Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Anne Kilango
MWONGOZO wa ada elekezi utakaondoa utata wa utofauti wa kulipa ada
baina vyuo na vyuo nchini, unatarajiwa kukamilika na kuanza rasmi
kutumika mwezi ujao.
Kwa sasa mwongozo huo umeshaandaliwa na kinachosubiriwa ni mfumo wa
kompyuta utakaosaidia kukokotolea ada zitakazotumika katika vyuo vikuu
nchini ambao ndio utakamilika rasmi Aprili mwaka huu.
Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Anne Kilango, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Amina
Makilagi (CCM), aliyetaka kujua mchanganuo wa ada baina ya Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na endapo
unaendana na hali halisi.
Akijibu swali hilo, Kilango alikiri kuwa kumekuwa na tatizo hilo la
utofauti wa utozaji ada katika vyuo mbalimbali nchini kwa muda mrefu, na
kwa sasa Tanzania ina vyuo vikuu 53 na taasisi 21 zinazotoa shahada. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.