Wednesday, August 20, 2014

ASERNAL YATOKA 0-0 NA BESIKTAS, AARON RAMSEY ALETA MAJANGA KWA KUONESHWA KADI NYEKUNDU


1408480185825_Image_galleryImage_Aaron_Ramsey

Kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey alitolewa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo wa kwanza wa mtoano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya  Besiktas
ASERNAL wamelazimisha suluhu pacha ya bila kufungana na Besiktas ya Uturuki katika mchezo wa kwanza wa mtoano wa ligi ya mabaingwa barani Ulaya uliopigwa jana usiku katika dimba la  Ataturk Stadium
Kutoka sekunde za mwanzo, almanusura Demba Ba afunge bao lakini mpira aliopiga wa adhabu ndogo uligonga mwamba na ilionekana kuwa ni mechi ambayo ingekuw ana magoli mengi. Lakini Aaron Ramsey naye aliwakosa Waturuki hao baada ya kupiga shuti lililogonga mwamba.
Kadi nyekundu ya Aaron Ramsey aliyopata dakika za majeruhi kufuatia kuoneshwa kadi mbili za njano aliwahuzunisha zaidi Asernal kutokana na ukweli kuwa anahitajika sana katika mchezo wa marudiano ndani ya dimba la Emitarates.
Besiktas, na Ba wameonekana kuwa na nia ya kuwaonesha Chelsea kuwa walifanya makosa kumuuza mshambuliaji huyo kwani alionesha kiwango kizuri. Ili kusonga mbele, Asernal wanahitaji ushindi wa bao 1-0 tu mjini London jumanne ijayo.
Silly boy: Ramsey received (left) his second yellow card for bringing down Besiktas' Oguzhan Ozyakup (right)

HARUNA SHAMTE, JABIR AZIZ, JACKSON CHOVE WASAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA MMOJA JKT RUVU

SIMBANAYANGA2
Haruna Ramadhan Shamte

MAAFANDE wa JKT Ruvu wamekamilisha usajili wa wachezaji watatu kati ya wengi waliokuwa wanafanya majaribio chini ya kocha mkuu, Fredy Felix Minziro. Beki wa kulia aliyeichezea Simba sc msimu uliopita, Haruna Ramadhan Shamte amesajiliwa na maafane hao na kusaini mkataba mwa mwaka mmoja. Pia nyota wa zamani wa Simba sc na Azam fc, Jabir Aziz ‘Stima’ ameanguka mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia klabu hiyo yenye nia ya kuonesha changamoto kubwa zaidi msimu ujao. Katika kuhakikisha lango lake linakuwa mikono salama, klabu hiyo imemsainisha mlinda mlango mzoefu, Jackson Chove mkataba wa mwaka mmoja. Wachezaji hao watatu walikuwa chini ya uangalizi wa kocha Minziro kwa muda mrefu kwa lengo la kujiridhisha na viwango vyao pamoja na suala muhimu la nidhamu.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz Wachezaji wengine waliokuwa wanafanya majaribio na klabu hiyo ni pamoja na Betram Mombeki na Henry Joseph, wote waliachwa na Simba sc mwishoni mwa msimu uliopita.
 
Jabir Aziz
Pia Athumani Idd ‘Chuji’ alijitokeza mara kadhaa katika mazoezi hayo, lakini aliondoka zake baadaye na sasa anajifua na Mwadui FC ya Shinyanga inayoshiriki ligi daraja la kwanza. Meneja wa JKT Ruvu, Frank Joel Cibaya aliwahi kukaririwa na mtandao huu akisema wachezaji wengi walioachwa na klabu kubwa za Simba na Yanga wanaomba kufanya majaribio klabuni hapo, lakini kocha Minziro yuko makini zaidi kuangalia nani anamfaa.

