Tuesday, August 19, 2014

WAPENZI WA JINSIA MOJA KENYA KUPIGWA MAWE HADI KUFA...!!!

Screen Shot 2014-08-19 at 8.03.13 AM
(Nje ya bunge la Kenya. Picha na Maktaba)
 
Bunge la taifa nchini Kenya linapanga kujadili sheria ya kipekee inayopendekezakupigwa mawe hadi kufa kwa raia wa kigeni atayeshiriki mapenzi ya jinsia moja huku wazawa wakikuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

Mwandishi na mdhamini wa sheria hiyo Edward Onwong’a Nyakeriga anapendekeza kuharamishwa kwa ulawiti na kisha kuhukumiwa jela kwa wale wanaotenda kosa hilo huku akisisitiza kuwa upo umuhimu wa kuwalinda watoto na vijana ambao wanalengwa na dhulma ambazo kwa mda mrefu zinaepukwa kutokana na mabadiliko ya teknolojia na habari isiyo chujwa na watoto yatima kukosa mwakilishi pamoja na majaribio ya wanaoshiriki uhusiano wa jinsia moja kuwalea watoto ilihali wanaendeleza uhusiano wao’
 Screen Shot 2014-08-19 at 8.06.26 AM
Muswada huo wa chama cha Republican Liberty Party unaharamisha uhusiano wowote wa jinsia moja na tayari umeungwa mkono na wabunge zaidi ya 78 na wengine zaidi wanaendelea kushawishiwa. Pia spika wa Bunge Mh. Justin Muturi ameupokea na kuuwasilisha katika kamati ya sheria bungeni ambayo inatathmini kisha kutoa ripoti kwa bunge.
 Mmoja kati ya waaandishi wa vitabu maarufu nchini Kenya Binyavanga Wainaina amekua miongoni mwa waliojitokeza hadharani na kukiri kushiriki mapenzi ya jinsia moja na wakati huohuo Mashirika ya kutetea haki za wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja hivi karibuni yaliwasilisha pendekezo la kutaka Wabunge kuondoa sheria zote zinazowazuia kuishi maisha yao kama watu wengine. Muswada huo unatarajiwa kupata upinzani mkali kutoka kwa wanaotetea haki za binadamu.
Kwa upande wa Katiba ya Kenya ya mwaka 2010 imeharamisha ndoa ya jinsia moja japo haiharamishi moja kwa moja uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja ambapo pia mwezi uliopita utafiti uliofanywa na kampuni ya Ipsos Synovate umeonyesha kwamba 64% ya Wakenya wanaamini kwamba hisia za kushiriki mapenzi na jinsia sawa ni jambo la kujifunza ilihali 14% kati yao wanaamini watu hao huzaliwa walivyo.

Chanzo: Millard Ayo

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...