Tuesday, August 19, 2014

OBAMA ASIFU MAJESHI YA IRAQ NA KURD

Rais wa Marekani, Barack Obama
Rais wa Marekani Barack Obama amesema majeshi ya Iraq na yale ya Kikurd yamepiga hatua kubwa kulitwaa tena bwawa muhimu la Mosul kutoka kwa wapiganaji wa kiislamu kaskazini mwa Iraq.
Amesema wamethibitisha kwamba wanauwezo wa kufanya kazi kwa pamoja na wataendelea kuungwa mkono na majeshi ya Marekani, ambayo tayari yamefanya mashambulio Zaidi ya anga katika eneo linalokaliwa na wapiganaji wa kiislamu.

Ripoti zinasema kuwa mapambano katika juhudi za kudhibiti maeneo yanayozunguka bwawa hilo yanaendelea. Katika hatua nyingine kundi la himaya ya kiislamu linalofanya mashambulizi dhidi ya Wakurd limekanusha kwamba wapiganaji wake wamepoteza udhibiti wa bwawa hilo.

Wakati huohuo kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis amesema jumuia ya kimataifa itakuwa na haki katika kuchukua hatua dhidi ya wanamgambo hao. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Papa Amesema ni halali kuzuia kile alichokiita dhuluma ya kichokozi. Lakini ametahadharisha kuwa hatua yoyote itakayochukuliwa lazima ifanyiwe tathmini. kusimamisha na kwamba hakusema. Mwandishi wa BBC MJINI Roma Italia anasema papa Fransis hajaonesha kuunga mkono mashambulio ya anga yanayofanywa hivi sasa na Marekani dhidi ya wapiganaji hao wa kiislamu.

Na BBC

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...