Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF) limefanyia marekebisho kanuni zake za michuano ya ngazi ya
klabu kwa upande wa malazi ambapo sasa timu zitachagua na kujilipia
zenyewe hoteli zinapokuwa kwenye mechi za ugenini.
Kabla ya marekebisho ya kanuni hiyo, timu ngeni ilikuwa ikilipiwa
hoteli na timu mwenyeji kwa msafara usiozidi watu 25. CAF ilikuwa
imepitisha hoteli maalumu katika kila nchi ambapo mwenyeji alitakiwa
kuziweka timu ngeni.
Kwa marekebisho hayo, Chama cha Mpira wa Miguu cha nchi mwenyeji
kitakuwa na wajibu wa kuitafutia hoteli timu ngeni iwapo tu kitaombwa
kufanya hivyo, lakini jukumu la kulipia malazi litakuwa la timu yenyewe.
Mwaka huu Tanzania inawakilishwa na timu mbili za Azam na Yanga
katika michuano ya CAF. Azam inacheza Ligi ya Mabingwa (CL) ambapo
itaanzia nyumbani Februari 15 mwaka huu kwa kuikaribisha El Merreikh ya
Sudan kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Nayo Yanga itacheza michuano ya Kombe la Shirikisho (CC), na
imepangiwa kucheza mechi ya kwanza nyumbani dhidi ya BDF IX ya Botswana.
Mechi hiyo itafanyika Februari 14 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)