Monday, August 18, 2014

ANGALIA PICHA ZA WASANII WALIOPITIA MORO KUMFARIJI AFANDE SELE KWA MSIBA WA MAMA TUNDA...!!!

Baadhi ya Wasanii waliokuwa kwenye onesho la Kilimanjaro Music Tour lililofanyika mkoani Dodoma jana, leo walipitia nyumbani kwa Mfalme wa Rhymes a.k.a Simba Mzee a.k.a Afande Sele kumpa mkono wa pole na kumfariji kufuatia kifo cha Mzazi mwenzake Mama Tunda kilichotokea mwisho mwa wiki mjini Morogoro. Pichani ni Msanii wa Muziki wa Bongofleva atambulikae kwa jina la Shilole akimfariji Afande Sele.

Malkia wa Taarab hapa nchini, Bi Khadija Kopa akimfariji Afande Sele,pichani nyuma ya Afande Sele ni guli wa muziki wa Reggae hapa nchini, Innocent Nganyagwa.
Afande Sele akifarijiwa na mkali wa Hip Hop katika anga ya muziki wa Bongofleva, Joh Makini. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Baadhi ya Wasanii waliokuwa kwenye onesho la Kilimanjaro Music Tour lililofanyika mkoani Dodoma jana, wakiwa katika picha ya pamoja na Afande Sele mara baada kupitia nyumbani kwa msanii huyo na kumpa mkono wa pole na kumfariji kufuatia kifo cha Mzazi mwenzake Mama Tunda kilichotokea mwisho mwa wiki mjini Morogoro.
Pichani ni mmoja Wanahabari kutoka gazeti la Mwananchi na Efm, Henry Mdimu, Joh Makini pamoja na Ben Paul wakiwa katika picha ya pamoja. Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumfariji Afande Sele.

Afande Sele aliwashukuru Marafiki, washabiki wake ndugu jamaa na Marafiki kwa umoja na mshikamano waliouonesha kwake katika kipindi hiki kigumu ambacho hakikuwahi kumtokea katika maisha yake ya kuondokewa na Mpendwa Mke/mzazi mwenzake. 

''sina maneno yanayoweza kuelezea kwa wepesi faraja, upendo na ushirikiano nilioupata kutoka kwenu, nawashukuruni sana ndugu zangu'', alimaliza kusema Afande Sele huku akionekana kuwa mwenye simanzi kubwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Picha Na Dj Choka

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...