Cibaya alimtaja Aziz, Shamte na Chove kuwa walionesha juhudi kubwa kwa muda wote wa uangalizi, hivyo kocha amependekeza wasajiliwe rasmi kuitumikia klabu hiyo. Meneja huyo alisema wachezaji wengi wanaotoka timu kubwa huwa wanasumbua sana wanapojiunga na timu ndogo wakitaka kupata kila kitu walichokuwa wanapata Simba na Yanga.
Dirisha la usajili limeongezwa kwa siku 10 hadi Agosti 27 mwaka huu, hivyo bado maafande wana nafasi ya kuongeza au kupunguza wachezaji wanaoona hawana manufaa kwao. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na Baraka Mpenja

Tuesday, August 19, 2014

WAPENZI WA JINSIA MOJA KENYA KUPIGWA MAWE HADI KUFA...!!!

Screen Shot 2014-08-19 at 8.03.13 AM
(Nje ya bunge la Kenya. Picha na Maktaba)
 
Bunge la taifa nchini Kenya linapanga kujadili sheria ya kipekee inayopendekezakupigwa mawe hadi kufa kwa raia wa kigeni atayeshiriki mapenzi ya jinsia moja huku wazawa wakikuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

Mwandishi na mdhamini wa sheria hiyo Edward Onwong’a Nyakeriga anapendekeza kuharamishwa kwa ulawiti na kisha kuhukumiwa jela kwa wale wanaotenda kosa hilo huku akisisitiza kuwa upo umuhimu wa kuwalinda watoto na vijana ambao wanalengwa na dhulma ambazo kwa mda mrefu zinaepukwa kutokana na mabadiliko ya teknolojia na habari isiyo chujwa na watoto yatima kukosa mwakilishi pamoja na majaribio ya wanaoshiriki uhusiano wa jinsia moja kuwalea watoto ilihali wanaendeleza uhusiano wao’
 Screen Shot 2014-08-19 at 8.06.26 AM
Muswada huo wa chama cha Republican Liberty Party unaharamisha uhusiano wowote wa jinsia moja na tayari umeungwa mkono na wabunge zaidi ya 78 na wengine zaidi wanaendelea kushawishiwa. Pia spika wa Bunge Mh. Justin Muturi ameupokea na kuuwasilisha katika kamati ya sheria bungeni ambayo inatathmini kisha kutoa ripoti kwa bunge.
 Mmoja kati ya waaandishi wa vitabu maarufu nchini Kenya Binyavanga Wainaina amekua miongoni mwa waliojitokeza hadharani na kukiri kushiriki mapenzi ya jinsia moja na wakati huohuo Mashirika ya kutetea haki za wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja hivi karibuni yaliwasilisha pendekezo la kutaka Wabunge kuondoa sheria zote zinazowazuia kuishi maisha yao kama watu wengine. Muswada huo unatarajiwa kupata upinzani mkali kutoka kwa wanaotetea haki za binadamu.
Kwa upande wa Katiba ya Kenya ya mwaka 2010 imeharamisha ndoa ya jinsia moja japo haiharamishi moja kwa moja uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja ambapo pia mwezi uliopita utafiti uliofanywa na kampuni ya Ipsos Synovate umeonyesha kwamba 64% ya Wakenya wanaamini kwamba hisia za kushiriki mapenzi na jinsia sawa ni jambo la kujifunza ilihali 14% kati yao wanaamini watu hao huzaliwa walivyo.

Chanzo: Millard Ayo

UAMUZI MGUMU CCM KATIKA KAMATI KUU LEO

Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya CCM inakutana leo mchana mjini Dodoma chini ya mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete huku ikitarajiwa kufanya uamuzi mgumu wa mchakato wa Katiba.

Kikao hicho kinaketi mara ya pili katika muda mfupi, baada ya hivi karibuni kukaa jijini Dar es Salaam na kueleza kuridhishwa na mchakato huo.

Hata hivyo, safari hii kikao hicho kinaketi kukiwa na maswali lukuki ambayo hayajapata majibu: Je, Bunge la Katiba liendelee au livunjwe? Je, lisitishwe kwa muda kupisha maridhiano au la? Je, kuna umuhimu wa maridhiano? Kuna ulazima wa kuwapo Ukawa bungeni?

Akizungumzia kikao hicho, mtaalamu wa sayansi ya siasa na utawala katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Alexander Makulilo alisema jambo kubwa litakalojadiliwa katika kikao hicho ni kauli tofauti zilizotolewa na wananchi kuhusu mchakato wa kupata Katiba Mpya. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

"KAULI YA WEREMA NI YA KINAFIKI" MBATIA


Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia (kulia) akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Mosena Nyambabe.


Siku moja baada Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kueleza kuwa hakuna mwenye mamlaka kisheria kuvunja au kusitiza Bunge la Katiba, mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi amesema kauli hiyo imejaa unafiki na kwamba upo uwezekano wa kuahirisha vikao kwa muda mpaka mwafaka wa kitaifa utakapopatikana.

Mwenyekiti huyo, James Mbatia amesema kuahirisha Bunge kunawezekana kama ambavyo iliwezekana kusitishwa vikao vya Bunge hilo Aprili mwaka huu kupisha Bunge la Bajeti na kubadilishwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kinyemela kwa kuongeza idadi ya siku za Bunge la Katiba kutoka 70 hadi 90 mpaka kuwa muda wowote ambao utaonekana unafaa.

Wakati Mbatia akieleza hayo, jana waliibuka wazee wa Jiji la Dar es Salaam wakiwataka Watanzania kuyaombea makundi yanayovutana na moja likisusia vikao vya Bunge hilo vinavyoendelea mjini Dodoma, ili yakutane na yakubali kufikia mwafaka kwa pamoja.

Kauli ya Mbatia

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mbatia alisema kauli iliyotolewa juzi na Jaji Frederick Werema imejaa unafiki. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOSTI 19, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.


.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

SOMA ALICHOANDIKA MAULID KITENGE BAADA YA KUACHA KAZI ITV/ RADIO ONE

Screen Shot 2014-08-19 at 8.22.01 AM 
Maulid Kitenge yuko kwenye orodha ya Watangazaji wa muda mrefu wa michezo nchini Tanzania ambapo ujazo wa jina lake uliongezeka baada ya kuanza kufanya kazi na ITV/RadioOne zaidi ya miaka 10 iliyopita.
August 18 2014 Maulid aliandika yafuatayo kwenye page yake ya twitter >>> ‘Namshukuru sana Mungu leo nimemaliza miaka 14 ya kutumika kuwa kama mtangazaji wa michezo Radio one stereo na hakika naondoka rasmi
Mpaka asubuhi ya August 19 2014 Maulid alikua hajaandika tweet nyingine ya anakokwenda au atakachofanya baada ya kuondoka ITV/Radio One
Screen Shot 2014-08-19 at 8.16.51 AM

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WATU WEUSI WABAGULIWA KOREA KUSINI...!!!

Watu weusi wanyanyapaliwa Korea Kusini
Tangu kuanza kwa ugonjwa wa Ebola kumekuwapo na malalamiko ya watu wanaotoka Barani Afrika kutengwa kwa kutopewa huduma za kijamii nchini Korea ya kusini ikiwamo kutoruhusiwa kuingia katika Migahawa na usafiri wa umma kwa madai ya kuwa huenda wana virusi vya Ebola.

Aidha, baadhi yao wamedai watu weusi wanaposimamisha TAXI hazisimami kutokana na hofu ya virusi hivyo vya Ebola. Nimezungumza na Kijana RWEHUMBIZA KALANGALI,ambaye ni mwanafunzi anayesoma huko Korea Kusini, na hapa anaeleza hali ilivyo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

OBAMA ASIFU MAJESHI YA IRAQ NA KURD

Rais wa Marekani, Barack Obama
Rais wa Marekani Barack Obama amesema majeshi ya Iraq na yale ya Kikurd yamepiga hatua kubwa kulitwaa tena bwawa muhimu la Mosul kutoka kwa wapiganaji wa kiislamu kaskazini mwa Iraq.
Amesema wamethibitisha kwamba wanauwezo wa kufanya kazi kwa pamoja na wataendelea kuungwa mkono na majeshi ya Marekani, ambayo tayari yamefanya mashambulio Zaidi ya anga katika eneo linalokaliwa na wapiganaji wa kiislamu.

