Mchezaji
wa Ivory Coast Gervinho ameomba msamaha baada ya kupewa kadi nyekundu
kwa kumpiga mlinzi wa timu ya Guinea Naby Keita katika mechi ya timu
hizo mbili ilioisha 1-1.
''Nataka kuomba msamaha kwa taifa la
Ivory Coast,wachezaji wenzangu na waandalizi wa michuano ya mataifa ya
Afrika kwa kitendo hiki cha hasira'',aliandika katika mtandao wake wa
Twitter.
''Haikuwa mimi na vitendo kama hivyo havina nafasi katika viwanja vya soka'',,aliongezea.
Kulingana
na sheria za FIFA, mchezaji hukosa mechi moja anapopewa kadi nyekundu
,lakini shirikisho la Soka barani Afrika huenda likaongeza adhabu hiyo.
Kawaida
mtu hupewa marufuku ya mechi mbili katika michuano ya Afrika,lakini
adhabu hiyo inaweza kuongezwa na kufikia mechi nne iwapo kamati ya
nidhamu itahisi mchezaji huyo anahitaji kupewa adhabu kali. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment