wa Televisheni ya Super Sport Bi. Carol Tshabalala  katika mjadala kuhusu Tanzania inavyo jitahidi kupamabana na ugonjwa wa Malaria mjadala huo ulifanyika kwenye kituo cha mikutano cha Sandton kilichopo jijini Johannesburg Afrika Kusini.(picha na Chris Mfinanga).
Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisaini mpira ikiwa ni ishara ya kupambana na Malaria kwakupitia michezo kutoka kulia Mama Tunu Pinda, kushoto kwake Meneja wa mpango wa kudhibiti malaria nchini Dr. Ally Mohamed, Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Dr Seif Rashid  anayefuatia ni Mwana muziki marafu nnchini Afrika kusini na Balozi wa kupambana na ugonjwa wa malaria Bibi Yvonne Chakachaka, kushoto kwa waziri mkuu ni Mh Dr. Hamisi Kigwangalla (Mb) kulia. Waziri Mkuu alikuwa amehudhuria mjadala wa kupambana na Malaria uliofanyika katika kituo cha mikutano cha Sandton kilichopo Johannesburg Afrika Kusini.(Picha na Chris Mfinanga).
Mh Mama Tunu Pinda akisaini juu ya mpira ikiwa ni ishara ya kutumia michezo kupambana na Malaria. Kulia ni Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangaliatukio hilo na katikati ni Balozi wa kupamabana na Malaria na mwanamuziki marufu nchini Afrika kusini Yvonne Chakachaka. Mama Pinda aliongozana na waziri mkuu katika mjadala wa kupamabana na Malaria uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Sandton Johannesburg Afrika Kusini.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...