Ripoti zinasema kuwa mapambano katika juhudi za kudhibiti maeneo yanayozunguka bwawa hilo yanaendelea. Katika hatua nyingine kundi la himaya ya kiislamu linalofanya mashambulizi dhidi ya Wakurd limekanusha kwamba wapiganaji wake wamepoteza udhibiti wa bwawa hilo.

Wakati huohuo kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis amesema jumuia ya kimataifa itakuwa na haki katika kuchukua hatua dhidi ya wanamgambo hao. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Papa Amesema ni halali kuzuia kile alichokiita dhuluma ya kichokozi. Lakini ametahadharisha kuwa hatua yoyote itakayochukuliwa lazima ifanyiwe tathmini. kusimamisha na kwamba hakusema. Mwandishi wa BBC MJINI Roma Italia anasema papa Fransis hajaonesha kuunga mkono mashambulio ya anga yanayofanywa hivi sasa na Marekani dhidi ya wapiganaji hao wa kiislamu.

Na BBC

Monday, August 18, 2014

MeTL GROUP YAPATA MKOPO WA BILIONI 300/- KUTOKA RMB...!!!

signing deal
Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (Mb) (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Rand Merchant Bank (RMB), Bw. Bruce Macfarlane (wa pili kulia) wakitiliana saini ya mkopo huo wa bilioni 300 za kitanzania. Kushoto ni Makamu wa Rais wa MeTL GROUP, Vipul Kakad na kulia ni Gregory Havermahl wa RMB wakishuhudia tukio hilo la utiliaji saini wa mkopo baina ya RMB na MeTL Group.

 Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) imetiliana saini mkataba na benki ya Rand Merchant (RMB) ya Afrika Kusini utakaoiwezesha kupata mkopo wa zaidi ya sh bilioni 300. Mkataba huo umetiwa saini nchini Afrika Kusini na Ofisa Mtendaji Mkuu MeTL GROUP, Mohammed Dewji.

Akizungumza kabla ya kutiwa saini kwa mkataba huo,Dewji alisema kwamba mkataba huo wa kihistoria unatokana na RMB kuiamini kampuni yake ya MeTL tangu walipoanza mahusiano ya kibiashara mwaka 2007.

“MeTL na RMB tulianza mahusiano yetu mwaka 2007, wakati RMB ilipotukopesha dola za Marekani milioni 7.5million. Wakati huo MeTLilikuwa na bidhaa mbili tu,ngano na sukari! Toka wakati huo, MeTL imekuwa ikikua na kuongeza bidhaa zaidi.” Alisema Dewji na kuongeza kuwa mwaka jana 2013, uwezo wa MeTL wa kukopa sasa umefikia dola milioni 100. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAN U TAYARI KUMTOA ‘KAFARA’ LUIS NANI ILI KUINASA SAINI YA MARCOS ROJO

1408305526734_wps_2_MANCHESTER_ENGLAND_AUGUST
United wapo tayari kumruhusu Nani (kulia) kujiunga na Sporting Lisbon kama sehemu ya kubadilishana na beki Marcos Rojo.
MANCHESTER United imefanya mazungumzo na Sporting Lisbon ili kumjumuisha Luis Nani kama sehemu ya jaribio la kutaka kumsajili beki wake, raia wa Argentina, Marcos Rojo.
Baada ya mazungumzo baina ya wakala wa Rojo na Sporting mapema wiki hii, United wanajiandaa kumjumuisha Nani kwa mkopo.
Hata hivyo winga huyo mwenye miaka 27 anaonekana kuweka ngumu kurudi katika klabu yake hiyo ya zamani ya nchini Ureno.
Sporting wao wanahitaji kumuuza Rojo kwa paundi milioni 24, lakini wiki hii Man United waliweka mezani dau la paundi milioni 16.
Rojo, 24, aliwaomba radhi mashabiki wa Sporting katika mahojiano maalumu na TV ya klabu jumapili usiku baada ya kujaribu kulazimisha kuondoka.
Apology: Rojo said sorry to the Sporting Lisbon fans on Sunday night for attempting to force through a move

ANGALIA PICHA ZA WASANII WALIOPITIA MORO KUMFARIJI AFANDE SELE KWA MSIBA WA MAMA TUNDA...!!!

Baadhi ya Wasanii waliokuwa kwenye onesho la Kilimanjaro Music Tour lililofanyika mkoani Dodoma jana, leo walipitia nyumbani kwa Mfalme wa Rhymes a.k.a Simba Mzee a.k.a Afande Sele kumpa mkono wa pole na kumfariji kufuatia kifo cha Mzazi mwenzake Mama Tunda kilichotokea mwisho mwa wiki mjini Morogoro. Pichani ni Msanii wa Muziki wa Bongofleva atambulikae kwa jina la Shilole akimfariji Afande Sele.

Malkia wa Taarab hapa nchini, Bi Khadija Kopa akimfariji Afande Sele,pichani nyuma ya Afande Sele ni guli wa muziki wa Reggae hapa nchini, Innocent Nganyagwa.
Afande Sele akifarijiwa na mkali wa Hip Hop katika anga ya muziki wa Bongofleva, Joh Makini. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

LIPUMBA: MOYO WETU UKAWA NI WAJUMBE 14

Mwenyekiti wa CUF Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa gazeti hili.

Wakati mchakato wa Katiba mpya unaendelea mjini Dodoma na suala la theluthi mbili likisumbua vichwa vya wengi, mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ameeleza kuwa kura za wajumbe 14 kutoka Zanzibar ndizo zitauokoa au kuukwamisha mchakato huo.
Profesa Lipumba alikuwa kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi nyumbani kwake, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam kuhusu mustakabali wa mchakato wa Katiba baada ya kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia kuhudhuria vikao.
Kundi hilo lilisusia vikao Aprili 16 kwa madai kuwa Bunge lilipoteza mwelekeo kwa kuacha kujadili Rasimu ya Katiba, hasa katika suala la muundo wa serikali ya Muungano na kwamba chama tawala, CCM kiliingiza suala la serikali mbili ambalo halimo kwenye rasimu hiyo badala ya serikali tatu.
Kutokana na uamuzi wa Ukawa, ambayo inaundwa na wajumbe kutoka CUF, Chadema, NCCR Mageuzi na baadhi wa kundi la 201 kutoka taasisi mbalimbali za kijamii, kuna shaka kwamba mchakato huo huenda usifanikiwe kutokana na ukweli kuwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inataka uamuzi upitishwe na theluthi mbili ya wajumbe kutoka Bara na idadi kama hiyo kutoka Zanzibar. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATATU AGOSTI 18, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.

.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

PHIRI AONGEZA DOZI MSIMBAZI, HANS POPPE ASAKA VIFAA KIGALI, YANGA, COASTAL WATIMKIA PEMBA

DSC_0007
WEKUNDU wa Msimbazi Simba wanaendelea vyema na maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara unaotarajia kuanza kushika kasi septemba 30 mwaka huu.
Simba wamepiga kambi visiwani Zanzibar (Unguja) chini ya kocha mkuu mpya, Mzambia, Patrick Phiri akisaidiwa na kocha msaidizi, kiungo wa zamani wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Suleiman Abdallah Matola ‘Veron’ na kocha wa makipa, Idd Pazzi ‘Father’.
Simba ilianza programu ya mazoezi mara moja kwa siku hapo jana katika fukwe za bahari ya Hindi, lakini Phiri ameamua kuongeza dozi ambapo leo atafanya mazoezi mara mbili, (asubuhi na jioni).
Lengo la Phiri ni kupata muda wa kutosha wa kusuka kikosi chake akijua wazi kuwa msimu ujao atakumbana na changamoto kubwa ya kusaka ubingwa wa Tanzania bara.
Pia kocha huyo alisisitiza suala la mechi za kirafiki ili kukiona kikosi chake kwa mara ya kwanza na kujua nini cha kufanya zaidi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...